Wamakonde noma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamakonde noma!

Discussion in 'Jamii Photos' started by Askari Kanzu, Dec 28, 2012.

 1. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Duhu, mabango!

  Mshua hii gesi ni ya wamakonde tafuta ya wakwere
  Mh. Kikwete tatizo sio ges mikataba yako noma
  Gesi kwanza uhai baadae
  Ukiiuaa tunakupeleka the Heg, gesi haitoki
  Bandari Bagamoyo, Gesi Bagamoyo, Bandari Bagamoyo, Mtwara wapuuzi?
  Gesi ibaki au tugawane inchi.

  [​IMG]
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na nyie nanyi hamtambuliki! Walipodai Wazanzibari mlio uch i mvi!
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Huu sasa upuuzi. Kila yakinguduliwa mafuta au gesi watu wanataka nchi yao. Ajabu watu hao hao wamefaidi raslimali nyingine kama madini na mbuga za wanyama vilivyoko mikoa mingine bila malalamiko. Ingawa tunajua mnasumbuliwa na umaskini na ujinga, tusiendekeze njaa na ujuha wa changu changu chako chetu au chako kitamu changu kichungu. Mtwara hawajanyimwa fursa ya kufaidika na gesi bali ukweli kuwa hakuna miundombinu ya kufanikisha uuzaji wa gesi husika. Ni ajabu kuwa kila mjinga anadhani yakigunduliwa mafuta au gesi basi sehemu yake itageuka Dubai overnight bila hata mipango!
   
 4. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jamaa wameshaanza kutengeneza pinde na mishale, tayari kuwafyatua wazungu mpaka waseme "oh my god"!
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,904
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Duh!Huo ujumbe Baba nani hii hawezi kuamini kama ntu wameamua
   
 6. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,009
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Pamoja sana mkuu.
   
 7. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jk maliza mda wako uwaachie wanacho kitaka
   
 8. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  sasa nyinyi wa mjini mulituona sisi wamikoani sio, maendeleo mjini, sisi vijijini jembe mjini ofisini leo mtatujua sisi bah sawa kuliko sudan, mulituona washamba sana oh wamachinga sijui wamakonde oh wamahiwa oh machale tunakwenda Msumbiji hatutaki tena Darsalam itakuwa kabirigado mpya ya msumbiji, wale renamo nyinyi hata mlikuwa hamuwajui mtawaona sasa
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,509
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huu ni ujinga wa kutupa. kwani mtwara ni ardhi ya wamakonde peke yao? ujinga gani huu, polisi wakiwapiga hata hawa tutawalaumu? kwani hapa dsm gesi si inakuja kwaajili ya kuiongezea thamani ili tupate hela za nchi, hela itakayotumika kwa manufaa ya watz wote including wamakonde? ardhi ni mali ya umma, vilivyoko chini yake si vya wananchi ni vya umma wote, na serikali ndio yenye mamlaka navyo. polisi kamata hao watu wanatuharibia siku. wajinga sana hao.
   
 10. Azizi Mussa

  Azizi Mussa Verified User

  #10
  Dec 28, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,512
  Likes Received: 1,992
  Trophy Points: 280
  ka kuwa mererani kuna TANZANITE NADHANI NAO WANATAKIWA WAJITENGE ILI WATUMIE TANZANITE YAO. SISI WA MOSHI TUTAJITENGA ILI TUFAIDI PESA YA UTALII WA MLIMA KILIMANJARO.MARA NAO WATATAKIWA WAHAKIKISHE KWAMBA HELA YA SERENGETI WANAKUSANYA WENYEWE;ZAIDI YA HAPO WAPEWE NCHI YAO.MWANZA WANATAKIWA WASIKUBALI MTU AKACHUKUA DAGAA WAO.WENYE DHAHABU WAACHWE WAPUMUE.SI WAPEWE NCHI YAO! UPUUZI MKUBWA! TATIZO WAKATI WENGINE WANAFIKIRI KWA KUTUMIA AKILI WENGINE WANAFIKIRI KWA KUTUMIA 07........
   
 11. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,145
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hahaha!hii isije kuwa kama "KIBANGA AMPIGA MKOLONI" ila jamaa kwa mishale tu hawajambo, na pia wanautaalam wakujigeuza Simba si unakumbuka wale simba wala watu toka ukanda huo!
   
 12. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe nadhani huijui Mtwara kabisa unakurupuka tu, hata kusoma historia yake bado pia! Mtwara wanafaidika na rasilimali zingine kama madini etc kivipi?? Mkoa masikin wa kutupa unasema wanafaidika? Kajipange na sio lazima uchangie hata kama huna point. Siungi mkono mgawanyo wa rasilimali kiukanda ila napinga upotoshaji wako about Mtwara.
   
 13. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,267
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  napinga hoja yako....gharama za hizo pipes na hao contractors wa kichina zinatosha kujenga miundombinu hiyo.....wametumia pesa nyingi for nothing,,,jaribu kufika pale songosongo uangalie watu wa pale walivyo maskini na gesi yao ndo inatengenezea umeme unaolipiwa mabilioni na Tanesco kwa siku,,,,,kaa chini fikiria kiundani,why dar-es-salaam and why bagamoyo na kuko over-populated tayari,,,mpaka wabomoe nyumba za maskini wawahamishe tena ili kupitisha gesi na mafao yao muwanyime pia......inakera,,,,wana-Mtwara kaka yenu nawa-support...do what is right for your generation,hii ni very big project ****** anahamishia kwao.
   
 14. taamu

  taamu JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2012
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 3,815
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Sitaki kusema sana mtwara hamna bandari?pili je kuacha hao tunaowaita wapuuzi gesi itanufaisha nchi au ni kama tanzanite na kenya pia south africa.
   
 15. englibertm

  englibertm JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2012
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 9,123
  Likes Received: 1,821
  Trophy Points: 280
  Kale kadhambi Kaubaguzi aliko tabiri Mwalimu naona kanaanza kuota mizizi" sisi wamakonde wao wakwere."
   
 16. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,099
  Likes Received: 4,119
  Trophy Points: 280
  Gesi ibaki au tugawane nchi........hapa namkumbuka aliyekuwa mbunge wa Tandahimba Mh Said Salim Nandonde......
   
 17. VOICE OF MTWARA

  VOICE OF MTWARA JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 2,464
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu shida si gas kutotoka mtwara, swali la kujiuliza ni je mtwara na ukanda wote wa kusini utanufaikaje na hiyo gas? mikoa ya lindi na mtwara ni maskini sana, amini usiamini kuna wilaya nyingi kama vile nanyumbu, liwale, ruangwa, nachingwea bado hazina umeme wa kueleweka licha ya gas kua jirani. kumbuka ni zaidi ya miaka mitano sasa gas inahamishwa toka songosongo kilwa kwenda dar, ilihali watu wa maeneo jirani kama liwale hawana umeme. kwanini huo uwekezaji mkubwa usifanyike hukuhuku kusini? kwanini gas ipelekwe bagamoyo?kwa nini viwanda visijengwe mtwara ila bagamoyo? kwa nini bandari ya mtwara yenye kina kirefu tanzania isiboreshwe?kwa nini ikajengwe mpya bagamoyo?
   
 18. K

  Kulya JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Charity begins at home Gentleman... Shuzi ulilojamba halianzi kunuka mita mia mbele, huanzia kwako!
   
 19. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hivi unafikiri Mtwara hawataki hio hela? wanataka lakini Arusha kuna utalii mji wao mzuri Dar makao makuu ya nchi ndio kuko mbele zaidi sisi Mtwara mmmhh na sisi tunataka maendeleo zaidi ya Bandari kuna nini zaidi na hiyo bandari ilijengwa ili kupitisha silaha kwenda kusini wakati wa ukombozi kule kusini
  Hivi nyinyi munaopiga kelel mumefika kule Kusini? angalia barabara ya kibiti ukivuka daraja tu ndio utajuwa kwanini wale wanaopewa uhamisho kwenda kusini wanaacha kazi
   
 20. MMAHE

  MMAHE JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 831
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Father of All except me! unategemea miujiza ilete hiyo miundo mbinu? miaka 51 bila barabara,huduma za afya,elimu duni, kutapeliwa korosho,hizo rasimali zenu tumezifaidi wap?
   
Loading...