safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 12,312
- 18,177
Hii pepo yenu ni miongoni mwa yanayonifanya nibaki kuwa muislamu nikaipate pepo ya kiislamu.Ah hivi kumbe ndo nyie pia mnaojipa moyo kuwa wanaume wa kiislam watakaofanikiwa kuingia mbinguni watakuta wameandaliwa wanawake mabikira 72 kila mmoja? Aisee hii dini ina mambo ya ajabu sana yaani watu wanadanganywa kila kitu na wanaamini
Mtu anashindwa kufikiria tu kwamba kule mbinguni kinachoenda ni roho na siyo mwili yaani mwili ukishaoza kule kaburini ndo basi na siku zote chenye tamaa na shauku ya kutaka kufanya dhambi ni mwili na siyo roho sisi wakristo huwa tunamnukuu Yesu aliposema "roho i radhi lakini mwili u dhaifu sana"
Halafu tendo la ndoa kwa Mungu ni uchafu haya mambo mliyowekewa duniani msitegemee mtaenda kuyakuta mbinguni yaani kitu ambacho Mungu alikiweka ni starehe kwa viumbe vyake hadi wanyama ndege na wadudu duniani ndo kikawepo na mbinguni? Subhanallah hivi nyie mbinguni mnapachukuliaje wandugu?
Kule ni patakatifu siyo sehemu ya kwenda kufanya zinaa wala kufunga ndoa tena kule ni sehemu ya kumsifu na kumuabudu Mungu tu hata hao kina Solomon na David hayo ya kuoa wake wengi waliyaacha hapa hapa duniani huko walipo wanasujudu tu saa hizi na ndo maana hata Yesu alizaliwa kupitia njia ya kawaida ya mwanamke lakini hakuzaliwa kupitia tendo la ndoa sema daah watoto wa bi mdogo mna kazi
Yani duniani niabudu alafu malipo iwe ni kuabudu huko huko,sio poa kabisa.
Ni sawa na mtu afanye kazi ya kulima alafu malipo iwe ni kulima huko huko ndo malipo yake.akili yangu inakataa kabisa.
Waislamu tunajua kwamba baada ya kazi ni bata,sio baada ya kazi ni kazi hiyo hakuna.
Baada ya dhiki faraja kubaudu ni jambo gumu hivyo mwenye kulifanya lazima alipwe faraja.
Uislamu naupomgeza sana haukuwa mnafiki kabisa,umetaja wazi kwamba peponi tutapewa vile tunavyopenda.pepo ya waislamu hakuna kuabudu,huko ni burudani na kula raha kwa kwenda mbele unapata utakacho bila dhiki yeyote.