Wallah!! Siitaki tena CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wallah!! Siitaki tena CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Jul 13, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wana jamvi, kabla ya yote niseme kwamba nilikuwa mwanachama wa CCM.
  Nimeamua kuvua magamba niliyokuwa nayo CCM na sasa naangalia upepo unavyokwenda nikiwa nje ya Chama Cha Magamba. Kifupi ni kuwa nimekichukia vibaya as if sijawahi kuwa mwanachama wake.

  Zamani tulizowea kuwazushia uongo wapinzani kwa kuwaita wakabila(Enzi za NCCR na CDM), wadini(CUF), wajimbo(UDP) na pia kusema kuwa wapinzani wanaendesha vyama vyao kama kampuni.

  Leo hii tuhuma zote mbaya zipo CCM. CCM ni waroho wa madaraka(tazama sasa wanavyotoana macho kwa ajili ya urais). CCM ni waroho wa fedha na wachumia tumbo(tazama issue ya posho za vikao zilivyowatoa roho).

  Mzee Malecela mwaka 1995 aliwahi kukaririwa akisema, CCM itatawala miaka 50 mbele, akiwa na maana hadi mwaka 2045. Nadhani mzee huyu alikosea hesabu na inawezekana alikusudia CCM itatawala mwisho 2010.

  Tazama, Samwel Sitta anawananga wabunge wa upinzani ambao walikuwa wanachukua sitting allowance ktk bunge lililopita. INANISHANGAZA. mzee huyu amezeeka vibaya sana. Kwani haiwezi kutokea mtu akawa muovu lakini baada ya muda akaamua kuacha uovu na kumrejea Mungu wake? UBAYA UKO WAPI!!! Mbona yeye aliwahi kumuita naibu spika wake kuwa ni mtu wa kukurupuka lakini baadae alimuomba radhi na akasamehewa.

  Sasa hivi ni aibu kwa kijana kuwa CCM, labda kwa wenye vyeo kama Nape, Januari, Bashe, Malisa na wengine kama wao. Leo hii si ajabu kukuta mtu anakwenda kwenye kikao cha UVCCM akiwa na nguo mbili. Moja(ya kawaida) anaivaa pindi akitoka nyumbani na wakati wa kurudi na ile inayoonesha kuwa ni mwanaCCM anaivaa katika kikao tu, akitoka anaivua na kuiweka ktk begi.

  NIMETAFAKARI KWA UMAKINI, NA KWA MUDA SASA. CCM haitufai. Nakaa pembeni
   
 2. k

  kiloni JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Be serious and have a choice of your heart.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kwa maamzi yako sahihi, naamini hujakosea...Karibu CHADEMA kwenye chama makini..
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  karibu sana chadema! siku nilipoachana na ccm na kuchukua kadi ya chadema nilijisikia kuzaliwa mpya..... yaani sasa ni mtu huru! yaani kama vile mtu aliyeokoka!
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ndugu, ngoja tudeal na hii ya Rostam kwanza....ile sredi ita-jam sasa hivi, members wote wapo kule!! Huku tutakuja badae!!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Hongera zako Mkuu kwa kuweza kusoma alama za nyakati mapema na pia kuzigundua propaganda za CCM ambazo hazina mshiko kuudanganya umma wa Watanzania kwamba CHADEMA ni Chama cha Wachagga na Wakristo ili wao waendelee kubaki madarakani na kuiifilisi nchi kwa ufisadi.
   
 7. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata wewe kama mpaka leo ulikuwa bado CCM lazima kuna kitu tu ulikuwa unafaidika nacho huko. Kwa kuwa naamini kabisa hakuna kijana aliyekwenda shule ambaye anayeweza kuisapoti CCM kwa kuwa lazima atakuwa anajua maovu waliyo na wanayoendelea kuwafanyia watanzania. Hawana huruma hata kidogo na Watanzania, ni Walafi halafu wengi Upeo wa kujenga hoja za maana hawana zaidi ya Wabunge wao kuzomea na kutumia wingi wao bungeni kupitisha kitu chochote hata kama ni kibaya kwa Wananchi so long as kimeletwa na Serikali.
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja, hii ai'update badae kidogo, ila kitendo chake cha kujitoa kwenye gamba CCM ni cha kishujaa zaidi kuliko hata kujivua gamba kwa yule mwizi RA.
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hongera karibu kwetu huku TLP Tuendeleze vita na magamba si unamwona mwenyekiti wetu anavyopambana
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mmmh ndugu yangu sina imani saana na mwenyekiti wenu mana juzi kati alianza kudai marupurupu ili atetee wananchi
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  hata kwenye kikao juzi jumamosi tulimuliza kulikoni marupurupu akasema anatetea haki yake dadangu
   
 12. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ndio unashtuka? Umechelewa sana ila msamaha upo.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu sema akili zinatofautiana tuu kila mtu ataihama ccm including MS isipojisafisha kwa dhati!
   
 14. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Karibu mwana mpotevu, ulikujaga kuwaje ukawa gamba?? Kule waacha makada wenyewe akina 6, wakilala wanaongea hili wakiamka wanaongea lile kama wamerogwa yani kama popo ndege si ndege mamalia si mamalia. Mweh!!!
   
 15. p

  plawala JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushauri uachane ya tabia ya ki-shibuda shibuda na ki-mrema mrema huko utakapoenda
   
 16. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Ila huwa anatoa udenda bungen
   
 17. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera ka gamba kadogo kujivua hako kagamba kako kadogo ila naamini wewe upo safi hivyo wewe sio gamba mkuu wangu cha msingi tukatae wala wabaya hata kama wapo cdm tutawatimua
   
 18. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tuliza kichwa tafuta chama makini ila usiwe kama shibuda.
   
 19. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  ukitema ccm hata uwezekano wa kwenda akhera kwako ni mkubwa mno.
   
 20. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  big up, nakupongeza,karibu sana CDM, Uhuru wa kweli, Mabadiliko ya kweli.
   
Loading...