Walutheli wawafuata waanglikana!

Hii mbona tangu mwaka jana? tatizo la wasedish kwao kila mtu ni equal, mtoto na baba wote wako sawa, mama na baba wote wako sawa,mwanamume na mwanamke wote wako sawa na wanahaki sawa, mwalimu na mwanafunzi wote wako sawa,hili lilichelewa saana nachok´jiuliza Ni Mungu Yupi hawa watu wanamwabudu na kumhubiri?

Nimekuwa pale GOTHENBURG (GOTEBORGS) CITY nilimshangaa rafiki yangu mswedish aliponiambia kwamba kanisa ndilo lililowacheleweshea maendeleo. Makanisa wakiyaita DORMSHIRIKAN yametelekezwa, mengi yanageuzwa GODOWNS> Suala la kuamini kuwa kila mtu ana haki ya kufanya anachotaka ndipo walipopotoka. Ushoga unafanyika hadharani, mashoga wameandika vitabu kuhusu philosophy ya ki-shoga. Mashoga kwenye University huwa wanaalikwa kutoa mhadhara hasa masuala yanayohusu SEXUALITY. Hawa watu wamelewa maendeleo yao na yatawafanya vibaya
 
mi siku zote siziamini hizi dini za kizungu kwa sababu eti nazo zinakwenda na wakati kwa kukiuka misingi ya imani yao, makanisa yote ni mihimili ya shetani toka enzi yaliposhabikia UTUMWA mbaka sasa wanashabikia USHOGA

NADHANI UNASHINDWA KUPAMBANUA DINI NA MAAMUZI YA WATU, TUKIZUNGUMZIA UKRISTO, TUNAZUNGUMZIA BIBLIA NA HIYO NDIO KATIBA YA UKRISTO, SWALI LA KUJIULIZA MBONA MWANZO HAWAKUUHARARISHA HUO USHOGA? JIBU NI KUWA KATIBA (BIBLIA) HAIRUHUSU, NA BIBLIA BADO NI ILEILE TU, KWA MAANA NYINGINE HAO WALIOMUA HIVYO WAMEVUNJA KATIBA (BIBLE), NA KWA MAANA NYEPESI NI KUWA HAO SASA SIO WAKRISTO TENA KWA SABABU HAWAFUATI MISINGI YA DINI YAO, na adhabu ya hayo matendo hipo wazi
 
kuweni waislamu period, ujinga huo hauruhusiwi na akipatikana ni ananyongwa..period!
 
kweli, ha!!!! yanatisha haya mambo! watu wanafanya kanisa kuwa ni society ya kiuchumi zaidi badala ya kuangalia Roho za watu!!!!!
 
Naimani Baba Mwalasusa atalitolea tamko hili!!

Kimey,

Niliwahi kusikia mahubiri ya Baba Askofu malasusa mwanzoni mwa mwaka huu. Naye alisema kuwa kamwe KKKT halitakubali ndoa za jinsia moja kutokea. Kama hao wazungu wameanzisha basi KKKT halitwasupport. Akasema hata kama watakata misaada, Mungu atafungua njia nyingine kwa KKKT. Akasema dini siyo NGO, kwani NGO nyingi bila misaada haziwezi kufanya kazi, ila kwa kanisa Mungu anajua jinsi ya kulisaidia.

Masaiti
 
Hii mbona tangu mwaka jana? tatizo la wasedish kwao kila mtu ni equal, mtoto na baba wote wako sawa, mama na baba wote wako sawa,mwanamume na mwanamke wote wako sawa na wanahaki sawa, mwalimu na mwanafunzi wote wako sawa,hili lilichelewa saana nachok´jiuliza Ni Mungu Yupi hawa watu wanamwabudu na kumhubiri?
Nadhani atakuwa Mungu wa Sweden
 
Kwa wale wanaoamini katika "evolution", je hii ndio namna mwanadamu atakavyokuwa "extinct"? Maana naona sasa mashoga wanaanza kukaribia idadi ya wasiomashoga, baadae watakua majority na hivyo kupelekea kupotea kwa kizazi cha mwanadamu!
 
Walutheri waruhusu ndoa za mashoga


na Mwandishi Wetu, STOCKHOLM, Sweden



KANISA la Kiinjili la Kilutheri lenye waumini wengi zaidi nchini hapa, limekubali kubariki ndoa za watu wa jinsia moja.
Sweden, imekuwa ni nchi ya kwanza duniani kuruhusu mashoga kuoana ndani ya kanisa hilo kubwa duniani.
Hatua ya kanisa hilo imekuja ikiwa ni miezi mitano tu baada ya serikali ya hapa kulifanya suala la watu wa jinsia moja kuoana kuwa la kisheria. Karibu asilimia 70 ya wakuu 250 wa kanisa hilo, walipiga kura kuunga mkono kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana ndani ya Kanisa la Kilutheri.
Muongo mkubwa we. Hayo yametokea Sweden unaingizaje KKKT? Ni lini KKKT limeruhusu ndoa hata uzinzi ni marufuku unatengwa na kanisa kama ikidhihirika. Futa hiyo red tafadhali usiwe kama waandishi wa udaku.
 
Heri yao wameweza kuface the reality.Hata tusipohalalisha idadi ya mashoga inazidi kuongezeka siku hadi siku..hili haliepukiki.Ni heri kuwahalalisha kuliko kuwakataza lakini bado mambo yanaendela nyuma ya pazia.
 
Niko off point kidogo. Eti, ulisoma primary? Ulijifunza kuandika imla? Kwenye kuongea nitakusamehe. Yawezekana umeathiriwa na lugha mama. Lakini hata kuandika?? Omba mods warekebishe title
 
Muongo mkubwa we. Hayo yametokea Sweden unaingizaje KKKT? Ni lini KKKT limeruhusu ndoa hata uzinzi ni marufuku unatengwa na kanisa kama ikidhihirika. Futa hiyo red tafadhali usiwe kama waandishi wa udaku.

Duh! Besti mbona umekurupuka? Ndio umeamka? Hamna sehemu yoyote hapo alipoandika KKKT. Kanisa la Kiinjili la Kiluteri halipo Tanzania tu, Marekani lipo, na Sweden lipo!

Futa wewe tafadhali na umuombe mwenzio msamaha
 
Back
Top Bottom