Wall street financial analyst is lying | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wall street financial analyst is lying

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Yo Yo, Apr 5, 2009.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mijadala mingi imeibuka na si jambo la ulazima uwe na degree ya uchumi ujue couses ya financial crisis duniani.Its a shame kwa msomi na mwanaharakati kama John mashaka kupotosha umma kuwa mtikisiko wa kiuchumi unaondelea sasa hivi umetokana na sababu moja wapo ikiwa vita ya Iraq na ongezeko la bei ya mafuta.

  John mashaka kama msomi ni reflection ya wasomi wetu tunaowapa dhamana ya kutoa maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi na matokeo yake ni kutumbukiza kwenye matatizo.
  Nimemsikiliza kwenye interview yake na daily news nikasitika¬Ö.is this the man called financial analyst? Muoneni muongo mkubwa wa wall street

  Daily News | The leading Online news edition in Tanzania
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Heheheheheheehee....kapataje kazi huyu huko Wall Street? Anafanya kazi Wall Street kweli huyu?
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Nini hasa kimekushtua kuhusu JM.
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu mie nimemsoma "KUTOA NI MOYO,SI UTAJIRI"-JOHN MASHAKA - BongoCelebrity .....unajua wengi wakitoka majuu wanatuambia mengi na sisi huku tunawaamini kwa kuwa wanajua kingereza..
  ......kila akihojiwa na bbc swahili wamekuwa wakimtambulisha kama mtanzania anaefanya kazi soko la fedha New York au yapo mengi huko?

  Unajua na wewe mkuu hii ni bongo amekuwa akipiga ziara sana kesho keshokutwa utamsikia kawa waziri wako wa fedha...
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Apr 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  God forbid
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Hii ndio sababu iliyokufanya ugundue kuwa anadanganya?
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  lol nimetumia factor za kiuchumi hata binti yangu anajua kuwa financial crisis haijawa caused na vita vya iraq na kupanda kwa mafuta...
   
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bali? Nini chanzo cha financial crisis? Nijuze ndugu na mie niweze kujua uongo wa John Mashaka, asizidi kudanganya.
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Soma maelezo haya.....

  Ukweli ni kwamba Mpasuko wa uchumi umeanzishwa na tatizo mmoja tuu nalo ni subprime meltdown ( Kushindwa kwa watu wenye kipato cha chini kulipa madeni yao ya nyumba).

  Mpasuko ulianza kuonekana mwaka 2007 mwezi wa 8 siku ambayo Cit bank walitangaza hasara ya mabilioni ya fedha kwenye mapato yao ya nusu mwaka. Jee swala la suprime linachangia vipi? Habari ni hii; mwisho mwa miaka ya 90, chama cha democratic waliandaa mswada wa sheria ya kupunguza vigezo za kupata mkopo wa nyumba. Mswadwa huo ulipita na kuwa sheria. Mwanzoni mwa 2000 baada ya Bush kuingia madarakani agenda mpya ilikuwa ni kupandisha namba ya wanaomiliki nyumba kwa 5%. Vile vile mwanzoni mwa miaka hiyo ya 2000 wataalamu wa Hisabati wakaja na formula mpya ambayo inaweza kuchanganya riski kutoka kwa wakopaji mbali mbali na kutengeneza mfuko mkubwa wa wadaiwa ambao ukigawanya vipande vipande unaweza kuuzwa kama share (mortgage backed security maarufu kama derivatives).

  Mabenki makubwa yakaona faida ya hizi security (yaai hii mifuko ambayo imetengenezwa kwa kuchanganya mikopo ya nyumba ya watu mbali mbali), ili likahamsha ununuzi wa madeni ya wamiliki wa nyumba kutoka kwenye benki ndogogo ndogo kwenda kwenye benki kubwa. Yaani mfano rahisi ni kwamba benki ya nyumba ya Tanzania wanakopesha, kisha wanachanganya mkopo wangu na wa Michuzi na wanawauzia bank kubwa kama CRDB, then CRDB wanakatakata hii mikopo miwili katika vipande vipande na kuviuza kwa wananchi mbali mbali duniani. TATIZO LINAKUJA KWAMBA Benki ya nyumba sababu haikai na hii mikopo hivyo inakuwa haijali nani anakopa sababu CRDB yeye atanunua kwa vyoyote vile. Hivyo matokeo yake ni kwamba mtu asiye na vigezo vya kupewa mkopo akawa anapewa bila tatizo lolote. SASA, SIKU YA SIKU IKAFIKA WATU WAKAABZA KUSHINDWA KULIPA MALIPO YAO YA KILA MWEZI KWENYE HII MIKOPO, HAPO NDIO HILI DHAHAMA LILIPO ANZA KATIKATI YA MWAKA 2007.

  Wakopeshwaji walipoanza kushindwa kulipa malipo ya mwezi, maana benki kubwa zikaanza kushindwa kuwalipa wawekezaji walionunua shea, na Insuarence company (AIG) ambazo ziliweka bima kwenye hii mifuko zikaanza kushindwa kulipia na tatizo likaawa linazidi kutanuka.

  Kwa nini John Mashaka is wrong? hii ni sababu; Uchumi wa Marekani mpaka mwaka 2008 kwa asilimia zaidi ya 40% ulikuwa ukishikiliwa na Mashirika ya fedha (financial Institutions). 40% Ya Index kubwa kama Standard and Poor 500(s&p 500) ni makampuni ya fedha. Kumbuka ya kwamba makampuni yote ya fedha kwa njia moja au nyingine yameusika kuuza hizi shea hewa kwa jamii. Matokeo yake ni kwamba kadri muda ulipozidi kwenda ndio watu walio kopeshwa nyumba walishindwa kulipa, na mabenki yanajiendesha kwa kukopesha na sio other wise. Sasa kama watu hawalipi madeni yao matokeo yake ni kwamba ukopeshaji unapungua na sheria za kukopa zikaanza kuzidi (ndio unakumbuka neno Credit Crunch lilitawala sana muda fulani). Sasa benki zinapoacha kukopesha maana yake ni kwamba Uwekezaji nazo unapungua, na kama uwekezaji zinapungua maana yake ni kwamba watu wanapunguzwa kazi.

  Uchumi wa Marekani unaangalia mambo 3, Inflation (mlipuko wa bei), idadi ya watu wasio na kazi (unemployment rate) na ukuaji wa uchumi (economic Growth). Lolote kati ya haya matatu likisumbua ndio utaona seriakali inakimbilia kwenye mambo mawili yaani Fiscal Policy (kama kuwapa watu cheki za bure ili wakatumie) au monetary policy (Banki kuu ya marekani kupunguza kiwango cha riba.) Haya yote yamekwisha fanyika lakini hali bado ni tete. Makampuni makubwa ya fedha bado yanatapa tapa, mengi yamekwisha anguka. Sasa kumbuka kama 40% ya uchumi unategemea makampuni ya fedha haya makampuni yakiyumba kidogo tuu uchumi lazima uterereke.

  Vita ya Iraq sio sababu ya kusumbua uchumi wa America, kama unajua uchumi vizuri utakumbuka ya kwamba Marekani ilikwenda kwenye dipression mwaka 1929, baada ya hapo mambo yalikuwa mabaya sana kwenye uchumi wa marekani, mpaka mwaka 1940 ambako America ilikwenda kwenye vita vya dunia. Na baada ya hapo Uchumi ulisimama. Uchumi wa America unategemea kazi na kama kazi zipo basi hakuna tatizo. Sasa sidhani kama vita ya Iraq ndio iwe tatizo, wachumi wengi hapa marekani hawaliweki hilo hata kwenye mabano.

  Ongezeko la bei ya mafuta sio tatizo la kusumbua uchumi. Kumbuka ya kwamba Mafuta yamepanda bei kuanzia mwishoni mwa 2006 mpaka mwisho mwa 2008. Na mafuta yashapanda kabla, Ulaya wanalipa mafuta ghali kwa miaka yote mbona chumi zao hazitetereki? Jee kuna uwiano gani kati ya $80 na Economic downturn? I need data na sio kelele kama kasuku.
  Bei ya mafuta sio kwamba yaliweza kuathiri mambo 3 Inflation, Unemployment rate and Economic growth na usipo adhiri haya mambo 3 huwezi kuyumbisha uchumi wa marekani.
   
 10. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bado sijaelewa, naomba nieleweshe ulichoelewa hapo.
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Unataka ligi?
   
 12. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ligi ndio maelezo ya kueleweshana?
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  malezo yepi zaidi niliyo kuwekea hapo juu?

  au sijaelewa unataka nini mkuu?
   
 14. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mashaka zaidi ya sababu ya vita alitoa sababu gani nyingine? Je, hakutaja suala la morgage defaults?
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu kumbe hujamsikia vema......

  bonyeza ile link ya daily news msikie then tujadili......
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hivi jamaa ni financial analyst wa firm gani?
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu mie nasikia waki quote kama mtaalam wa mambo ya kifedha toka wall street wakati mwingine yuko north carolina anahudumu kule
   
 18. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Amesema matatizo ya nishati na vita yamechangia financial crisis, hayo ya mortgage defaults 'wall street finacial analyst' hakuyataja?
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ndo hapo ninaposhindwa kuelewa na mimi. Na kwa kweli nitashindwa kuelewa Wall Street analyst anayedai Iraq war imesababisha economic crisis, kama ni jamaa fulani tu then fine.
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Duh jamaa umemshitukia kuwa ni mtupu? Acha kunivunja Mkulu UM mbavu Bwa! ha! ha! ah! ah! ha!

  Respect.

  FMES!
   
Loading...