Wamarekani Wanawezaje kumtoa RAIS aliyeko madarakani kwa Ballot Paper? Yaani Rais ana CIA, FBI, Polisi na Jeshi lakini Rais anakaa Term 1

Ama kweli nimeamini hapa hakuna mtu ninayeongea naye kwa hoja.

Kwahiyo corona inaondolewa kwa nguvu ya kijeshi?
Nadhani ni wewe tu miongoni mwa watu wote duniani usiyefikiri kwamba korona inahitaji nguvu ya kijeshi kuiondoa. Na kwa vile Tanzania imeifyekelea mbali, basi kijeshi sisi ni "hyperpower" kuliko nchi yako ya Marekani.
 
sio tena kwamba corona imeondoka Tz kwa maombi ya kufunga nakusali kama viongozi wanavyotuaminisha?

Tushike lipi mkuu maana huku mtaani kwetu hatukuona jeshi mtaani kipindi cha corona bali kipindi cha uchaguzi walijaa kila kona.
 
Huko Tanganyika Rais anayapelekesha majeshi kama gari-moshi.

Akisema nyuma geuka, yote yanageuka mzobe mzobe kama misukule.

Vyombo vya ulinzi "vimesiasishwa" na kuwa vyama vya siasa vyenye magwanda.

Either security services have been politicized OR politics have been militarized.

Ni mwendo wa upolisi polisi tu. Hata ukijamba mkuu wa wilaya anatuma vikosi vije vikudhibiti.

Nchi zilizostaarabika kisiasa na kijamii, polisi sio mali ya Rais au mali ya chama. Rais hana mamlaka ya kutumia polisi hovyo hovyo kwa utashi wake tu anavyojisikia.

Huko Danganyika Republic, Rais anaamrisha mpaka jeshi lishambulie wananchi kwa risasi. It is terrific!
Ndiyo maana Rais ana cheo cha Amiri Jeshi Mkuu. Halafu, nilisikia wimbo huko eti fulani, fulani "wapelekeshe mchakamchaka." Mwendo wenyewe si ndio huo mmeuona kwa Dkt. wa Kemia? Na huo ni mwanzo tu. Wazembe, wala-rushwa, 'wasanii,' mafisadi, wahujumu-uchumi, wapiga-dili, wavurugaji, wazushi, waongo, vibaraka, madalali, makuwadi, muminina wa mabeberu & mabepari na wapinga kila kitu hawana nafasi katika utawala wake.
 
sio tena kwamba corona imeondoka Tz kwa maombi ya kufunga nakusali kama viongozi wanavyotuaminisha?

Tushike lipi mkuu maana huku mtaani kwetu hatukuona jeshi mtaani kipindi cha corona bali kipindi cha uchaguzi walijaa kila kona.
Kama umechanganyikiwa, basi itoshe tu kusema kwamba korona out, au vipi?
 
Kweli kabisa. Kule serikali na dola ni vitu viwili tofauti.
Kuna mtu aliwahi kuniambia humu kwamba Rais wa Marekani ni mkuu wa majeshi yote ya polisi yaliyopo Marekani.

Kucheka nikashindwa. Kushangaa nikashindwa.

Nilipotaka kumwelewesha na kumuelimisha, akashupaza shingo kwa ubishi na kuanza kudai najifanya najua/ mjuaji.

Nikamwuliza ni kitu gani nimejifanya nakijua ilhali sikijui, hakuwa na jibu!

Pata picha ya watu waliopo JF....
 
Tumemchinjia baharini Trump.

Kura zinahesabiwa, sheria zinaheshimiwa, mifumo inq nguvu, watu wanajua haki zao.
 
Ndiyo maana Rais ana cheo cha Amiri Jeshi Mkuu. Halafu, nilisikia wimbo huko eti fulani, fulani "wapelekeshe mchakamchaka." Mwendo wenyewe si ndio huo mmeuona kwa Dkt. wa Kemia? Na huo ni mwanzo tu. Wazembe, wala-rushwa, 'wasanii,' mafisadi, wahujumu-uchumi, wapiga-dili, wavurugaji, wazushi, waongo, vibaraka, madalali, makuwadi, muminina wa mabeberu & mabepari na wapinga kila kitu hawana nafasi katika utawala wake.
Naona unajifurahisha na ngonjera zako za kimagufuli za hapa na pale.

Fanya kazi halali uache kubabaika mitandaoni kwa ujira kiduchu wa kutetea wahalifu.
 
Unajifurahisha mwenyewe na ngonjera zako za kimagufuli za hapa na pale.

Fanya kazi halali uache kubabaika mitandaoni kwa ujira kiduchu wa kutetea wahalifu.
Na yako hii ingepaswa kuwa taarab, ila tu tatizo haina mahadhi na vina kama tulivyozoea lahani za watu wa mwambao.
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia humu kwamba Rais wa Marekani ni mkuu wa majeshi yote ya polisi yaliyopo Marekani.

Kucheka nikashindwa. Kushangaa nikashindwa.

Nilipotaka kumwelewesha na kumuelimisha, akashupaza shingo kwa ubishi na kuanza kudai najifanya najua/ mjuaji.

Nikamwuliza ni kitu gani nimejifanya nakijua ilhali sikijui, hakuwa na jibu!

Pata picha ya watu waliopo JF....
Yaani ni ngumu saana kukuelewa, hasa akitumia uzoefu wa hizi nchi zetu.
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia humu kwamba Rais wa Marekani ni mkuu wa majeshi yote ya polisi yaliyopo Marekani.

Kucheka nikashindwa. Kushangaa nikashindwa.

Nilipotaka kumwelewesha na kumuelimisha, akashupaza shingo kwa ubishi na kuanza kudai najifanya najua/ mjuaji.

Nikamwuliza ni kitu gani nimejifanya nakijua ilhali sikijui, hakuwa na jibu!

Pata picha ya watu waliopo JF....
Unaweza kujibu mada kwa hisia , wakati mada uwezo wake ni kufikiri.

Utawala wa Marekani hakuna ambaye ni mgeni, lakini watu wanataka uelewa kule nako kuna mtawala lakini kufanya mambo ya ajabu hafanyi!!

Hapa kwetu spika mjinga na mahakama ndio mazombe. Yani mtu anataka huruma kama elimu yake kaokota. Uwezi kukuta marekani ujinga huu.

Yani rais kachika remote anapunguza sauti na kuongeza.
 
Wenzetu hata ukiwa na mchepuko tu una hatari ya kutolewa labda wakusamehe ila ukirudia tu out hawana msalie mtume.
Hapa kwetu unakuta mgombea ubunge kazaa mpaka na housegel plus shemeji plus binamu. Nini mchepuko.
 
Back
Top Bottom