Wall street financial analyst is lying

Amesema matatizo ya nishati na vita yamechangia financial crisis, hayo ya mortgage defaults 'wall street finacial analyst' hakuyataja?
mkuu ndio maana nikasema kadanganya kama mtaalam wa uchumi na masoko ya kifedha huwezi kuongea mbele ya chombo cha habari na kusema mgongano wa kifedha umesababishwa na vita ya iraq na kupanda kwa mafuta.....

.....
 
- Duh jamaa umemshitukia kuwa ni mtupu? Acha kunivunja Mkulu UM mbavu Bwa! ha! ha! ah! ah! ha!

Respect.

FMES!
sisi wakazi wa kinyerezi hatuna muakilishi online wa kutusemea......

....hapa najua hugusi hamna longo longo zinaongea fact sio za chimwaga
 
sisi wakazi wa kinyerezi hatuna muakilishi online wa kutusemea......

....hapa najua hugusi hamna longo longo zinaongea fact sio za chimwaga

- Wenzako tunazo share huko labda tukupe darasa tu jinsi mchezo unavyochezwa huko Wall Street mkuu, hatusomi kwenye magazeti tu na online ni Alhamis tu nilikuwa pale 747 7Th Avenue, NYC kwenye ghorofa ya 21 unajua kufuatilia haya mambo mkuu, vipi unajua hiyo address ina jengo la nani? Haya ya wall Street huyawezi mkuu lakini tunaweza kukupa darasa ikibidi! Bwa! ha! ha! ah!

- Kinyerezi tunaishi wananchi makini sana na wote tunajuana pale wkenye kijiji, ujumbe umefika na nimewafahamisha kijijini kuwa umefika.

Respect.

FMES
 
Soma maelezo haya.....

Ukweli ni kwamba Mpasuko wa uchumi umeanzishwa na tatizo mmoja tuu nalo ni subprime meltdown ( Kushindwa kwa watu wenye kipato cha chini kulipa madeni yao ya nyumba).

Mpasuko ulianza kuonekana mwaka 2007 mwezi wa 8 siku ambayo Cit bank walitangaza hasara ya mabilioni ya fedha kwenye mapato yao ya nusu mwaka. Jee swala la suprime linachangia vipi? Habari ni hii; mwisho mwa miaka ya 90, chama cha democratic waliandaa mswada wa sheria ya kupunguza vigezo za kupata mkopo wa nyumba. Mswadwa huo ulipita na kuwa sheria. Mwanzoni mwa 2000 baada ya Bush kuingia madarakani agenda mpya ilikuwa ni kupandisha namba ya wanaomiliki nyumba kwa 5%. Vile vile mwanzoni mwa miaka hiyo ya 2000 wataalamu wa Hisabati wakaja na formula mpya ambayo inaweza kuchanganya riski kutoka kwa wakopaji mbali mbali na kutengeneza mfuko mkubwa wa wadaiwa ambao ukigawanya vipande vipande unaweza kuuzwa kama share (mortgage backed security maarufu kama derivatives).

Mabenki makubwa yakaona faida ya hizi security (yaai hii mifuko ambayo imetengenezwa kwa kuchanganya mikopo ya nyumba ya watu mbali mbali), ili likahamsha ununuzi wa madeni ya wamiliki wa nyumba kutoka kwenye benki ndogogo ndogo kwenda kwenye benki kubwa. Yaani mfano rahisi ni kwamba benki ya nyumba ya Tanzania wanakopesha, kisha wanachanganya mkopo wangu na wa Michuzi na wanawauzia bank kubwa kama CRDB, then CRDB wanakatakata hii mikopo miwili katika vipande vipande na kuviuza kwa wananchi mbali mbali duniani. TATIZO LINAKUJA KWAMBA Benki ya nyumba sababu haikai na hii mikopo hivyo inakuwa haijali nani anakopa sababu CRDB yeye atanunua kwa vyoyote vile. Hivyo matokeo yake ni kwamba mtu asiye na vigezo vya kupewa mkopo akawa anapewa bila tatizo lolote. SASA, SIKU YA SIKU IKAFIKA WATU WAKAABZA KUSHINDWA KULIPA MALIPO YAO YA KILA MWEZI KWENYE HII MIKOPO, HAPO NDIO HILI DHAHAMA LILIPO ANZA KATIKATI YA MWAKA 2007.

Wakopeshwaji walipoanza kushindwa kulipa malipo ya mwezi, maana benki kubwa zikaanza kushindwa kuwalipa wawekezaji walionunua shea, na Insuarence company (AIG) ambazo ziliweka bima kwenye hii mifuko zikaanza kushindwa kulipia na tatizo likaawa linazidi kutanuka.

Kwa nini John Mashaka is wrong? hii ni sababu; Uchumi wa Marekani mpaka mwaka 2008 kwa asilimia zaidi ya 40% ulikuwa ukishikiliwa na Mashirika ya fedha (financial Institutions). 40% Ya Index kubwa kama Standard and Poor 500(s&p 500) ni makampuni ya fedha. Kumbuka ya kwamba makampuni yote ya fedha kwa njia moja au nyingine yameusika kuuza hizi shea hewa kwa jamii. Matokeo yake ni kwamba kadri muda ulipozidi kwenda ndio watu walio kopeshwa nyumba walishindwa kulipa, na mabenki yanajiendesha kwa kukopesha na sio other wise. Sasa kama watu hawalipi madeni yao matokeo yake ni kwamba ukopeshaji unapungua na sheria za kukopa zikaanza kuzidi (ndio unakumbuka neno Credit Crunch lilitawala sana muda fulani). Sasa benki zinapoacha kukopesha maana yake ni kwamba Uwekezaji nazo unapungua, na kama uwekezaji zinapungua maana yake ni kwamba watu wanapunguzwa kazi.

Uchumi wa Marekani unaangalia mambo 3, Inflation (mlipuko wa bei), idadi ya watu wasio na kazi (unemployment rate) na ukuaji wa uchumi (economic Growth). Lolote kati ya haya matatu likisumbua ndio utaona seriakali inakimbilia kwenye mambo mawili yaani Fiscal Policy (kama kuwapa watu cheki za bure ili wakatumie) au monetary policy (Banki kuu ya marekani kupunguza kiwango cha riba.) Haya yote yamekwisha fanyika lakini hali bado ni tete. Makampuni makubwa ya fedha bado yanatapa tapa, mengi yamekwisha anguka. Sasa kumbuka kama 40% ya uchumi unategemea makampuni ya fedha haya makampuni yakiyumba kidogo tuu uchumi lazima uterereke.

Vita ya Iraq sio sababu ya kusumbua uchumi wa America, kama unajua uchumi vizuri utakumbuka ya kwamba Marekani ilikwenda kwenye dipression mwaka 1929, baada ya hapo mambo yalikuwa mabaya sana kwenye uchumi wa marekani, mpaka mwaka 1940 ambako America ilikwenda kwenye vita vya dunia. Na baada ya hapo Uchumi ulisimama. Uchumi wa America unategemea kazi na kama kazi zipo basi hakuna tatizo. Sasa sidhani kama vita ya Iraq ndio iwe tatizo, wachumi wengi hapa marekani hawaliweki hilo hata kwenye mabano.

Ongezeko la bei ya mafuta sio tatizo la kusumbua uchumi. Kumbuka ya kwamba Mafuta yamepanda bei kuanzia mwishoni mwa 2006 mpaka mwisho mwa 2008. Na mafuta yashapanda kabla, Ulaya wanalipa mafuta ghali kwa miaka yote mbona chumi zao hazitetereki? Jee kuna uwiano gani kati ya $80 na Economic downturn? I need data na sio kelele kama kasuku.
Bei ya mafuta sio kwamba yaliweza kuathiri mambo 3 Inflation, Unemployment rate and Economic growth na usipo adhiri haya mambo 3 huwezi kuyumbisha uchumi wa marekani.


Kwa kweli mimi siyo mchumi wala analyst.

LAKINI KATIKA POST ZOOOOTE ambazo niliwahi kusoma (including magazeti na TV za nje kama CNN nk kuhusu hii FC)...Hi POST ndiyo imenipa MWANGA hasa kuhusu hii Financial crisis. YAANI JAMAA AMEIELEZEA FRESH SANA. Huyu nampa respect. Maana hajapiga blah blah nyingi.,..yaani kitu kinasomeka na kueleweka hata kwa mtu ambaye elimu yake ni fupi. Bravo YO YO kwa kuitundika hapa....

Kwa kweli Mashaka mimi simjui zaidi ya kusoma story zake pale kwa misupu...lakini maelezo yake mengi hayaeleweki kabisa. Ila nilijisemea moyoni kama hawa ndo financial analyst wa Wall Street, No wonder the Financial sector is going under the drain....wako too academic..for common people kuwaelewa. HARAFU GUESS WHAT? WANAENDA KWENYE BLOG YA MITHUPU KUTUNDIKA IDEAS ZAO KULE...SASA SIJUI HAWAFIKIRII JAMAA WANAOPITIA ILE BLOG YA MICHUZI..HATA AKINA YAKHE WA DARASA LA SABA WAMO...ANYWAY..IN TZ ANYTHING IS POSSIBLE.....KAMA UMEAMUA KUWAELEWESHA WATU..GONGA KISWAHILI WATU WAKUELEWE..KAMA UNATAKA KIZUNGU INGIA JF KUTANA NA AKINA FMES NA KICHUGUU WAZEE WENYE SHULE NDEFU...
 
-Wenzako tunazo share huko labda tukupe darasa tu jinsi mchezo unavyochezwa huko Wall Street mkuu, hatusomi kwenye magazeti tu na online ni Alhamis tu nilikuwa pale 747 7Th Avenue, NYC kwenye ghorofa ya 21 unajua kufuatilia haya mambo mkuu, vipi unajua hiyo address ina jengo la nani? Haya ya wall Street huyawezi mkuu lakini tunaweza kukupa darasa ikibidi! Bwa! ha! ha! ah!

-
FMES
Lol wakuu mmemuelewa FMES?

mkuu fmes tupe darasa la financial crisi ya kwamba unapajua sijui una share haina maana kwetu....hatuitaji upige simu chimwaga.....
 
Yo Yo;

Soma maelezo haya.....

Ukweli ni kwamba Mpasuko wa uchumi umeanzishwa na tatizo mmoja tuu nalo ni subprime meltdown ( Kushindwa kwa watu wenye kipato cha chini kulipa madeni yao ya nyumba).

- Mpasuko wa uchumi umeletwa na tamaa za watu wa Wall Street, wakiwa encouraged na Clinton alipokuwa rais wa US na ile hands off approach katika ku-regulate big financial corporates.

- Msingi maalum wa Capitalism ni Free Market na serikali kuhakikisha kuwa na policies za zero tolerance inapokuja kwenye ku-regulate wale wanaoshika njia kuu za uchumi, mfano mzuri hapa ni Madoff ambaye pamoja na all red flags kua raised mapema kwamba alikuwa anavunja sheria, hakuna aliyemfuatilia na matokeo yameonekana sasa huwezi ku-playdown the impact ya tamaa yake huyu katika kuchagia mpasuko wa uchumi.

- Huwezi kukata short cut that fast, kwamba eti kwa sababu wananchi walishindwa kulipa madeni kutokana na kipato kidogo, kwa sababu watoaji mikopo wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanatoa mikopo kwa wale tu wanaoweza kulipa kwa kuonyesha satisfying financial cresidentials zao kwa watoaji kabla ya kupewa mikopo, hawa watoaji wakaanza kulifumbia macho hili kwa sababu ya tamaa za kupata hela ndogo za haraka haraka.

- Nilikuwa ninaishi huko hiki kipindi cha utoaji wa mikopo kiholera holera, ifact I almost joined tha train kwenye kuchukua mkopo wa nyumba, lakini nikabadili mawazo dakika ya mwisho na kui-nvest kwenye transportation industry, badala ya nyumba na magari kama wananchi wengi walivyoangukia huo mtego.

Hivi unajua kua tatizo zima la sasa la uchumi, lina-base na industry mbili tu, nzao ni nyumba na magari tu, ambako ndiko makosa makubwa yalikafanyika, I mean cha msingi hapa ni kwamba huwezi mpa mwananchi asiye na uwezo wa kulipa back mkopo wa gari na nyumba, halafu tena ukageuka na kumlaumu yule mwananchi kwamba ndiye chanzo cha kuharibika kwa uchumi, hapa mwenye tatizo ni mtoaji sio mpokeaji.

Ninaendelea kuiangalia post yako na kuichambua vizuri, maana I have lived hii crisis, hata ile ya 90s, ya baba yake joji kichaka alipokuwa rais.

Respect.

FMES!
 

Quote:Yo Yo

Mpasuko ulianza kuonekana mwaka 2007 mwezi wa 8 siku ambayo Cit bank walitangaza hasara ya mabilioni ya fedha kwenye mapato yao ya nusu mwaka

- Mkuu again naomba nikupe darasa zaidi kwa ufupi, ni kwamba Us congress walipitisha The 1933 Glass Act, baada ya kuitafakari kwa makini hali iliyosababisha The Great Depression, nia na madhumuni ya hii Act au sheria, ilikuwa ni ku-separate Commercial banking na Investment bankig, ambachio ndio hasa ulikuwa uti wa mgongo wa The Great Depression.

- Lakini kwa sababu ya tamaa mbele, Citi Group wakafanya lobbying ya ajabu kwa Congress, na mwaka 1999 Congress wakapitisha The Gramm-Leach-Billey Services Modernization Act of November 1999, ambayo kimsingi ilivunja nguzo zote zilizowekwa na sheria za ile ya mwaka 1933.

Matokeo yake ni sasa miaka 10 baadaye tunapata haya matokeo ya kupasuka kwa uchumi kwa sababu hii Act ya mwaka 1999 ilifanikiwa kutupilia mbali msingi mzito wa kutoa mkopo, yaani:-

1.Character, 2.Capital, na 3.Collateral.

kwa hiyo mkuu wangu yo-yo, ni kwamba sina muda wa kutosha tu lakini ningeweza kukupa darasa zito sana, na huyu Ndugu yako Mashaka, yupo mbali sana na ukweli.

Respect.

FMES
 
Mijadala mingi imeibuka na si jambo la ulazima uwe na degree ya uchumi ujue couses ya financial crisis duniani.Its a shame kwa msomi na mwanaharakati kama John mashaka kupotosha umma kuwa mtikisiko wa kiuchumi unaondelea sasa hivi umetokana na sababu moja wapo ikiwa vita ya Iraq na ongezeko la bei ya mafuta.

John mashaka kama msomi ni reflection ya wasomi wetu tunaowapa dhamana ya kutoa maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi na matokeo yake ni kutumbukiza kwenye matatizo.
Nimemsikiliza kwenye interview yake na daily news nikasitika….is this the man called financial analyst? Muoneni muongo mkubwa wa wall street

Daily News | The leading Online news edition in Tanzania

- Ona sasa ni nani aliyekwambia kwamba huyu kijana anafanya kazi Wall Street? Huyu kijana anafanya kazi kwenye bank branch moja kule North Carolina sio Wall Street mkuu, yaani mtu akipiga blah! blah! kidogo na uchumi uchwara anakwua mtu wa Wall Street? bongo bwana!.

Respect.

FMES.
 
- Ona sasa ni nani aliyekwambia kwamba huyu kijana anafanya kazi Wall Street? Huyu kijana anafanya kazi kwenye bank system moja kule North Carolina sio Wall Street.

Respect.

FMES.

Mkulu hebu nipe shule kwa lugha nyepesi, Serikali ya Nchi zinazoendelea zifanye nini ili kukabiliana na hili tatizo? Thailand nadhani serikali inagawia wananchi wa kipato cha chini mshiko! I am ignorant na hii kitu TBH

Pili kwa kama mwanachi wa kule Mwanalumango nayetegemea kuuza embe anatakiwa afanye nini?

Natanguliza shukrani
 

1. Mkulu hebu nipe shule kwa lugha nyepesi, Serikali ya Nchi zinazoendelea zifanye nini ili kukabiliana na hili tatizo?

2. Thailand nadhani serikali inagawia wananchi wa kipato cha chini mshiko! I am ignorant na hii kitu TBH

3. Pili kwa kama mwanachi wa kule Mwanalumango nayetegemea kuuza embe anatakiwa afanye nini?

Natanguliza shukran
i

1. - Mkuu wangu mimi sio mchumi, lakini kwa maoni yangu ni kwamba Tanzania na nchi zingine zinazoendelea itachukua muda mrefu sana kukumbwa na matatizo ya hili janga, Africans nations majuzi kule London wamedai kwamba wakaipewa Dola $ Billioni 50, basi zitatatua tatizo, lakini hawaku-mention ni tatizo gani? Kwa sababu kama ni kuahtirika kwa uchumi wa West, bado bongo hatujakumbwa na chochote kwa sababu bado hatujajikita kwenye biashara za kukopa kwa big time kwa wananchi wetu, binafsi ningewaomba tu benki zote za bongo zikatae kabisa kuwakopesha wananchi wasiokuwa na uwezo kurudisha hela wanazozikopa, kwa sababu kama bongo tungekua na system ya kukopa kama US by now tungekua tunakula majani.

- Huenda tunakula majani anyways, lakini sio kwa sababu ya kupasuka kwa uchumi wa dunia, ila ni ubovu wa policies zetu ambazo sio siri kwamba ni un-progressive, nchi zinazoendelea zinahitaji sana sasa kuungana na kuanzisha biashara baina yao, badala ya kutegemea biashara na West, lakini cha muhimu ni kujifunza kutokana na matatizo ya the west kujiepusha na kuanzisha system za kukopa kopa tu kama US, yaani wananchi wanaishia kwa kukopa tu na credit card, tusipojiingiza kwenye haya tutakua fine, kwa sababu the west ni soon watapata dawa ya matatizo yao.

- Tatizo kub wa zaidi tulinalo ni misaada na mikopo toka nje, kwa kweli hilo nalo linatisha sana, kwa sababu unajua mikopo mingi tunayolipa sasa hivi tunalipa interest tu lakini hatujagusa principle na wala hatutakuja kuweza kufikia kulipia principle, hili sinanuhakika tutalitatuaje as a nation.

2. Tatzio la kugaia wananchi mshiko ni kwamba hela zinazotumika kwa huo mshiko mara nyingi huwa zinakwua sio za ile serikali, kwa mfano US hela zote walizokwisha tumia os far ni za mkopo kutoka China, kwa sababu wakiingia kuchota hazina yao ya taifa, then inabidi kuwe na devaluation, kitu ambacho sio progressive kwa uchumi wa taifa, sasa unless you are US, sijui nchi kama Thailand itawezaje kuzirudisha hizo hela za nshiko iwapo hazitarudi intime au zikirudi zikiwa less, kwa sababu ni lazima in some cases taifa lipunguze kodi ya vitu ili kuurudisha uchumi tena, kwa Tanzania hili hatuliwezi la kugawa mshiko, ila sijui thailand wametoa hela ngapi za mshiko na wamezitoa wapi.

-3. Mwananchi wa Mwanalumango, anatakiwa tu ajiepushe na tamaa ya ammbo makubwa na kuridhika na maisha madogo aliyonayo ya kujinyima nyima, kwa sababu uwezekano wake wa ku-progress ni mdogo sana katika kpindi hiki kibaya cha uchumi.

In wabongo tunahitaji kujifunza kupunguza matumizi, kuaniza seriakli mpaka wananchi tunatumia hela vibaya sana, yaani sometimes unajiuliza kwamba eti hawa wananchi kweli wana shida, na hii serikali jkweli ina shida? Yaani maofisa wadogo tu wa serikali wanasafiri kwenye business class, first class, hivi unajua bongo to US na kurudi first class ni dola karibu $ 10,000 za US sasa uanjua wka mwaka wanasafiri mara ngapi? Inasikitisha sana.

Mkuu samahani sana kwa maelezo marefu, sina ujuzi sana na uchumi, ila niaujua mdogo sana wa kuniwezesha kuishi simple lakini,comfortable.

Respect.

FMES!
 
Mwananchi wa Mwanalumango, anatakiwa tu ajiepushe na tamaa ya mambo makubwa na kuridhika na maisha madogo aliyonayo ya kujinyima nyima, kwa sababu uwezekano wake wa ku-progress ni mdogo sana katika kipindi hiki kibaya cha uchumi.

Nimekuelewa asante sana!! hahahah mzee umeuwa mwananchi wa Mwanalumango na embe Ng'ongo zake hata weza endesha BMW X6 hahahaha..kama sisi tunatesa naza mikopo..Thanks a lot....

Nadhani misaada itapungua sana kutoka kwa wafadhili wa nchi maskini, hasa budget zetu tegemezi hali hii itatuathiri sisi wazee wa mabakuli..nchi hizi zimeweka strict regulation kama walivyoainisha kwenye G20.


Thanks again, nimejifunza kitu!
 
Wow!!! Jamani, instead of doubting his position at the Wall Street, lets debate his arguments. By the way he did mention about subprime meltdown as another factor of the current crisis. I also think he brought up energy as another factor. Anyways, I sometimes worry that our arguments become too personal and this just does not lead us anywhere. As far as I am concerned, there are so many Tanzania who have achieved so much and we should try to encourage them. I think Mashaka has become quite popular because he has a spotlight. Instead of discouraging him, we should rally behind his efforts. He is not always right, but he deserves constructive criticism.
Ciao
 
Wow!!! Jamani, instead of doubting his position at the Wall Street, lets debate his arguments. By the way he did mention about subprime meltdown as another factor of the current crisis. I also think he brought up energy as another factor. Anyways, I sometimes worry that our arguments become too personal and this just does not lead us anywhere. As far as I am concerned, there are so many Tanzania who have achieved so much and we should try to encourage them. I think Mashaka has become quite popular because he has a spotlight. Instead of discouraging him, we should rally behind his efforts. He is not always right, but he deserves constructive criticism.
Ciao

Nakubaliana nawe. Pia sababu ya kuanguka kwa uchumi inaweza kusababishwa na combination of factors. Wamarekani wanaweza kutopenda kuzitaja hizo sababu nyingine (mfano vita vya Irak na kupanda kwa bei ya mafuta) kwa sababu wanazozijua wao au haziwapendezeshi watawala. Lakini mtu mwingine kulingana na upeo wake wa kuangalia mambo anaweza kuunganisha matukio mbalimbali ili kujua kwa kina tatizo la kuporomoka kwa uchumi. Ndugu mashaka alijitahidi kuelezea sababu zaidi ya ile ambayo tunalazimishwa kuiclaim kuwa ndio sababu pekee.
 
Wow!!! Jamani, instead of doubting his position at the Wall Street, lets debate his arguments. ..... Instead of discouraging him, we should rally behind his efforts. He is not always right, but he deserves constructive criticism.

Hatuwezi ku-ignore kwamba jamaa sio mkweli kuhusu career yake. Mtu anaeongea kwa kuji introduce kama mtalaam wa Wall Street maana yake kile anachokisema ana mamlaka nacho na na ujuzi nacho kwa msingi wa uzoefu/kazi yake. Sasa kama anaongopa kuhusu hilo hilo hatuwezi kuli ignore.

Abaki huko huko kumdanganya Michuzi na wasomaji wa blog ya Michuzi, sio hapa. Hakuna Wall Street North Carolina.
 
Hatuwezi ku-ignore kwamba jamaa sio mkweli kuhusu career yake. Mtu anaeongea kwa kuji introduce kama mtalaam wa Wall Street maana yake kile anachokisema ana mamlaka nacho na na ujuzi nacho kwa msingi wa uzoefu/kazi yake. Sasa kama anaongopa kuhusu hilo hilo hatuwezi kuli ignore.

Abaki huko huko kumdanganya Michuzi na wasomaji wa blog ya Michuzi, sio hapa. Hakuna Wall Street North Carolina.

Jamani Mbona hilo la Mtaalamu wa Wall street sijalisikia au maskio yangu ndio mabovu? Nimeskikia akitambulishwa kama mtaalamu wa masuala ya kifedha anayefanya kazi katika masoko ya kifedha huko marekani. Je masoko ya kifedha wanamaanisha kuwa ni Wall street? Soko la kifedha ni wall street peke yake au kuna masoko mengine huko marekani?
 
Jamani Mbona hilo la Mtaalamu wa Wall street sijalisikia au maskio yangu ndio mabovu? Nimeskikia akitambulishwa kama mtaalamu wa masuala ya kifedha anayefanya kazi katika masoko ya kifedha huko marekani. Je masoko ya kifedha wanamaanisha kuwa ni Wall street? Soko la kifedha ni wall street peke yake au kuna masoko mengine huko marekani?


Hujasikia kwa sababu Daily News wameondoa the original interview, ambayo ilikuwa ya Kiingereza. Alidai yeye ni mfanyakazi wa Wall Street New York na North Carolina.

Siku hizi ameanza kurekebisha uongo, anasema New York na North Carolina. Zamani alikuwa anasema New York peke yake, alidhani watu ni wajinga sana hawajui Wall Street iko wapi. Sasa siku hizi anasema New York na North Carolina.

Bado hajaacha hako ka uongo ka Wall Street ya North Carolina, akaondoe hako. Au amdanganye Michuzi na wasomaji wa Michuzi.
 
Bado hajaacha hako ka uongo ka Wall Street ya North Carolina, akaondoe hako. Au amdanganye Michuzi na wasomaji wa Michuzi.

Binafsi nafikiri kuna aina fulani ya chuki dhidi ya huyu John Mashaka, na sidhani kama inatusaidia sana. Kwani iwapo tunauwezo mkubwa kuchambua masuala haya na kutoa suluhisho hasa kwa nchi zetu kama alivyo fanya FMES huu mjadala uongo wa kitoto kama mtu nafanya kazi sehemu fulani unamaana gani?au unafaida gani kwa mtu wa manerumango? Nafikiri tunamkuza sana huyu mtu hadi tunasahau mambo ya muhimu.
 
Yo Yo post nzuri sana,

FMES, FEDS sasa hizi wanafanya Nationwide crackdown ya hizi real estate scam.
 
Nakubaliana nawe. Pia sababu ya kuanguka kwa uchumi inaweza kusababishwa na combination of factors. Wamarekani wanaweza kutopenda kuzitaja hizo sababu nyingine (mfano vita vya Irak na kupanda kwa bei ya mafuta) kwa sababu wanazozijua wao au haziwapendezeshi watawala. Lakini mtu mwingine kulingana na upeo wake wa kuangalia mambo anaweza kuunganisha matukio mbalimbali ili kujua kwa kina tatizo la kuporomoka kwa uchumi. Ndugu mashaka alijitahidi kuelezea sababu zaidi ya ile ambayo tunalazimishwa kuiclaim kuwa ndio sababu pekee.
Ufisadi unaanzia hapo....yeye kama anavyojiita mtaalam wa fedha wa wall street hawezi kutudanganya sisi tusiojua a wala b ya uchumi.....hawa wsomi ndio waliotufikisha hapa na mitatizo kibao.......
BTW chech this
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=1EgGZoJyt7U"]YouTube - Keith Olbermann: The best explanation of the causes of the financial crisis you'll ever see[/ame]
 
Back
Top Bottom