Wallet wallet wallet!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sinai

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
288
47
Leo hii asubuhi nikiwa ktk daladala, niliwasikia akina dada wanaongelea mambo yao ya jana usiku, mmoja akiwa anamweleza mwenzake kuwa, baada ya kuona jamaa anamwangalia kwa ishara ya kumtamani, na huku akiwa anatoa wallet iliyotuna kulipia vinywaji, mdada akaamua kumwomba kaka yule wakae meza moja! Kisha alipo pewa ruksa, akaanza kumlegezea hadi jamaa akatia timu, cha ajabu walipoenda kunako mambo, yule dada hakulipwa chochote na wala jamaa hakuwa na pesa kama yule dada alivyozania! Yule dada akasema wanaume wengine bwana, washenzi sana wana mawallet makubwa kumbe hayana kitu ndan! Hivi akina dada, kwanini macho yenu yanaelekezwa zaidi kwenye wallet za wanaume kuliko upendo wa kweli???????????
 
Usituchanganyie habari hapa bana wewe yaani hao wadada wawili tu ushasema wadada wanaangalia wallet?? Inaonekana na wewe ni mmoja wapo mie naangali maloveee tu hata kama hana kitu nampatia mimi ha ha ha ha
 
hiyo daladala ni ya route gani na saa ngapi ulipanda?

Hili swali ni zuri sana hata mimi natamani kupata majibu yake!!! Asije kutuambia Mwenge Posta kupitia Ali Hassani Mwinyi road tu!!!!
 
Leo hii asubuhi nikiwa ktk daladala, niliwasikia akina dada wanaongelea mambo yao ya jana usiku, mmoja akiwa anamweleza mwenzake kuwa, baada ya kuona jamaa anamwangalia kwa ishara ya kumtamani, na huku akiwa anatoa wallet iliyotuna kulipia vinywaji, mdada akaamua kumwomba kaka yule wakae meza moja! Kisha alipo pewa ruksa, akaanza kumlegezea hadi jamaa akatia timu, cha ajabu walipoenda kunako mambo, yule dada hakulipwa chochote na wala jamaa hakuwa na pesa kama yule dada alivyozania! Yule dada akasema wanaume wengine bwana, washenzi sana wana mawallet makubwa kumbe hayana kitu ndan! Hivi akina dada, kwanini macho yenu yanaelekezwa zaidi kwenye wallet za wanaume kuliko upendo wa kweli???????????

Aaaah, kumbe!
 
Upendo wa kweki hautafutwi kwenye
Mabaa ..
na mbaya kabisa kuringishia wallet iliyojaa makaratasi
huyo alikuwa anataka One Night Stand ...

Yaani maelezo yako na swali lako hayafani kabisa. ..

Ni kama vile unajaribu kumpa tembo mabawa..
 
Hili swali ni zuri sana hata mimi natamani kupata majibu yake!!! Asije kutuambia Mwenge Posta kupitia Ali Hassani Mwinyi road tu!!!!
Hawa wa route hii ndio wanaangalia wallet??
 
Wanaangalia ukubwa wa wallet ili wajue kama na vijicent vyao vitaenea humo!
 
Huyo demu nae maharage ya mbeya,yaani kuona walet tu macho pima!!.Nimefurahi kuona jamaa alikopa hadi majambozi,duuh.Haya sasa mwanamke hakuumbuka hapo!!
 
Umeshasema dada alikuwa anategemea kulipwa kwa huduma aliotoa kwahiyo ni 'mjasiriamali',sasa mapenzi yanahusika vipi ? na inawahusu vipi kinadada kwa ujumla wao ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom