Walutheri waruhusu ndoa za mashoga
na Mwandishi Wetu, STOCKHOLM, Sweden
KANISA la Kiinjili la Kilutheri lenye waumini wengi zaidi nchini hapa, limekubali kubariki ndoa za watu wa jinsia moja.
Sweden, imekuwa ni nchi ya kwanza duniani kuruhusu mashoga kuoana ndani ya kanisa hilo kubwa duniani.
Hatua ya kanisa hilo imekuja ikiwa ni miezi mitano tu baada ya serikali ya hapa kulifanya suala la watu wa jinsia moja kuoana kuwa la kisheria. Karibu asilimia 70 ya wakuu 250 wa kanisa hilo, walipiga kura kuunga mkono kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana ndani ya Kanisa la Kilutheri.
Lahaula!! This is too much now!!Walutheri waruhusu ndoa za mashoga
na Mwandishi Wetu, STOCKHOLM, Sweden
KANISA la Kiinjili la Kilutheri lenye waumini wengi zaidi nchini hapa, limekubali kubariki ndoa za watu wa jinsia moja.
Sweden, imekuwa ni nchi ya kwanza duniani kuruhusu mashoga kuoana ndani ya kanisa hilo kubwa duniani.
Hatua ya kanisa hilo imekuja ikiwa ni miezi mitano tu baada ya serikali ya hapa kulifanya suala la watu wa jinsia moja kuoana kuwa la kisheria. Karibu asilimia 70 ya wakuu 250 wa kanisa hilo, walipiga kura kuunga mkono kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana ndani ya Kanisa la Kilutheri.
Naimani Baba Mwalasusa atalitolea tamko hili!!Karibu asilimia 70 ya wakuu 250 wa kanisa hilo, walipiga kura kuunga mkono kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana ndani ya Kanisa la Kilutheri.
Mimi ndio maana wakati mwingine huwa naamua kunywa bia zangu na kulala tu! Kwenda kanisani inakuwa kama vile kwenda kupoteza muda tu! Inakatisha tamaa sana!
Mh!!Masaki anaona hata kwenda kanisani haina maana, ebu angalia hata wao idadi inazidi kupungua, soma sehemu ya taharifa hiyo hapa chini.
Nchini hapa, kati ya watu wanne, watatu kati yao ni waamini wa dhehebu la Kilutheri. Kwa maana hiyo, robo tatu ya raia wa nchini hapa ni waumini wa dhehebu hilo, japo idadi ya wanaohudhuria ibada imepungua sana.
Kanisa la Kilutheri nchini hapa, ambalo lilikuwa likiongoza nchi hadi mwaka 2000, linaungana na Bunge ambalo lilipitisha sheria ya kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, ambako utekelezaji wa sheria hiyo ulianza rasmi Mei 1, mwaka huu.
Mimi ndio maana wakati mwingine huwa naamua kunywa bia zangu na kulala tu! Kwenda kanisani inakuwa kama vile kwenda kupoteza muda tu! Inakatisha tamaa sana!
Mkuu una hakika na ishu hii?
Mbona ni balaa hili tena?
KUMEGUNDULIWA NINI KATIKA USHOGA?
Kwa nini wanakuwa na nguvu ya namna hii hawa Bazazi?
Sasa wewe upo dini gani!??mi siku zote siziamini hizi dini za kizungu kwa sababu eti nazo zinakwenda na wakati kwa kukiuka misingi ya imani yao, makanisa yote ni mihimili ya shetani toka enzi yaliposhabikia UTUMWA mbaka sasa wanashabikia USHOGA
Its the future.. inevitable.. I dont like chichi mans but they have rights too..lol
Bora zirudi zile dini za asiri, maana zamani za dini hizo ilikuwa ni marufuku kutenda maovu, ukifanya kinyume unaadhibiwa pale pale, sio siku hizi eti Mungu wa rehema matokeo yake watu wanafanya hata wanyama hawayafanyi.mi siku zote siziamini hizi dini za kizungu kwa sababu eti nazo zinakwenda na wakati kwa kukiuka misingi ya imani yao, makanisa yote ni mihimili ya shetani toka enzi yaliposhabikia UTUMWA mbaka sasa wanashabikia USHOGA