Wametapika kisha wanataka tuyale

Wametapika kisha wanataka tuyale

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
WAMETAPIKA KISHA WANATAKA TUYALE

Waswahili tunasema akukatazae kukomba mboga, anataka ushibe... Apasuaye nguo basi lazima awe fundi wa Kushona.Ukiona mtu anatapika matapishi tena anatapika mpaka nyongo, kisha badala ya

kufuta na kupiga deki, anayageukia matapishi yake na kuyaramba tena uku akiyafurahia na kisha kukukaribisha ukae ule nae, basi ujuwe mtu huyo ana matatizo ya akili.
Binadamu sisi ni sawa na

kurasa za kitabu, ukitaka kumjuwa usiangalie jarada lililo nje, unatakiwa ukifungue kitabu na kukisoma. Juzi kati tumesikia mengi kuhusiana na viongozi wetu ambao walituhamanisha kuwa kuna

nyoka tena ni mwenye sumu kali, wananchi tukaamini na kukamata magongo ili tuwe tayari kuuwa nyoka aliye hatari kutoka kwenye shimo lake.

Lakini kwa ghafla bin Vuu, walio tutangazia kuwa nyoka yu karibu kutoka ni nyoka tu wa maigizo na si yule aliyekuwa kabla ya kutoka pangoni, nyoka huyu hana sumu na hata ukimpa mtoto wako

mchanga awezi kumdhuru, japokuwa nyoka huyo ni swira (Cobra), lakini tunaaminishwa kuwa ni nyoka mpenda watu.
Binafsi sina hofu na wabongo, kwa sababu nimeona wabongo ni kabila moja la ajabu na la kipekee. Kwa kawaida watoto wote duniani wana nyongo. Ukiwafinya wanalia, ukiwatekenya wanacheka.

Lakini wabongo wao huwa hawana nyongo, hawajui kulia. Ukiwatekenya wanacheka, ukiwafinya wanacheka, ndio maana watu wanaweza kufanya lolote waliwezalo ili wapate wanayoyataka, hata kwa rafu, na wao wakahamaki lakini wakacheka tu.

Wagombea fanyeni lolote muwezalo mpaka vyama vyenu vishinde. Wabongo hawana nyongo. Ukiwatekenya wanacheka, ukiwafinya wanacheka.

Wabongo ni viumbe wa ajabu kama nilivyosema hapo juu... Mfano ukiona mtoto anamwambia mtoto mwenzie kwa jambo la kitoto, watu wazima tutasema kuwa watoto wanacheza, na hata mtoto

akimwambia baba yake kuwa gari ile ni langu au ndege ile ni yangu, baba awezi sema kuwa wewe mtoto wacha uongo, atakacho sema baba ni kumtia moyo mtoto, kuwa ndege ile ikitua nitakuletea, huyu ni mtoto anakua. Lakini tunaposikia maneno ya kitoto anaambiwa mtu mzima, basi ujuwe hapo kuna walakini.

Ili tulilonalo sasa miezi hii michache ni dogo sana kuliko ilo linalokuja kwa sababu linalokuja tutakaa nalo si chini ya miaka kumi.
Lengo langu hapa ni kuwanasua wale wanaojiona kuwa wapo katika harakati za kidemokrasia zenye lengo la kuwapatia Watanzania wote
fursa sawa wasije kuingia katika mtego huu. Pia ni kuwajulisha wanaharakati hao kuwa mabadiliko hayawezi kuja kwa kumwondoa mtu mmoja tu, bali kwa kuuong'oa mfumo wote na pahala pake kuchukuliwa na mfumo mwingine.
Neno ili ?NINGEJUWA? Siku zote huja mwisho wa safari... Na majuto ni mjukuu!
 
Team chooni dot com na upuuzi wenu pelekeni huko. Raisi ni Lowassa
 
MziziMkavu

We mziziMkavu hua napenda sana kusona nakala zako nzuri za afya kumbe nawe ni mpuuzi tu.Siwezi kuziamini tena kama unaweza kuandika utumbo namna hii.Siasa wewe hazikuhusu kapigie watu ramli huko.
 
Last edited by a moderator:
Hakurazimishi, usitake ulivyo fuata upepo naye awe hivyo ni upuzi

Hivi bado huna hata aibu kujikalia CCM MTU mzima? Nina mashaka na age yako! Au ndio wale wale mliosemwa na Twaweza?
 
Kwa hali halisi anayeandika uzi kama huu anatakiwa awe sio ndugu tu[watu wengine hawawasaidii ndugu zao hata kama wana mali excess]wa kigogo wa CCM bali ni kigogo mwenyewe au mke au mtoto wa kigogo.Kama sivyo huyu mtoa mada atakuwa haishi nchi hii.
 
Mafumbo wafumbieni wajinga werevu mwendo mchakamchaka mpaka Ikulu.
 
Kwa hali halisi anayeandika uzi kama huu anatakiwa awe sio ndugu tu[watu wengine hawawasaidii ndugu zao hata kama wana mali excess]wa kigogo wa CCM bali ni kigogo mwenyewe au mke au mtoto wa kigogo.Kama sivyo huyu mtoa mada atakuwa haishi nchi hii.

Na yawezekana wewe ndo ukawa mtanzania no. 1
 
we mzizimkavu hua napenda sana kusona nakala zako nzuri za afya kumbe nawe ni mpuuzi tu.siwezi kuziamini tena kama unaweza kuandika utumbo namna hii.siasa wewe hazikuhusu kapigie watu ramli huko.

kiongozi bora ni yupi? R.I.P. BABA mwl. Jk nyerere



 
Last edited by a moderator:
Huna uwezo wa kumnasua yoyote, so save yourself some trouble.
Kubeba box wewe na Mzee Mwanakijiji mnaona mna uwezo mkubwa ya kujua sisi malofa na nyumbu tunataka nini kuliko sisi wenyewe.
Subiri week 3 na siku 3 zijazo mtajua malofa aka nyumbu tunataka nini.
Mabadilikoooo......Lowassa.
Lowassa............Mabadiliko.
 
Last edited by a moderator:
Mzizi mkavu nilikua nakuheshim kumbe Ni mpumbavu na mjinga kiasi hii?f$$$$c&&&k
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom