Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Pole sana
Hupaswi kuwa na jazba

Mke ni dhamana yako kama ilivyo mwanao

Waliombaka mkeo pia 'wamekutukana na wewe na kukuonyesha dharau kubwa'

Hata kama utasema umuache mkeo...kama adhabu yake vipi hao walio mbaka?

Why usijue ukweli wote?

Yaani watu waje wambake mkeo na kumlawiti na wwe unaona tu bora kumuacha mkeo ndo umemaliza?

Na hao jamaa wakihonga mahakama watatoka nje free kabisa?

Nimi ningekuwa wewe ningeanza na hao watu..nijue ukweli na nihakikishe wanazikwa ndo narudi kumuadhibu wife
Subaru murua kutoka kwa the boss
 
MAAMUZI SAHIHI,KWA WAKATI SAHIHI NA SABABU SAHIHI....
hongera...kwa maamuzi ambayo yatakuweka huru na nafsi yako kwa nafasi yako kama mwanaume kwenye familia...
wacha akaziwajibikie mari zake anazoziona ni za umuhimu kuliko mume...pengine mama yake atamtafutia mume ambae atakubali kidharauriwa kwa kiasi ambacho ulikuwa unafanyiwa wewe.....
naunga mkono hoja..[emoji817] %....mkuu..
 
Pole sana
Hupaswi kuwa na jazba

Mke ni dhamana yako kama ilivyo mwanao

Waliombaka mkeo pia 'wamekutukana na wewe na kukuonyesha dharau kubwa'

Hata kama utasema umuache mkeo...kama adhabu yake vipi hao walio mbaka?

Why usijue ukweli wote?

Yaani watu waje wambake mkeo na kumlawiti na wwe unaona tu bora kumuacha mkeo ndo umemaliza?

Na hao jamaa wakihonga mahakama watatoka nje free kabisa?

Nimi ningekuwa wewe ningeanza na hao watu..nijue ukweli na nihakikishe wanazikwa ndo narudi kumuadhibu wife
Looh
Mkuu ushauri wako haufai hata kidogo. Nadhani hujawahi kuishi na mwanamke jeuri.

Anachokisema huyu jamaa nevile pablo alikitegemea sema lilikuwa na suala la muda tu ili yatimie. Sasa unamwambiaje aendelee kuwa man na kudeal na wale mafirauni wakati wametafutana wenyewe huko. Acha wafunge ama wasifungwe watajuana wenyewe lakini yeye aendelee na ustaraab wake.

Wanakera sana hawa, mtu unamwambia kuna shimo hapo mbele halafu hakusikilizi anaenda makusudi kujitumbukiza halafu unasema niingie gharama ya kumtoa!!! Acha akafie mbali tumbafuuuu kabisa.
 
Wakuu salaam,

Mimi ni mwenyeji humu ndani ila tu kutokana uzito wa habari hii niliona nije under cover kwa miaka 4 niliyokaa Jf kuna ambao tunajuana personally na ni wengi tu.

Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.

Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.

Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."

Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.

Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.

Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.

Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.

Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.

Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.

Tulikotoka na mwanamke huyu:-

Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)

Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.

Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.

Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaño yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.

Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.

Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.

Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.

Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.

Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.

Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.
kaka najua hupo kwenye kifungo kikubwa sana.huyu ni mkeo na hakuweza kupanga haya.kaa chini muombe mungu pia jaribu kuwa karibu na washauri.mrudie mkeo si kosa lake.mpokee mungu ndio mwenye jibu
 
Pole sana mkuu.mke wako na maamuzi ni yako full stop.watu wana comment hayajawakuta tuu
 
Asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu! Ameshapata funzo. Pili fahamu kuwa watoto bado wanahitaji malezi yenu. Pamoja na yote aliyokutendea msamehe, kuwa sehemu ya maumivu na mateso yake na atapona kimwili,kiroho na kisaikolojia.

Hili pigo litambadilisha na mtaanza maisha mapya. What if kama ingekuwa ni wewe ulilewa usiku wakakubaka na yeye akachukua maamuzi ya kukuacha? Ungekisikiaje? Fahamu kwamba Hali hii ndo inafanya watu wanajiua!Hakuna aliyemkamilifu! Msamehe! Mwisho nakusihi uende kwa kiongozi wako wa Dini na utapata Masada zaidi! Asante!
Nilikuwa nasoma tu nifarijike humu,,,,, ila mkuu umeniamsha,,,,,, yani mtu huyu akaanze kufunguliwa vifungu ndio ataelewa na kuamini maamuzi sahihi? Viongozi wa dini mbona hata hawaonekani siku hizi? Ya kwao yamewashinda watawezaje haya mazito!!! Kikubwa nafsi yake ndio roho iamini inachofanya ni sahihi? Kwa wakati sahihi? Ndugu yangu yalinikuta makubwa zaidi ya haya,,,,,, ila baadhi ya walimwengu kama baadhi ya wachangiaji humu walinipa nguvu nikasimama na ninalea wanangu bila kutetereka japo watoto wapo kwa wazazi,,,,, baadhi ya wanawake hapana wanaumiza sana vichwa,,,,,,, anachofanya huyu anapumua hapa pressure ikipungua atafanya maamuzi sahihi kabisa!
 
Mimi nimekimbilia nikataka niandike mwandishi kakopi na kupesti ndo naona ni lile bandiko la 2015. Tupatiwe Mrejesho sasa. Au alijiua?
 
