Waluyha na msosi

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Huwa mara kadha natazama Churchill show.

Nikiwa Kijana mdogo nimeishi na Waluyha kama jirani zetu, nafahamu upenzi wao kwa chai. Nakumbuka wakati flani kuna Mluyha aliniambia akinywa chai analima sana kuliko kawaida.

Siku hizi mara kadhaa ukitizama Churchill show unaona Waluyha wanataniwa sana juu ya kupenda msosi.

Ni kweli kwamba Waluyha ni 'walevi' sana wa msosi?
 
LuhyaTings-1.png
Ni kama tu watz mnavopenda kuwatania wasukuma na wanyakyusa. Watu wa aina zote Kenya huwa wanataniwa, lakini sio zaidi ya waluyha. Utani huo huwa haufanywi kwa chuki ila ni kwasababu waluhya wenyewe huwa wanajivunia sana mila zao, miziki, vyakula na pombe zao za kitamaduni pia. Alafu wapo 'visible' sana kila sehemu Kenya na kawaida yao ni kwamba ni wapenda amani. Bure ingekuwa ni wengine wetu tunataniwa kiasi hicho, pangechimbika sio mchezo.
 
Kuwa makini usiwaseme vibaya maana ni mashemeji zangu, ila kuna kaukweli maana wao likija suala la ugali wa dona yaani kama wanavyoita kwa kilugha 'vusuma', huwa hamna cha utani, nafikiri wana kaundugu na Wasukuma maana niliwaona Wasukuma wakitembeza ugali kama mchezo.
Kwa hawa Waluhya, yaani mwanamke akiolewa kule halafu aandae wali au pilau au githeri/makande ambavyo anategemewa viliwe na watu wanaotokea shambani kulima, ataishia kurudi jikoni akaandae mzee mzima...yaani 'ukali'..hehehe ugali.

Luhya.jpg
 
LuhyaTings-1.png
Ni kama tu watz mnavopenda kuwatania wasukuma na wanyakyusa. Watu wa aina zote Kenya huwa wanataniwa, lakini waluyha ni sana. Sidhani inafanywa kwa chuki ila ni kwasababu waluhya wenyewe huwa wanajivunia sana mila zao, miziki, vyakula na pombe zao za kitamaduni pia. Alafu wapo 'visible' sana kila sehemu Kenya na ni wapenda amani. Bure ingekuwa ni wengine wetu tunataniwa kiasi hicho pangechimbika sio mchezo.
Hata Mimi najua si chuki.
Nilikuwa najua Waluyha kwa chai ndiyo kiboko kumbe mpaka msosi. Namkumbuka Captain Ottoyo kuna wakati alisema wakati anaingia Nyeri alijua ni Nyeri kwa sababu kila hatua kuna bank au Mpesa ila kwa Waluyha kila hatua kuna restaurant halafu choo
 
LuhyaTings-1.png
Ni kama tu watz mnavopenda kuwatania wasukuma na wanyakyusa. Watu wa aina zote Kenya huwa wanataniwa, lakini sio zaidi ya waluyha. Utani huo huwa haufanywi kwa chuki ila ni kwasababu waluhya wenyewe huwa wanajivunia sana mila zao, miziki, vyakula na pombe zao za kitamaduni pia. Alafu wapo 'visible' sana kila sehemu Kenya na kawaida yao ni kwamba ni wapenda amani. Bure ingekuwa ni wengine wetu tunataniwa kiasi hicho, pangechimbika sio mchezo.

hicho kiswahili chako safi kabisa kaka
 
Waluya ndo akina Musalya Mudavadi?
 
MK254, shemeji zako watasema huna heshima hata kidogo. Omwami, ukiandika jina Ugali hakikisha inaanza na, 'U', herufi kubwa tafadhali. Tusizoeane. Huu mlo umetolewa hadi hit song!

Hehehe!! Hapo kweli bila herufi 'U' kukuzwa ni ukosefu wa hesima, halaafu kunao Wasukuma Tz hutaniwa sana kwenye hili la Ugali, check picha zao...Hadi nahisi njaa sasa, ila hata mimi likija suala huu msosi wa 'Ukali' sipendi utani maana kawaida lazima niuchezee...

f01527a7e306ee6cee0bd8ea0d4318a1.jpg

IMG-20141211-WA0007.jpg
 
Waluya ndo akina Musalya Mudavadi?
Ndio, na aliyekuwa makamu wa rais, mwendazake Kijana Wamalwa, aliyekuwa waziri na baadaye makamu wa rais Moody Awori. Waziri Eugene Wamalwa, wanasiasa machachari Ababu Namwamba na Dr. Boni Khalwale na kinyangarika mwingine, aliyekuwa kinara wa muungano wa vyama vya upinzani, NASA, Moses Wetangula.
 
Hehehe!! Hapo kweli bila herufi 'U' kukuzwa ni ukosefu wa hesima, halaafu kunao Wasukuma Tz hutaniwa sana kwenye hili la Ugali, check picha zao...Hadi nahisi njaa sasa, ila hata mimi likija suala huu msosi wa 'Ukali' sipendi utani maana kawaida lazima niuchezee...

f01527a7e306ee6cee0bd8ea0d4318a1.jpg

IMG-20141211-WA0007.jpg
Hahaha! :D Mungu wangu, hapa sasa ni siku ya kawaida kwao??? Hii shughuli wakishaimaliza itakuwa ni hatar, hapa lazima watacheua hadi dhambi zote. :D
 
Ndio, na aliyekuwa makamu wa rais, mwendazake Kijana Wamalwa, aliyekuwa waziri na baadaye makamu wa rais Moody Awori. Waziri Eugene Wamalwa, wanasiasa machachari Ababu Namwamba na Dr. Boni Khalwale na kinyangarika mwingine, aliyekuwa kinara wa muungano wa vyama vya upinzani, NASA, Moses Wetangula.
Kijana Wamalwa Mzee wa totoz na kupenda cartoon
 
Back
Top Bottom