Sabasaba
Senior Member
- Jul 12, 2007
- 102
- 54
Hii inakuwaje jamani, sheria ya umiliki ardhi kama mashamba inasemaje kuhusu hili wadau?
Serikali wilayani hapa Mkoa wa Pwani, imesema baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, waliouziwa mashamba katika kijiji cha Mwanzega wametapeliwa kwa sababu haijashirikishwa katika zoezi hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Henry Clemens wakati akizungumza kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho na Jeshi la Polisi Wilaya ya Mkuranga kwa mahojiano zaidi huku mtendaji wake akisakwa baada ya kutoroka kuhusiana na uuzaji wa mashamba hayo kiholela.
Alisema makundi ya watu kutoka jijini humo yamekuwa yakimininika wilayani humo kununua mashamba katika kijiji hicho bila ya serikali hiyo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuwa na taarifa.
Clemens, alisema makundi ya watu kutoka jijini humo yamekuwa yakimiminika katika kijiji hicho kupitia taasisi moja kwa lengo la kukabidhiwa mashamba ambayo imedai imewatafutia wakati si kweli.
"Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo, wilaya ipo karibu na jiji la Dar es Salaam, inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga kwa wanaotaka kuja wafuate taratibu kwa kupitia halmashauri, wasipitie katika asasi wasipitie kwa mtu wa kati lazima ardhi itolewe kwa uhalali," alionya mkuu huyo.
Clemens, alisema mwishoni mwa wiki watu 1,000 kutoka Dar es Salaam walifika wilayani humo na magari mengi wakidai wameletwa na taasisi hiyo kukabidhiwa mashamba ambayo imewatafutia bila ya tarafa, kata halmashauri na wilaya kufahamu mpango huo.
"Kuna umuhimu wa kujua ardhi kama ilitolewa kiuhalali je kuna watu wangapi watafika katika kijiji hicho kwa malengo yapi,licha ya kupewa ardhi lakini kijiji kina mamlaka ya kutoa eka 50 wakati watu wapo 1,000 halmashauri ndiyo yenye uwezo wa kutoa ekari 100 zaidi ya hapo ni wizara, kwa hiyo ekari 50 ndio zitakuwa halali hao wengine watapelekwa wapi? " Alihoji. Alisema uongozi wa wilaya hiyo uliwazuia watu waliouziwa baadhi ya mashamba wasifanye kitu chochote kwa vile kuna matatizo ya mipaka baina ya kijiji hicho na jirani cha Msorwa.
" ... tayari uongozi wa taasisi hiyo umeandika barua ya kuomba radhi kwa wilaya kwa usumbufu na wilaya imeridhia lililojitokeza na mambo mengine yataendeshwa kwa taratibu na sheria za ardhi zilizopo,tunataka amani iwepo siku zote" alisema.
Source: IPP media