Wamiliki wa magari mnajua hili?

Wamiliki wa magari mnajua hili?

Kudhibiti kiwango chenye kuleta madhara, wataalam watatusaidia.

Hii kampeni ni ya kuungwa mkono
Kampeni ambayo inaanza kwa kusema watatoa number plates? Bila elimu yoyoote.
 
yes ,ni wajibu wa kila nchi kulinda mazingira yake,sharia zipo ila utekelezaji wake tunaufanya kama idara ya Zima moto,wapi sheria inaagiza watu wachukuliwe documents zao?wanapokuwa wametenda kosa?hairuhusiwi polisi au yeyote yule kushukua number plates,driving licences,disc etc etc ,kosa limefanyika toa faini that's all,Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu kila mtu anakurupuka na sheria zake alizoziota.
 
Wenzetu wana vifaa na garage kwa kazi hio, pia tangu magari yao yanatengenezwa wameweka hizo standards.
Ukisikia hizo fununu jua kuna mhindi kashakuwa na garage kwa ajili hiyo. Reference gavana za mabasi. Ndiyo Tz
 
Sasa hapa TZ tunafanyia wapi? Au ndio wanakaa barabarani kukamata watu na kulets usunbufu? Hii ndio ilitakiwa iwe kazi ya sticker za nenda kwa usalama. Gari ikipewa ile sticker ina maana imequalify kutembea kwa mwaka mzima.


Fursa
 
Itakuwa jambo jema ili kunusuru afya na mazingira yetu kwa ujumla.

Hydrocarbon ni hatari sana hatujui tu


Kama lengo ni hilo kwa upande mmoja lakini kwa upande mwingine ni kutengeneza ulaji na hasa wasipozingatia kiwango cha uadilifu wa hao wakaguzi

Pendekezo:

Hilo zoezi lianze na utoaji wa elimu kwa wadau na hizo emission readings zirekodiwe centrally kuondoa chances za rushwa na uonevu kama wale wakaguzi wa fire extinguisher wanaonusa kizibo na kusema mtungi ume expire
 
Kama hujajua Serikali hii ina vita na wenye magari. Ndo maana hata askari traffick wao sasa ni kutafuta makosa tu hata kwa darubini ili tu wakutwange faini!
 
Lengo na mantiki yao ni nzuri kwa faida ya kimazingira na afya za watu wengine....walichokosea ni namna walivyowasilisha mchakato wao......nadhani inaweza kuwa ni kichaka kingine cha kuzalisha wala rushwa kama ilivyo kwa majembe na yono...,.
 
Tatizo ni utekelilezaji wake, hata hizo stickers ni ujinga tu. Ni wapi gari zinakaguliwa ili mtu apewe sticker?
 
Kuna juhudi kubwa za kuwachonganisha watanzania na dola ili yanayoendelea rufiji huko yawe escalated nchi nzima na hatimaye kuitia nchi kwenye historia ya nchi walizotoka hao wanaofanya hivyo. Unfortunately vyombo vinavyopaswa kubaini hilo na vyenyewe vimo usingizini. Let's wait and see.
 
Uvumilivu una kiwango, vyanzo vya mapato vya hovyo vitawagharimu watu.
 
mchezo huu , hauhitaji hasira , mzee siro akajifunze Nigeria ..
 
Mkuu RRONDO nimekuja kuutafuta uzi huu baada ya wewe kuutaja kwenye ile uzi wa 2017 threads. Nikushukuru kwa niaba ya watanzania wenzangu wengi wasioelewa ni kiasi gani hatujajipanga kuanza kukagua emmissions.
 
Leo nimesikia redio kuna taasisi hapa Tanzania itakuwa inakagua/inapima moshi wa magari kujua kama uko sawa kwa mazingira yetu, yaani vehicle emission standard.

Kwa nilivyosikia redioni hawa wapimaji wakiona gari lako halijafaulu viwango vyao wanatoa number plate na kukwambia ukarekebishe, gari halitaruhusiwa kutembea mpaka lirekebishwe.

Sasa nina maswali kwa wahusika natumaini masali yangu yatasaidia wengi.
1.What is the vehicle emission standard kwa Tanzania?

2.Huko tunakoagiza magari huwa mnawapa emission standard zetu ili magari yakija yakidhi hizo standard?

3.Emission standard zinatofautiana nchi na nchi na Tanzania tunanunua magari kutoka nchi mbalimbali je watawezaje kupambana na hio changamoto?

4.Magari mengi ya zamani (<2005 ) hayafikii emission standard za >2010 na wenzetu huko wana phase out taratibu hizo gari nyinyi hapa mtafanyaje na gari nyingi hapa Tanzania ni za miaka 10 au zaidi iliopita.
Mfano kuna magari yana catalytic converter na mengine hayana hasa hasa ya Japan kuanzia 2005 kushuka hili mnalichukulia vipi?

5.Gari zilizojaa 'showrooms' mmezipima kabla ya kuuziwa sisi ili tukinunua msije kuzikamata na kutoa number plate?

Wakaguzi wa haya magari naomba mjibu maswali haya natumaini mtatusaidia maanake tunakoelekea mtatoa number plates za magari mengi sana na yatabaki ya serikali yale mapya tu!

Emission standard - Wikipedia
Harufu ya rushwa inasikika
 
Back
Top Bottom