Wanawake western education inawacorrupt na ndio maana siku hizi ndoa chache sana, hata ukioa kuacha ni dkk mbili tu. Hawana adabu, wamejaa dharau na usiombe kipata chako kikawa kidogoa chake kikubwa balaa kabisa.

Ndio maana zamani wazee walikua wanawaachisha kazi wawe mama wanyumbani tu.
 
Ingawa stori nyingi za humu ndani ni chai....


Umeongra meeeeeengi lakini ukiangalia ulichokiandika ni hasira ya pesa/ madili /mafanikio ya mkeo ndio yanayokutesa

Na umetumia kubakwa kwake kama sababu


Nikirudi kwa wanawake...mnachochagua waume chagueni wanaume sio tu wanaowapenda kwa dhati kiasi cha kuwa tayari kusupport ndoto zenu. ..watakawaelewa..... na kujitoa kwenu kwa hali na mali.....mwisho mhakikishe Nyumba yenu iwe na mawasiliano

Kwanza mwanamke hachagui mume,pili Kiongoz ni rahisi kunzungumzia kitu kama wew sio muhusika,na tatu mambo ya ndoa ni makubwa kuliko unavofikil,na kweny ndoa amna kitu kinaumiza kama mwenzi anakuficha mambo flan flan,ur so immature unaposema kwamb utajiri na mafanikio ya mke,hakuna kitu, kweny familia mke na mume ni mwili mmoja ukitengeneza tabaka unauseparate mwili na sio mmoja tena,uyo mwanamke anatakiwa ajifunze ndoa si kama unaenda sokon unafany unachkita,atakiwa aombe msamahaa kwa mume wake,na wajenge jinsi watakavoishi kila MTU na Mali zake au ziwe za familia
 
Mkuu kule wanakula na kulala bure unawaacha watoke halafu unakuwa unamtafuta mmoja baada ya mwingine hadi unawamaliza wote!
Msimpotoshe kama ingekuwa amekuta tukio akawamaliza sawa,ila sasa atahesabika mhalifu,mwisho Wa siku familia inapata tabu.achia sheria,move on.
 
Huwa nashangaa sana inapofika kwenye kumhukumu mwanamke kila mtu anataka kutupa jiwe wa kwanza. Najiuliza mara ngapi mwanaume mkewe anamsihi na kumuonya na hamsikilizi katu katu. Ila yakimpata majanga jamii yote inategemea mwanamke kusimama hapo.

Mara ngapi mwanaume mzinzi na mlevi ana anapata ajali na mke anauguza kwa kuogesha na kubadili hata bed pans? Mara ngapi mwanaume mleviii anamtesa mkewe na anapokaanga ini mkewe analaumiwa kwa kushindwa kummudu na 'kuua' mume.

Mimi nakulaumu kwa kushindwa kumlinda mkeo. Mkeo anatoka nyumbani anaenda huko huna habari hadi giza linafika. Hebu mpe support mkewe acha mambo ya aibu. Unajikomoa na wewe hapo
Ww Akil hauna..... Inaonekana ndo wale wale.... Unataka amulinde amekuwa bodigadi?... ....acha upuuz ww
 
Ingawa stori nyingi za humu ndani ni chai....


Umeongra meeeeeengi lakini ukiangalia ulichokiandika ni hasira ya pesa/ madili /mafanikio ya mkeo ndio yanayokutesa

Na umetumia kubakwa kwake kama sababu


Nikirudi kwa wanawake...mnachochagua waume chagueni wanaume sio tu wanaowapenda kwa dhati kiasi cha kuwa tayari kusupport ndoto zenu. ..watakawaelewa..... na kujitoa kwenu kwa hali na mali.....mwisho mhakikishe Nyumba yenu iwe na mawasiliano

UNAZUNGUMZIA MAFANIKIO YAPI MKUU?
- Mafanikio ya kurudi nyumbani saa 6?
- Mafanikio ya kusoma kozi 2 za usiku?
- Mafanikio ya kufanya vitu kwa siri?

Au urithi!!!
Mbona wanaume wengi wanaachiwa Mali na maisha yanaendelea! Kwanini kwa mwanamke iwe tofauti?

Lengo la kuanzisha familia lilikuwa ni nini? Mtafikiaje malengo kama hakuna maelewano na miongozo haifuatwi?

Nyumba ya mumeo/yenu sio geto!
Lazima itunzwe na kuheshimiwa, mume ni kama Rais na mke ni Makamu katika familia yenu. Itakuwaje kama mke sio mtiifu kwa mkuu wake?
Mtaiendeshaje familia!

Au ndio haki sawa?!
Haki sawa ikiwepo, ndio amani itoweke na kila mtu ajiamulie mambo yake?

Kama mke anafikiri yeye ni bora zaidi
na hawezi kuongozwa na mwanaume kwanini alikubali kuingia kwenye ndoa?

Hata wanyama wana miongozo katika kaya zao, Angalia ngombe au simba dume anajijua yeye ni dume na simba jike anautambua uwepo wa dume.

Mleta mada anaweza kuonekana mbaya kwa maamuzi yake...
Lakini kwa historia ya mkewe inaonyesha ana makosa mengi na ya kujitakia + kesi nyingi zinaonyesha wanawake ndio huanza kuleta shida.
 
Excellent 100% hata mimi naelekea huko huko mkuu..............kuna wanawake hawabadiliki kamwe...yaani nimejiona mwenyewe 100%....Well Done!...Any updates???
 
Back
Top Bottom