Kuhusu kuua huyu mzee hakuwa muuaji hata kidogo. Hapa tumpe haki yake kabisa. Hata wale waliostahili kuuawa yeye hakusaini wauawe. Katika uongozi wake wa zaidi ya miaka 20 nasikia alisaini wauawe watu wawili tu ( ambao hata wewe ungesahini). Ina semekana mmoja alimuua binti yake ili apate malipo ya bima.
Vile vile nakumbuka Marehemu Mohamed Babu (RIP) kusema kuwa Nyerere alimwokoa asiuawe, hivyo alikuwa anawajali hata watu wengine mzee wa watu.
Kwa upande wa kuwatandika Bakora kama ilivyoanishwa na TBC katika kipindi chake Mimi siungi mkono kabisa, nafikiri hapa alipotoka. Mwanzoni nilifikiri ni porojo kumbe wapi.Hii inaonyesha ni jinsi gani akishaona jambo lina manufaa,.alikuwa anajituma kupita kiasi kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa.
Kwa ujumla mzee huyu alikuwa na nia nzuri kabisa karibu katika kila move aliyoianzisha mfano JKT, vijiji vya Ujamaa n.k. Lakini katika kila jambo kuna uzuri na ubaya wake. Kwa vijiji vya ujamaa ukitembelea vijiji vya nchi nyingine kama Kenya na Uganda ndipo utajua uzuri wa wazo lile. Huku kwetu kuna mpango angalau lkn kwa wenzetu ni tofauti kabisa.
Tukirudi nyuma kuna mtu kaongelea porojo juu ya viongozi wetu wakuu, hasa Mwl. Na mzee Kawawa kweli kwa watanzania Documentation ni sifuri. Mambo mengi ya uongo yanasemwa, kwa kuwa hakuna anaye yakanusha yanaonekana ya kweli wakati sivyo.
Mwisho mjadala huu ulianzishwa kwa nia ya kupata mawazo ya watu juu ya mambo yaliyojiri siku za nyuma, Hii itatusaidia wakati mwingine tukipewa nafasi tujue jinsi ya kukabiliana na changamoto mbali mbali katika utendaji kazi.
Majina yaliyotumika mwanzoni BMW na JKN ni ya kusadikika tu kwa nia ya kuanzisha mjadala na kichwa cha habari kwa nia hiyo hiyo pia.
Mkitaka kufahamu mazuri ya Mwalimu angalieni yanayotuandama sasa hasa baada ya yeye kuwa ameondoka hapa DUNIANI. Angalau nimemsikia Msekwa jana akikiri hadharani kuwa walikosea kuiacha MIIKO na MAADILI ya UONGOZI alioiacha Mwalimu.
Bluray,
Kama kuna kosa ambalo naweza kusema Nyerere alifanya ni hili la Urithi ktk UONGOZI..
Kifupi navyomjua mimi Nyerere hakuwa mjanja katika hilo, hata wanawe mwenyewe aliwapenda zaidi waliopwaya kiakili..Sielewi kama ilikuwa ugonjwa au alitaka zaidi control..
Pengine ni jadi yetu maanake sisi Miafrika, mtoto juha juha na mpole sana ndiye tunampa sifa za mtoto mzuri! Yule makeke na anapenda kum challenge mzee huyo ni mhuni na hasara atapigwa laana.
Blueray,
Uongozi hauandaliwi na mtu mwingine. Uongozi ni hulka. Mwulize Mkapa alijifunza nini kutoka kwa Nyerere. Mwulize Obama aliandaliwa na nani?
Blueray,
Uongozi hauandaliwi na mtu mwingine. Uongozi ni hulka. Mwulize Mkapa alijifunza nini kutoka kwa Nyerere. Mwulize Obama aliandaliwa na nani?
ndiyo nyie nyie mnaoacha watoto bila ya kuwaandaa kwa maisha.
Uongozi ni hulka na si kila mtu ana hulka ya uongozi.Tukishajua hilo, rais, kwa sababu the buck stops at his desk, anatakiwa kuchagua watu wenye hulka ya uongozi na kuwaweka kwenye team yake, aka wa groom kiasi kwamba akiondoka yeye wawe na uwezo wa kuongoza.
Julius,ndiyo nyie nyie mnaoacha watoto bila ya kuwaandaa kwa maisha.
Uongozi ni hulka na si kila mtu ana hulka ya uongozi.Tukishajua hilo, rais, kwa sababu the buck stops at his desk, anatakiwa kuchagua watu wenye hulka ya uongozi na kuwaweka kwenye team yake, aka wa groom kiasi kwamba akiondoka yeye wawe na uwezo wa kuongoza.
Sasa obviously Nyerere alikuwa failure, kitu pekee chenye jina lake kilicho survive mpaka sasa ni muungano, ambao unakufa soon anyway.Kwa hiyo sitegemei failure huyu awe na uwezo wa ku groom watu waende kuongoza nchi.
Unahitaji dikteta. Nionyeshe dikteta mmoja wa Afrika aliyefanya vizuri?Bluray,
Mkuu katika hilo mimi nipo na Nyerere.. Tanzania inahitaji Dikteta huu mpango wa Ubia umetufikisha hapa tulipo. JK anashindwa kufanya maamuzi muhimu kwa sababu nyuma yake kuna wajanja kupindukia...
Ukweli wa mambo naanza kuona kwanini MIAFLIKA HIPO ILIVYO. Mawazo ni kitu muhimu sana. Kushabikia kupiga viboko ndio kumejenga nidhamu ya woga. Na sishangahi kwanini mijitu kama JK iliyoenda shule kwa nidhamu ya woga kushindwa kuongoza.
Unahitaji dikteta. Nionyeshe dikteta mmoja wa Afrika aliyefanya vizuri?
Zakumi,
Muamar Ghadafi na Hussein Mubarak hawa wamefanya vizuri kuliko marais wote wa demokrasia combined...
Zakumi,
Muamar Ghadafi na Hussein Mubarak hawa wamefanya vizuri kuliko marais wote wa demokrasia combined...
Zakumi,
Muamar Ghadafi na Hussein Mubarak hawa wamefanya vizuri kuliko marais wote wa demokrasia combined...
Acha Afrika..kwani Afrika ni nchi gani inayofanya vizuri ukiondoa Afrika Kusini. Wapi duniani dikteta aliyefanya vizuri?
Hapa watu wasichanganye kati ya rule of law na dictatorship? Vitu viwili tofauti kabisa
Tuko pamoja. Rule of law na udikteta ni vitu viwili tofauti. Lakini wajomba kwa kuona hawaendelei wanataka kukimbilia udikteta. Mchukueni Mugabe.