Wamakonde noma!

Huu sasa upuuzi. Kila yakinguduliwa mafuta au gesi watu wanataka nchi yao. Ajabu watu hao hao wamefaidi raslimali nyingine kama madini na mbuga za wanyama vilivyoko mikoa mingine bila malalamiko. Ingawa tunajua mnasumbuliwa na umaskini na ujinga, tusiendekeze njaa na ujuha wa changu changu chako chetu au chako kitamu changu kichungu. Mtwara hawajanyimwa fursa ya kufaidika na gesi bali ukweli kuwa hakuna miundombinu ya kufanikisha uuzaji wa gesi husika. Ni ajabu kuwa kila mjinga anadhani yakigunduliwa mafuta au gesi basi sehemu yake itageuka Dubai overnight bila hata mipango!
Mkuu nadhani hujaelewa madai ya msingi ya wamakonde, viwanda na miundombinu ya kuprocess gasi vijengwe Mtwara - then safirisheni hadi Butiama. Hatujaona dhahabu ikachimbwa Bulyanhulu ikaletwa kusafishwa DSM. Wamakonde tunatamani sana kwenda kula sikukuu hizi kwetu, lakini mvua hizi baahhh ....siku 3 kufika Mtwara. Kama bandari ipo ni kuiboresha tu, barabara ya kusini haiishi toka niko mtoto napelekwa jando mpaka sasaiv na mi naitwa baba, reli waling'oa. WHY ALWAYS KUSINI TU????
 
Father of All, bila shaka watasema wewe mchaga. Ila wangepaswa kujua hata vinu vya gesi vikiwekwa mtwara its not a guarantee ya maendeleo. Kwani kwenye migodi kote wameendelea. Tatizo hapa ni kwamba tunachangamoto juu ya umiliki na ugawanaji wa rasili mali zetu
 
Last edited by a moderator:
huu ni ujinga wa kutupa. kwani mtwara ni ardhi ya wamakonde peke yao? ujinga gani huu, polisi wakiwapiga hata hawa tutawalaumu? kwani hapa dsm gesi si inakuja kwaajili ya kuiongezea thamani ili tupate hela za nchi, hela itakayotumika kwa manufaa ya watz wote including wamakonde? ardhi ni mali ya umma, vilivyoko chini yake si vya wananchi ni vya umma wote, na serikali ndio yenye mamlaka navyo. polisi kamata hao watu wanatuharibia siku. wajinga sana hao.

Nahisi ungewauliza wenyewe basi wangekuwa na jina muafaka kwako!
 
Father of All, bila shaka watasema wewe mchaga. Ila wangepaswa kujua hata vinu vya gesi vikiwekwa mtwara its not a guarantee ya maendeleo. Kwani kwenye migodi kote wameendelea. Tatizo hapa ni kwamba tunachangamoto juu ya umiliki na ugawanaji wa rasili mali zetu
what do you mean by '' UMILIKI" tuache ujinga jamani. kule mtwara ardhi karibia yote kwa sasa wanamiliki watu wa mikoa mingine wameenda kununua halafu wakarudi makwao kwasababu wanajua kutokana na gesi ardhi pale itakuwa na thamani sana badae, wachaga wamejaa kule wanatafuta maisha, watu makabila yote wamejaa kule, sasa hawa wacheza ngoma na wacheza bao ndo leo wanakuja kujifanya kusema gesi ni ya kwao? kwani nani anamiliki? na kama unasema mgawanyo, kivipi? kwani gesi ikiuzwa dsm si inaingia kwenye pato la taifa ambalo kila mkoa utafaidika? inakuwaje mkoa mmoja ambao kisheria hawamiliki resources zilizoko chini ya ardhi wakasema ni mali ya wamakonde? hivi polisi wameishiwa virungu vya kuwatandika hawa mbuzi mawe?
 
