Wamachinga waomba kukutana na Rais Samia

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma) limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane nao kumweleze kero walizonazo ili ajue namna ya kuzifanyia kazi.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 na Makamu Mwenyekiti wa wamachinga Taifa, Steven Lusinde wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vurugu za wamachinga zilizotokea jana katika soko la Kariakoo.

Soma hapa:Machinga waanza kuhamishwa Lusinde alisema Samia ndiye Rais wa kwanza kutenga fungu la fedha kwa ajili ya maendeleo ya wamachinga na kwamba mkutano huo utamwezesha kupokea maoni kutoka kwao moja kwa moja nini Sh5 bilioni zifanye kwa manufaa ya wajariamali hao wadogo.

“Tunamshukuru sana Rais ametoa zaidi ya Sh5 bilioni kuhakikisha yanaorodheshwa maeneo hayo kwa ajili ya wamachinga, sisi tupo pamoja na yeye akutane na sisi wamachinga wa mikoa yote tumueleze hata asiyoyajua.

“Yeye mwenyewe apange wapi ili tumweleze changamoto zetu na tushauri fedha hizo zinaweza kutatua changamoto zipi mengi yasiweze kutokea, tunashkuru suala hili amekasimisha kwa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi hivyo utekelezaji umewezekana,” amesema Lusinde.

Amesisitiza kuwa viongozi wanatakiwa wawashirikishe machinga maeneo wanayotaka kwenda kuwaweka ili kuondoa sintofahamu.

“Watushirikishe sisi changamoto zipo, ukiangalia maeneo mengi waliyoenda bila usumbufu walitushirikisha tunaamini kila kitu kitaenda sawasawa,” amesema Lusinde.

Makamu mwenyekiti Shiuma mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto amesema viongozi wa kundi hilo wana wajibu wa kuishauri Serikali katika kufanya maboresho changamoto zilizopo katika hayo maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wamachinga wanakuwa na mazingira bora ya biashara.

Soma hapa: Machinga Mwanza waanza kuhama, watishia kurejea barabarani

Mmachinga eneo la Shekilango, Mohamed Shaban amesema ameamua kubomoa banda lake kwa kufuata sheria bila shuruti hata hivyo amesema eneo analopelekwa halina biashara za uhakika ikilinganishwa na alipokuwepo.

Chanzo: Mwananchi
 
F3ABF0DA-36B2-408F-8D4A-CDEE0345795C.jpeg
 
so wameamua kupiga magoti siyo kwa mwenyekiti wa CCM taifa.. bac sawa.
 
Hivi kwa tafsiri ya sasa, Machinga ni Nani ? Ni nini vigezo / Sifa za mtu kuitwa Machinga
 
Ni Wamachinga wameomba Kukutana na Rais Samia au ni 'Mkakati' umesukwa vyema na 'System' ili Wamachinga jana wafanye Fujo kisha Mama ( Rais ) ajitokeze Kuwasikiliza na awape Suluhu ya Kudumu ya Maamuzi ya Kuwapendelea Wamachinga na Kuwapoza kisha apate Sifa ya kuonekana kuwa anawapenda na kuwajali Wamachinga?

Acheni Kutufanya Watu wote ni Majuha.
 
Back
Top Bottom