Wall Geckos: Mijusi hatari wa nyumbani wanaoweza kutekeleza familia yote kwa sumu. Chukueni tahadhari

Makala hii Kwa lugha ya kingereza inaeleza njia za kumdhibiti Mjusi hatari mwenye sumu Kali ya kuweza kutekeleza familia yote.

Huyu Mjusi makazi yake makubwa ni kweli nyumba ambapo hufuata wadudu.

Ikitokea Kwa bahati mbaya Akafikia chakula na wanafamilia wakaja kukila aisee hesabuni msiba Kwa Kila aliyekula.Huyo ndio Wall.

View attachment 2764803
Kama kinachozungumzwa kuhusu huyu mjusi kingekuwa kweli basi nusu ya watu wote duniani wangekufa!
 
Hao mjusi nyumbani kwetu wapo wengi kuliko maelezo, shuleni walikuwepo wengi hata jikoni, kwa bibi zangu wote hao gecko wapo.
Huwa nawapenda sababu wanakula wadudu hasa ukiwa na bustani inayolisha wadudu wanaoruka kama mbu.
Sipendi nyumba isiyo na mijusi huwa ni dalili ya uwepo wa kemikali na mazingira artificial sana. Kukiwa na kemikali nje huoni wadudu, wakikosekana wadudu huoni hao mijusi.

Kama wangekuwa na sumu hiyo basi wakulima wa ndizi wangeshakufa wote. Hao wadudu na migomba ni kama kijana wa Arusha na bangi
 
Dawa yao fuga paka tu. Mimi paka wangu amewamaliza mijusi yote na akaenda kwa jirani akawamaliza wote. Unampata mjusi mmoja mmoja naye akipatikana hamna rangi anaacha kuona mbele ya nyau
Paka akila huyo mjuzi anang'ata shuka, kiumbe pekee niliyeona anasurvive ni sisimizi wao bhana wanamla vizuri tu mpaka anaisha, sa sijui wanakufa ila kwa wingi wao ni ngumu kujua? hilo sifahamu.
 
Hao mjusi nyumbani kwetu wapo wengi kuliko maelezo, shuleni walikuwepo wengi hata jikoni, kwa bibi zangu wote hao gecko wapo.
Huwa nawapenda sababu wanakula wadudu hasa ukiwa na bustani inayolisha wadudu wanaoruka kama mbu.
Sipendi nyumba isiyo na mijusi huwa ni dalili ya uwepo wa kemikali na mazingira artificial sana. Kukiwa na kemikali nje huoni wadudu, wakikosekana wadudu huoni hao mijusi.

Kama wangekuwa na sumu hiyo basi wakulima wa ndizi wangeshakufa wote. Hao wadudu na migomba ni kama kijana wa Arusha na bangi
Ni kweli wana sumu tena kali sana kukaa kwenye migomba haimaanishi wanalamba ndizi kwa ndani ya ganda lake.
 
Ili uwamalize hao mijusi ni vema ufuge paka kwani ni chakula cha paka. Paka wanawakamata kweli kweli hao

Hata mimi nilikuwa sijui ni kwa nini Mtume Muhammad SAW alisema hao mijusi wauliwe ila karibuni hivi nikasoma sehemu kuwa wana sumu kali kuzidi nyoka.
Sometimes mnaweza msife ila mnaweza kuugua hasa maradhi ya tumbo.
 
Paka wanakula vizuri tu na hawafi hapa kwangu kila mara namuona paka anawakamata na kula na mbona hajafa. Mi huwa sipendi paka kabisa lakini nilipomuona anawala hao mijusi nikaamua kumuacha nilitaka nimtoe
Paka akila huyo mjuzi anang'ata shuka, kiumbe pekee niliyeona anasurvive ni sisimizi wao bhana wanamla vizuri tu mpaka anaisha, sa sijui wanakufa ila kwa wingi wao ni ngumu kujua? hilo sifahamu.
Wana
 
....Wameishakufa Wangapi Tanzania Kwa Mjusi huyo ?...
1695901928142.png

Watu watano wa familia moja ,baba, mama na watoto watatu wamefariki dunia kwa kula chakula chenye sumu iliyotokana na mdudu mwenye sumu jamii ya mjusi aliyedondokea kwenye chakula....
#EastAfricaTV
 
Acheni kulishana matango poli jamani msiandike vitu bila kufanya research.
FACT. WALLL GECKOS ( AKA HOUSE GECKOS)
AU MJUSI KAFIRI ARE NOT POISONOUS.

Ni kweli wana sumu tena kali sana kukaa kwenye migomba haimaanishi wanalamba ndizi kwa ndani ya ganda lake.
Sisi Waafrika huku kazi kulogana na uzinzi, ila binadamu kule duniani walishafanya classification ya reptiles hatari na hawa common house gecko hawapo kwenye wanyama wenye sumu.
Na wakati huo mjue asili ya hawa mijusi ni Southern Asia wamejazana uko.

Iko hivi, kutokana na kula wadudu mbalimbali huyu mnyama anakuwa na bacteria wengi na kusababisha magonjwa hasa ya tumbo kama akidondoka kwenye chakula na kisipashwe. Hayo mambo ya kulamba mwiko akaua familia ni story either ya watu hawajawahi ishi na hao mijusi au basi wana low thinking capacity.
Kama gecko ana sumu basi ninatype kutokea kuzimu, nishaishi nao sana na wanabanwa na milango wanatoa macho nawashika kwa mkono kuwatoa na sinawi mikono na siumwi hata homa.

Na hiyo migomba ndio habitat yake. Hao mijusi wangekuwa na sumu basi watu wa kwanza kujua wangekuwa Wahaya, Wachaga na Wanyakyusa walima ndizi. Lisingekuwa suala la blah blah lingekuwa wazi. Kuna sehemu unahitaji nguvu nyingi kuaminisha black mamba alivyo na sumu?

Hawa nyoka wengi ambao ni classified kuwa na sumu bado lethality yao inaweka kuwa 50% kwa mtu mmoja alafu common house gecko eti analamba mwiko tu anaua familia nzima na dunia haijui kasoro GT wa JF. Hii nchi ngumu sana hii
 
Vijijini kungekua na nyumba zisizokaliwa watu.

Ukisema akidondokea kwenye chakula akapikwa watu wasijue hapo naweza kukuelewa, lakini kwamba akikatiza sehem au akilamba kitu anaacha sumu ya kuua? Hapana.
 
Ilikuwa watu sio hii specie ambayo Ipo majumbani bongo ni aina nyingine. Ingekuwa hivyo jamii yote ya Watanzania ingeshaapukutika maana wapo Kila sehemu tunaishi nao na ni vigumu kuwamaliza
 
Sio Kweli

Home lizard au wengine wanawaita Wall gecko hana sumu kabisa na wala hana madhara kwa binadamu. Zaidi wana msaada mkubwa wa kukamata mbu, mende na wadudu wengine

Wapo wajusi wenye venom kama nyoka ila sio huyu

Wengine wanadai kuwa anasambaza magonjwa ila sio kweli

Kama una Mtu aliyeathiriwa na huyu Mjusi hebu tupe ushahidi hata kutoka kwa Daktari.
Wanadai akiangukia kwenye maji au chakula akafia humo ndiyo hutema sumu hiyo.
 
Sahihi mkuu.

Napsta tabu sana kuamini kwsmba huyu mdudu ana sumu kali kama tunavyoaminishwa.
 
Wanadai akiangukia kwenye maji au chakula akafia humo ndiyo hutema sumu hiyo.
Uongo. Matenki ya maji shule yangu ya msingi, sekondari na nyumbani kwetu hawa gecko walikuwa wanadondoka na hatujafa.
Mnapenda kuishi kwa hearsay leo mtu akiwababua ngozi hao mijusi akaipaki akadai ni dawa ya kuongeza maumbile na kutafuta team ya wapigakelele kama wanne mtanunua kwa sababu hizohizo za "wanadai"
 
Back
Top Bottom