Wamejitolea kufa kwa ajili yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamejitolea kufa kwa ajili yetu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kasinge, Aug 17, 2012.

 1. k

  kasinge JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kuna wanaharakati ambao siwezi kujaji kama wanatumiwa na vyama vya siasa au la, ila wameonekana kutoa maisha yao REHANI kusema kweli yao. Nambari moja namuweka Saed Kubenea ambaye mbali na kumwagiwa tindikali na kutishiwa kifo, bado ameendelea kutoa habari ambazo zinahatarisha maisha yake binafsi. Wapo wengine ambao mnawajua nadhani mtawataja (na hawaonyeshi dalili ya interest kugombea vyeo) lakini mbali ya kutishiwa wameendelea kutema cheche.
  SWALI NI ni je sisi tunawasaport vipi kuona taifa letu linakombolewa? Tumejitoa nara ngapi kusema ukweli tunaojua? Nadhani roho ya UBINAFSI inatutafuna, hatuko tayari kusema kweli, bali kusema hata uongo mradi tupewe chochote na wanasiasa wapumbavu wanochumia matumbo yao. Kule Aljeria, kijana mmoja alijitoa mhanga kwa kujichoma moto na maandamano yalisambaa nchi nzima na Ben Ali akaondoka madarakani. Kitendo cha wanaharati hawa kujitoa, ni sawa na kujichoma moto. Nadhani wakati ni huu kwetu sote wasio wachumia tumbo kutoa kweli zetu na kuwa nyuma ya wanaharakati. Naomba kuwasilisha.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Godbless J. E. Lema
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Alifanya hivyo ni mmoja tu katika dunia hii na hata kuja tokea mwingine, na huyo Yesu.
   
 4. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  USITUMIE HOMILIA ili kushawishi watu , watu huchukulia kama utamu wa injili.
  nakuunga mkono sana azimio lako na nimelipenda sana. maana uchungu uliokuwa nao ni sawa sawa kwa kila mwanaharakati aishie tanzania. wote tungekuwa na moyo wako basi tungefanya makuu makubwa sana kuliko hata Libya, Misri na Tunisia. ona walimu wameanza lakini njaa kali imewaponza, madocta wameanza lakini woga ukawaponza. sasa kuihakikishia selikali kama tupo serious, tuanzishe mtandao na kuwasiliana

  . lazima tujikusanye watu kama mia tano kwa siku moja na tukajazane pale Posta mpya halafu tunakesha pale mpaka asubuhi. basi tukianza siku moja utakuta tunajikuta tunajazana kila siku na kuanza kusambaza madai yetu. lazima tuikomboa nchi hii na iwe mikononi mwetu. Ona walivyoiba twiga na kumpelekea mwarabu! ona bajeti za wizi zinavyowekwa kwa mabilioni halafu pesa huingia mikononi mwa watu binafsi

  . Ona wabunge wanavyodai rushwa hadharani bila ya woga. Ona pesa za serikali za mitaa zinavyoliwa na mpaka mkaguzi mkuu wa serikali kalipua mabilioni yalioibiwa lakini wezi hawachukuliwi hatu. Ni sawa jamani baada ya miaka 50 ya uhuru shule za msingi hazina flush toilets nchini nzima? huo ndio wizi wa serikali za mitaa unavyorudisha nyuma maendeleo ya jamii.
   
 5. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Rate loading.............................
   
Loading...