Waliouza madafu kwenye futari ya Ikulu wahojiwa, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo cha NIT. Ni wauza madafu kweli?

Ni ngumu Sana, kuaminisha uma kua hao, Ni wauza madafu.
1.Wanajiamini Hilo Swala kwa Raia sio Jambo Jepesi.(Over Confidence)
2.Kwa Tanzania kumtambua mtu Kama Ni Askari au Mtumishi wa Srk Ni Jambo Jepesi Sana.
3.Muonekano wao sio wa mtu anae za madafu, na ukitaka kulikua Hilo Tumia mda wako kuonana na wauza madafu.
Alafu kama kweli ni wauza madafu...I expected kwa vile wamealikwa ikulu wangevaa atleast vizurii kuendana na location Lakin ukicheki wao wamevaa kawaida na makofia ikimaanisha wanajaribu kumaintain uhalisia wa muuza dafu...Kuna shida apoo...
 
Hawa wauza madafu watakuwa ni wa mchongo walishindwa kuonekana kama wauza madafu halisi kwa mionekano yao ilikuwa ina utata. Nilikutana na jibaba moja la miraba minne limeshiba mwili mzima linaonekana ni mtu wa mazoezi yaani linapiga chuma, ni baunsa machinga lilinikuta mgahawani nakula likawa linaniuzia mashine ya umeme ya kuua umbu huku likiwa linaongea kikakamavu nikalishitukia na kulishuku sio machinga wa kawaida. Mara likaagiza chakula likaanza kula. Cha ajabu likaanza kupiga simu huku linaongea kwa sauti kubwa likimlalamikia mke wake kuwa waachane limechoka tabia za mke wake hawaelewani, niliona kama anazuga iweje liongee kwa sauti kubwa mambo yake ya ndani mgahawani sie wengine mgahawani tusikie? Watu kama hawa huwa tunawaona kama wako kwenye kazi maalumu ya kitengo kwa jinsi approach mbovu wanazozitumia kama camouflage
 
Hivi vyuo vya kibongo unapata wapi muda wa kukariri madesa,course work na kwenda kufanya biashara ya kuuza madafu ambayo hujui mnunuzi atakuja kununua muda gani? Au wakiyafikisha hapo A-Z yananunuliwa yote kila siku?
Huna exposure wewe
Waulize wanaosoma Ulaya na marekani .Husoma na huku wanafanya kazi part time wengine ulinzi,supermark nk

Ukoo kwenye Dunia Yako mwenyewe ya kuota

Asilimia kubwa ya watanzania wasomao nje Husoma na kufanya kazi au biashara
Unatuaibisha wabongo Kwa ujinga ulioandika Hapa

Tatizo huna exposure
 
Hivi vyuo vya kibongo unapata wapi muda wa kukariri madesa,course work na kwenda kufanya biashara ya kuuza madafu ambayo hujui mnunuzi atakuja kununua muda gani? Au wakiyafikisha hapo A-Z yananunuliwa yote kila siku?
Kifupi wewe una pepo la umaskini .Na huwezi kuja kuwa mfanyabisha hata siku moja utaishia tu kuwa kibarua wa kuajiriwa au serikalini au Kwa Wahindi sababu huwezi anzisha hata biashara ya bodaboda sababu hujui wateja watatoka wapi na je utapata pesa kwenye kijiwe unapaki

Kifupi Kuna wanachuo wakipata mikopo hunumua bodaboda hawakabidhi mtu akiwa free anaendesha mwenyewe kujiongezea kipato.Ziko bodaboda kibao za wanachuo walioko Masomoni

Tunasifia marekani kuendelea.Marekani watu wanafanya kazi sana wakiwrmo.wanavyuo wanachuo Huwa msitari wa mbele kutafuta kazi yeyote ya kibarua ya kufanya akiwa free .Hana muda wa kupoteza unakuta anadoma akimaliza masomo.darasani mbio kusaka kibarua au biashara ya kufanya.

Hao wauza madafu hawana muda wa kupoteza ni Darasani akitoka anaenda mbio.kuuza madafu yake.

Huyo Kijana msomi anayesoma NIT yeye kazaliwa tukuyu mbeya kule hakuna madafu lakini kafika dar kajifunza kufanya hiyo biashara na akasema alipohojiwa kuwa akimaliza masomo anataka afanye kazi gani kasema yeye hachagui kazi kazi yeyote iwezayo mwingizia kipato atafanya hata isipokuwepo yeye ataendelea kujiuzia madafu yake anachojali kufanya kitu cha mwingizia kipato sio kukaa bute
 
Mbona povu linakutoka sana kuniaminisha vitu ambavyo huna elimu navyo?? Hivi haya maisha ya kusoma course 13 kwa semister 1 yenye miezi 3 unapata muda wa kwenda kukaa barabarani kuuza madafu?? Hivi unajua hustle za kutega kuuza hizo biashara ndogo ndogo halafu bado upate muda wa kwenda chuoni kusoma, kufanya assignments na revisions??

Au unajua maisha ya vyuo vya bongo unaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 4 asubuhi? Unajua biashara kweli wewe? Sidhani kama ulishawahi hata kusimama road kufanya hizo biashara ndogo ndogo.
 
Alafu kama kweli ni wauza madafu...I expected kwa vile wamealikwa ikulu wangevaa atleast vizurii kuendana na location Lakin ukicheki wao wamevaa kawaida na makofia ikimaanisha wanajaribu kumaintain uhalisia wa muuza dafu...Kuna shida apoo...
Mkuu,

Unataka muuza madafu avae suti wakati hana suti na katika mipango yake wala hana event ya kuvaa suti kwenda?

Unajuaje kuwa aina hiyo ya nguo si nguo zote walizonazo, unajuaje kuwa nhapo actually hawajavaa nguo zao nzuri kabisa?

Mtu kakupigia belo lake kali la Converse halafu unamchukukia poa?

Unajua huyo jamaa kwa hilo belo hata mitaa ya Bronx New York anaonekana anajua mapigo?
 
Mbona povu linakutoka sana kuniaminisha vitu ambavyo huna elimu navyo?? Hivi haya maisha ya kusoma course 13 kwa semister 1 yenye miezi 3 unapata muda wa kwenda kukaa barabarani kuuza madafu?? Hivi unajua hustle za kutega kuuza hizo biashara ndogo ndogo halafu bado upate muda wa kwenda chuoni kusoma, kufanya assignments na revisions??

Au unajua maisha ya vyuo vya bongo unaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 4 asubuhi? Unajua biashara kweli wewe? Sidhani kama ulishawahi hata kusimama road kufanya hizo biashara ndogo ndogo.

Huyo muuza madafu kaongea Yuko likizo hii ya pasaka Chuo kimefunga

Kasema yeye biashara hiyo hufanya siku za weekends na pia na akishatoka Masomoni chuoni yeye anakaa nje ya Chuo na wako wawili na yule Rafiki yake yeye hasomi ila wote ni washirika wanafanya biashara pamoja na ndie alimfundisha biashara Cha ajabu nini? nenda Chuo Cha uhasibu TIA wanachuo Wana Hadi vibanda vya kuchoma chips jioni ,sehemu za Mpesa,Tigo ,Pesa nk maduka ya Stationary nk
 
Mkuu,

Unataka muuza madafu avae suti wakati hana suti na katika mipango yake wala hana event ya kuvaa suti kwenda?

Unajuaje kuwa aina hiyo ya nguo si nguo zote walizonazo, unajuaje kuwa nhapo actually hawajavaa nguo zao nzuri kabisa?

Mtu kakupigia belo lake kali la Converse halafu unamchukukia poa?

Unajua huyo jamaa kwa hilo belo hata mitaa ya Bronx New York anaonekana anajua mapigo?
Unadhani kungekua na harusi ya Dada ake au ndugu yake angeenda amevaa ivyo kisa anauza madafu??...unazan Hana Ata suruali na sharti la kuzugia kukitokea event za kijamii.....unadhan alikosa dress code ya kanzu ambayo ndo ilitajika ili uweze kuingia.....unazan alikua hajui wanaenda kukutana na raisi kwaiyo atleast walipaswa kuvaa vizuri kidogo.....Yan Ata ungekua wew unauza madafu unaambiwa utaenda ikulu uwezi vaa ivyooo...infact kama ni wanachuo uko chuoni wanavaaga nin kama hawana Ata suruali na shart la kuzugia?
 
Kitu kikubwa kabisa ni kwamba hakuna ushahidi kwamba hao watu si wauza madafu.

Hayo mambo ya unadhani unadhani unaweza kudhani vyovyote unavyotaka kudhani, ukabaki unadhani tu. Kudhani si ushahidi, hapa unatakiwa ushahidi.

Wewe unaweza kudhani muuza madafu atavaa vizuri hivi, kumbe mwenzako hapo ndiyo anaona kavaa vizuri, nguo zake za kila siku zinaweza kuwa za viraka hapo ndiyo kajitahidi kabisa.

Mimi huwa naona hakuna sehemu ya kuvaa kwa heshima kama kwenye msiba, kumzika mtu.

Lakini wabongo wanavyovaa kwenye misiba huwa nashangaa.

Lakini, baada ya kushangaa, huwa najiuliza, hawa watu pengine hiyo ni kawaida kwao mtu kwenda kuzika na jezi ya basketball ya "Boston Celtics". Habari za suti nyeusi ni itifaki ambazo hata hawazielewi wala kuzifuatilia.

Sasa watu kama hao, unaweza kukuta wamechagua kati ya nguo zao nzuri kabisa za kwenda Ikulu wakakuta ni T- Shirt ya Converse.

Wabongo wa kawaida hawana standards wala protocol kwenye mavazi.

Utasemaje huyu si mbongo wa kawaida kwa sababu hana standard wala protocol kwenye mavazi? Hiyo ndiyo kawaida yao!

If anything, hao jamaa wangevaa suti kali au kanzu kali ndiyo ningesema hawa si wauza madafu wa kawaida.
 
Juzi Rais alialika wasanii (chawa?) wakajumuike nae Ikulu kwa ajili ya kupata futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao ndio ilikua chungu cha kwanza, jambo jema!

Baada ya hapo taharuki kuu imejitokeza baada ya picha ya Rais Samia akikatiza mbele ya wauza madafu wawili ambao walikua wamesimama kwa utii na upole(ukakamavu kiasi).

Swali la kujiuliza wauza madafu wale walikua na mapanga na mabisu yao kwenye viuno na mtenga kama wauza madafu wa mitaani kwetu?

Ikiwa waalikwa walipewa mualiko wa karamu ya chakula, wauza madafu walikua pale kwa ajili ya kumuuzia nani?!! Kwa mamia ya watu waliolikwa, tenga 2 za madafu zingewatosha wakina nani? Tutarajie siku nyingine wauza pweza, ngoka 11 nao kujumisha?

Mwezi mtukufu, kuna ulazima wa kuleta matukio ya kupika?

Ukiwaza kidogo nje ya box,ikiwa maigizo Hadi kwenye mambo ya mwezi mtukufu,je mambo mangapi muhimu na nyeti Watanzania wanafanyiwa hadaa na maigizo?

Imenikumbusha enzi za Magufuli kusambaziwa picha akiwa kijiweni anakunywa gahawa na walalahoi huku walalahoi hao wakiwa na fulana zenye nembo ya serikali ya Bibi na Bwana!

Matumizi mabaya ya bando kwa Shughuli zisizokuingizia kipato
 
Usimamaji, nywele, ndevu , ukakamavu na vingine vingi vinaonyesha hao ni askari, sio wauza madafu, wauza madafu Hawana ndevu
Sasa wewe shida yako ni nini, Badala ya kuwaza mambo yanayoweza kukuingizia pesa, haya basi kama ni askari analipwa, kama ni Muuza madafu bado kalipwa, wewe?
 
Huyo muuza madafu kaongea Yuko likizo hii ya pasaka Chuo kimefunga

Kasema yeye biashara hiyo hufanya siku za weekends na pia na akishatoka Masomoni chuoni yeye anakaa nje ya Chuo na wako wawili na yule Rafiki yake yeye hasomi ila wote ni washirika wanafanya biashara pamoja na ndie alimfundisha biashara Cha ajabu nini? nenda Chuo Cha uhasibu TIA wanachuo Wana Hadi vibanda vya kuchoma chips jioni ,sehemu za Mpesa,Tigo ,Pesa nk maduka ya Stationary nk
Only fools like you will buy that bs. Yaani watu wa usalama wakuamini tu kiwepesi kwasababu unafanya biashara ya kuuza madafu siku za weekend tu ...siku nyingine hawakuoni. Halafu waachwe watu ambao daily wanauza madafu hapo aje achukuliwe yeye anayeonekana kijiweni mara moja moja?
 
Watu wa usalama unawaonaje mbona Hadi Kwa mama nitilie tunakula nao
Shida Nini ? Tunakula Hadi mishikaki na wakubwa tu wa vyombo vya usalama mtaani

Kwenu labda hamna hata ndugu wa usalama .Hilo tatizo la kwenu ndio maana unashangaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom