SI KWELI Wambura amesema hivi kuhusu report ya CNN?

SI KWELI Wambura amesema hivi kuhusu report ya CNN?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Nukuu.jpg
 
Tunachokijua
Inspekta Jenerali wa Polisi, Camilius Wambura ni mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania.

Novemba 21, 2025 kituo cha habari cha CNN kilichapisha makala yake kuelezea mambo yaliyotokea Oktoba 29, 2025 ikionesha madhila yaliyowakuta wananchi.

Madai

Mdau amewasilisha grafiki inayoonekana kuwa na picha ya IGP Wambura kikiambatana na ujumbe unaodaiwa kuwa ni nukuu yake. Ujumbe huo unasomeka;

We have reviewed the video aired by CNN and we have concluded that they were most likely AI-generated. No such incidents have ever ccoured or been reported here in Tanzania, We therefore expect an apology"

Ikiwa na maanda kuwa;

Tumepitia video zilizorushwa na CNN na tumehitimisha kwamba kuna uwezekano mkubwa zilitokana na akili bandia (AI). Hakuna matukio kama hayo ambayo yamewahi kutokea au kuripotiwa hapa Tanzania. Kwa hivyo tunatarajia msamaha

Uhalisia wa nukuu hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo huru za kidigitali umejirirdhisha kuwa kauli ama Nukuu hiyo haijatolewa na IGP Wambura.

Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kingine kilichochapisha taarifa hiyo kwa siku hiyo na pia hakuna kumbukumbu zinazoonesha kuwa IGP alizungumza tarehe Novemba 23, 2025.

Kuhusu suala la video za CNN, msemaji wa serikali Gerson Msigwa alitoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa wameona makala hiyo na wanaendelea na ufuatiliaji kisha watakuja na ripoti yao.

Aidha Novemba 23, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari msemaji huyo alieleza kuwa bado ufuatiliaji unaendelea na hivyo kuwataka CNN kuitafuta serikali ili iwape taarifa za upande wao.
Back
Top Bottom