Ndugu Ubungoubungo, kama nchi ingeongozwa kwa jazba namna hiyo pengine tusingefika hapa. Tungekuwa pabaya. Tunapozungumzia umiliki hapa tunamaanisha kila mtanzanoa anayohaki juu ya rasilimali zilizojuu ya ardhi hii. Sasa katika hali ya kawaida mtu yeyote angependa kunufaika na kile anachokiona kwa karibu. Mathalani mchaga wa Kilimanjaro angependa sana kuona anavyofaidika na mlima kilimanjaro kuliko na ziwa Tanganyika. Sasa kunapokuwa na sera mbovu wananchi hawaoni au hawajui namna wanavyofaidika na rasilimali zao. Kunapokuwa na sera nzuri, wananchi wakaona manufaa yake, hapo tunasema wanamiliki sawa sawa rasilimali zao. Najaribu kutafakari ujinga nlioambiwa niache hapa. .
 
kuna maswali mengi unahitaji kujibu hapa;-
  1. sera mbovu ni zipi kwenye hili suala la gesi, hasa kujenga bomba toka mtwara hadi dsm ili gesi iuzwe viwandani na kutengeneza umeme.
  2. unaposema kila mtz anayo haki kumiliki rasilimali zilizoko juu ya nchi hii unamaana gani?, kwani mtu anaweza kumiliki rasilimali zilizoko chini ya ardhi (gas, mafuta, madini etc) bila kufuata utaratibu uliowekwa na sheria?, kwa tz ardhi ni mali ya umma, tunaweza kukodi tu rais ni mdhamini, ukikodishwa ardhi na serikali iwe iwa miaka yeyote ile hadi 99 haumiliki kilichoko chini yake kama vile madini, gas etc. sasa je? umiliki wa rasilimali za nchi ya tz haujawa regulated na sheria na sheria haitakiwi kufuatwa? au tunamiliki vipi? kila mtu anatakiwa kufanya apendavyo ili apate chake? au kuna utaratibu fulani ambao watu watapata haki ya kumiliki? haki hii iko moja kwa moja au ina conditions?
  3. mchaga wa kilimanjaro anapenda kufaidika na mlima kilimanjaro, je? mchaga wa mtwara na mchaga wa sumbawanga? sasa watasemaje gas ni ya wamakonde si ya wakwere?
 
napenda hao waliochora picha wakamatwe kwa kuhujumu uchumi au hata kutishia usalama wa nchi...manake wanaonyesha wanataka kulipasua au kuliharibu bomba kitu ambacho litalipuka na kama limeshaunganishwa gas nchi itaathirika sana kwa hasara kubwa.
 
Kwa matazamo wangu. Naona tatizo ni kutoweka kwa Imani toka kwa Wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kumekua na mfululizo wa madudu yanayofanywa na viongozi wa serikali na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya hao wahalifu.

Haya ni matunda ya usanii unaofanyika serikalini, kwasasa hata ije sera nzuri bado wananchi wataona ni "changa la macho"

Nchi imefikia mahali hata raisi mwenyewe haaminiki.

Tunaelekea Nigeria sasa kama viongozi wataendelea kupuuza hizi vuguvugu zilioanza toka kwa wananchi.

Muda si mrefu utasikia wapogolo nao wanafunga njia ya mikumi ili tugawane mapato.
 
Matumizi ya ges ni kuzalisha umeme lakini pia inaweza kutumika majumbani na viwandani. inawezekana kujenga kituo cha kuzalisha umeme Mtwara na kusambaza umeme huo sehem nyingine ya nchi kwa cable kama ilivyo umeme wa maji kule kidatu au mtera lakini tutakuwa tumei-under utilize hiyo gesi kuliko ikisafilishwa hadi sehemu yenye matumizi makubwa kama Dar na kufanya mambo mengi zaidi huko.

Angalizo kwa watu wa Mtwara; kugundulika kwa gesi huko (ama uzalishaji wa nishati) hakuna maana kuwa wana mtwara automatically mtakuwa matajiri, bali kikubwa ni umiliki wa rasilimali hiyo... kwa sasa na kwa katiba yetu, rasilimali yoyote, na popote ilipo, inamilikiwa na watanzania kwa kupitia serikali yao. Mafanikio au kutofanikiwa kutatokana na jinsi gani serikali itamiliki rasilimali hii kwa niaba ya watanzania. tuna rasilimali nyingi, mfano dhahabu ya geita lakini haina mchango sana kwa maendeleo yetu kwa sababu ya mfumo wa umiliki ambao serikali imekubaliana na wachimbaji. vivyohivyo, hata kama mitambo ya uzalishaji nishati hiyo itakuwa mtwara, bado inaweza isiwasaidie wana mtwara kama mikataba haitakuwa saidizi kwa watanzania.

kwa mawazo yangu, tunatakiwa siku zote tusimame kama watanzania na kusimamia rasilimali zetu popote pale iwapo iwanufaishe watanzania badala ya kuibuka usisi mara inapotokea rasilimali imegundulika sehem ya nchi.
 
Back
Top Bottom