Wamachinga haitokani na Marching Guy!!

Wamachinga haitokani na Marching Guy!!

Nimeelezea kuwa ni kutokana na waliokuwa wanafanya biashara ya kutembeza bidhaa hasa kwenye jiji la Dar es salaam miaka ya mwanzoni mwa themanini kuwa ni watu kutoka mtwara. Kwa ivo watu wakawa wanaulizana "hiyo bakuli umenunua wapi" na mnunuzi hujibu " nimenunua kwa wamachinga" muuliza swali huelewa kwamba imenunuliwa toka kwa watu watembezao bidhaa mitaani.
Mchinga ni jimbo huko Kusini. Liliwahi kuwa chini ya uongozi wa Mudhihir Mudhihir kabla ya 2010! Na 2010-2015 jimbo lilishikwa na Mh. Said M. Mtanda (DC Nkasi)! Mudhihir aliwahi kunukuliwa na Radio One akisema vijana wale (wamachinga) wengi Wao walitokea MCHINGA! Na akiwa hapo Radio One MM pia akazungumzia hiyo MARCHING GUYS kuwa ndio imeleta MACHINGA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza sina sababu ya kutafuta sababu kwani huo ndiyo ukweli na uhalisia. Sasa "Correlation" ya "Marching Guys" na "Wamachinga" iko wapi? Au kwa kuwa kimatamshi ni kama yanafanana?

Kwenye kiswahili kuna kundi la maneno "Mwa" ambalo neno "mmachinga" linakuwa "Wamachinga" sasa "marching Guys" iweje iwe "Wamachinga"?

Nimetoa Historia ambayo ni ya kweli wewe unaleta mapokeo ya zama hizi. Unaikumbuka bendi ya "Nchinga Sound" iliyokuwa inaongoza na Muumini Mwinyijuma? Sasa huko Nchinga ndiko wamachinga wanapotoka na wao ndiyo asili ya watembeza vitu mtaani kuitwa wamachinga.

Nimesema kwamba wazungu wamachinga wanawaita "Hawkers" basi ni kwa nini hawa wa huku kwetu waje wawaite "Marching Guys" wakati wanafanya biashara kwa mtindo unaofanana na ule wa "Hawkers" wa kule kwao?
Naikumbuka bendi ya Mchinga Sound,iliyoanzishwa na Mudhihir,Mbunge kutoka Mchinga,mkoani Lindi,tena Lindi ya upande wa kuelekea Kilwa ambayo inakua inaanza kupakana na Mkia wa Pwani(Wilaya ya Rufiji)!
Nadharia nyingine ya Wamachinga ni jina la Mchinga,eneo ambalo lipo mkoa wa Lindi na siyo Mtwara. Kwa hiyo ni uongo mkubwa kusema Wamachinga chimbuko lake ni Mtwara,bali Marching Guys au Watu wa Mchinga,na kwa kuwa Mchinga pia hupatikana kusini,ikabeba jina kwa watu wa kusini,lakink kamwe,siyo Mtwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe uko sahihi kabisa kwanza neno machinga halijaanza zamani sana nazani ni miaka ya 90 na hivi wakati huo walioanza kufanya kazi ya umachinga walitokea huko nachingwea na mtu mwingine yeyote akifanya kazi hiyo ilizaniwa ametokea huko na asili Yao hao watu wa nachingwea ni wachinga na ndio kitu ambacho kimezaa jina la machinga leo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndo ukweli mengine ubishi tu. Wamachinga ni jamii ya watu wa Mtwara waloboresha biashara za mikononi. Kuwaita 'Matching Guys' ni utani uloibuniwa na waloivamia fani ya Wamachinga
 
Ila kimatamshi ukisikia hiyo "machinga" inayohusiana na mtembeza bidhaa inavyotamkwa utafikiri imetokana na hayo maneno ya kiingereza "marching guy" tofauti na ambavyo ingetamkwa "machinga" iliyotokana na neno hasa la kiswahili. Hebu jifanye ni mzungu na kutamka neno "machinga" kisha utamke neno hilo hilo kama mswahili wa kawaida na kisha ulinganishe na linavyotamkwa siku zote kumaanisha hawa watembeza bidhaa tunaowafahamu.
 
CHAZA kwa suala la Mtwara na Lindi ni jambo la majadiliano. Ni kweli kuwa wamachinga wengi wanatoka Lindi lakini si kweli kwamba Mtwara hakuna Wamachinga!!
 
Kipindi cha zamani mi niliamini kusini ni Mtwara tu. Inawezekana wengi waliamini hivi pia hivyo Lindi ikachukuliwa kama sehemu ya Mtwara na kwa ujumla wake tukadhani machinga wanatokea mkoa wa Mtwara.
Wanaitwa Machinga ingawa si wote kutoka Mtwara- Prof. Jay Bongo Dsm
Uongo mtupu. Mimi mwenyewe natoka huko. Ukweli ni kwamba kuna wamakonde wa pwani(wamaraba,wengi wako eneo la Mtwara vijijini mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi,na lafudhi yao ni "Broken Swahili)! Halafu kuna wamakonde wa Bara(kule Newala na Tandahimba-Makonde Plateu),hao matamshi yao huwa makali kuliko wale wa pwani. Lakini pia kuna wamakonde wa Msumbiji ambao wana machale na ndonya kama ulivyosema. Katika makundi yote hayo matatu,kuna baadhi ya maneno huwa ni tofauti. Lakini tofauti kubwa iko kati ya wale wa Msumbiji na aina yoyote ya Wamakonde wa Tanzania. Kote huko hakuna neno,jina,au mtaaa,mji,kijiji kinachoteflect Wamakonde na Wamachinga,hakuna. Na ndiyo maana hata wewe mtoa hoja hujaonyesha ni wapi Wamachinga wanahusishwa na mkoa wa Mtwara.
Dhana pekee ambayo naweza kukubaliana nayo ambayo ni tofauti na Matching,Marching Guys(vyovyote utakavyoit) ni jina la eneo la mkoa wa Lindi kwenye jimbo la Mchinga,labda kwa nadharia hiyo. Lakini chimbuko la Wamachinga kureflect mkoa wa Mtwara na Wamakonde,hakuna affiliation kwa chochote,siyo jina,eneo,lugha au hata watu nasema hakuna.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom