Wamasai, Wasukuma sasa imetosha, karne hii ya 21 muache kutembeza mifugo nchi nzima

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,335
24,232
Naliangalia suala la Ngorongoro, Loliondo, Handeni na sasa huko Songea, Katavi na hata wale waliovurumishwa bonde la Ihefu kwa jicho tofauti.

Imefika muda wenzetu hawa Waasaai, na siye wasukuma na jamii za kifugaji, inabidi kubadilika na wakati.
Watu wanaisi karne ya 17 kwa kutembeza mifugo aporini na hata kwenye mashamba ya wakulima.
ini tutabadilika?

Mifugo yote inaishi kwa msimu, inanenepa wakati wa mvua na kukonda hadi kufa wakati wa kingazi.
Miaa nenda rudi hali ni hii.
Lini tutabadilika?

Imefika sasa ni wakati mfugo itunzwe kitaalam ili malisho ywe yanapatikana mwaka mzima baada ya kuvuna nyasi na kuwepo almost 70 range rearing.
Tubadilike.
 
Imefika muda wenzetu hawa Waasaai, na siye wasukuma na jamii za kifugaji, inabidi kubadilika na wakati.
Watu wanaisi karne ya 17 kwa kutembeza mifugo aporini na hata kwenye mashamba ya wakulima...
Finn/Saami hadi leo maisha yao yanategemes mifugo ya reindeer ilhali nchi wanazoishi ni tajiri na zipo mbali sana kimaendeleo.
 
Waulize hao waFinn anaofuga wanalisha mifugo yao hadi viungani mwa helsinki?
Loliondo na Ngorongoro yapo viungani mwa Daresalame? Halafu utakuta na wewe una ving’ombe vyako viwili vitatu unaviachia tu mtaani kila siku ndani ya Dar kuchafua mazingira. Huna hoja wewe.
 
Loliondo na Ngorongoro yapo viungani mwa Daresalame? Halafu utakuta na wewe una ving’ombe vyako viwili vitatu unaviachia tu mtaani kila siku ndani ya Dar kuchafua mazingira. Huna hoja wewe.
usifananishe Finn na Ngorongoro,wenzetu kwenye ufugaji wa kisasa na sisi ni kama mbigu na ardhi,ni kama kufananisha ufugaji wa kimasai na ufugaji wanaofanya ASAS ,wamasai wanafunga ng'ombe kama wanafuga mbwa za kienyeji vile,dunia imebadilika na wao wabadilike tunakoenda hata mapori yataisha.
 
Acha waendelee kufanya hivo , wakibadilika tuu bei ya nyama itapaa...
 
usifananishe Finn na Ngorongoro,wenzetu kwenye ufugaji wa kisasa na sisi ni kama mbigu na ardhi,ni kama kufananisha ufugaji wa kimasai na ufugaji wanaofanya ASAS ,wamasai wanafunga ng'ombe kama nwanafuga mbwa za kienyeji vile,dunia imebadilika na wao wabadilike tunakoenda hata mapori yataisha.
Wamasai na Saami wote ni jamii za wafugaji kiasilia, na wanatumia maeneo makubwa ya malisho kwa mifugo yao.
 
usifananishe Finn na Ngorongoro,wenzetu kwenye ufugaji wa kisasa na sisi ni kama mbigu na ardhi,ni kama kufananisha ufugaji wa kimasai na ufugaji wanaofanya ASAS ,wamasai wanafunga ng'ombe kama wanafuga mbwa za kienyeji vile,dunia imebadilika na wao wabadilike tunakoenda hata mapori yataisha.
Mkuu kuna wanaoabudu wazungu na kufikiri kila kitu ni cha kuiga.
 
Mkianzisha mashamba mapya huwa mnakata miti.
Ng'ombe hali miti anakula nyasi

Mnalima mpaka kwenye vyanzo vya mito.
Kama unapendekeza sisi makabila ya wafugaji tusihamehame na nyinyi wakulima msianzishe mashamba mapya.
 
Yani wamasai wamekua gumzo,huko site kwetu kutwa wamasai na ng'ombe zao alafu makundi ma kubwa na ng'ombe wakubwa wenye mapembe ya kutisha ,watu wameshaanza kukaa wao hata hawajali,wanaboa sana kwakweli dawa yao ni kuwawekea fence
 
Mtoa mada una hoja ya msingi. Haya makabila makuu mawili, ifikie wakati yabadilike. Yaani wakiingia tu sehemu, lazima pawe jangwa baada ya miaka michache baadaye!

Hayo maisha yao ya kuhama hama na ng'ombe kwa ajili ya malisho, ni kweli yamepitwa na wakati! Na yanasabisha migogoro isiyo ya lazima, lakini pia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Wafuge kisasa mifugo michache, kwa matokeo makubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom