Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

1.Sijafananisha afya na elimu ya ulaya na tz....hilo unalisema wewe.
2.Nimedanganya?! Unanifahamu wewe au unaongea tu?!
3.Una matatizo ya kuelewa? Home sickness nimekwambia wakati niko Ulaya sijawahi kupata huo 'ugonjwa' kwasababu nilikuwa na uwezo wa kurudi anytime i want.
4.Kama wewe unaona Ulaya kuna fursa kuliko Tz baki, mimi nimemjibu alieuliza kwanini mtu anaamua kurudi.
 
Siri ya kuishi nje ni hii: nenda kasome ikiwezekana mpaka hata PhD pata kazi yako nzuri work hard na hakuna atakayekusumbua. Bongo ni kuzuri sana mpaka siku ukipata medical emergency kama heart attack, stroke, kansa ...halafu uwe huna hela za kwenda India. Aisee unakufa ka mnyama. Niliwahi kusoma Boston USA kwa miaka 7 na yes kuna mambo mazuri na mabaya kila sehemu. Miaka 7 yangu sikuwahi kubaguliwa wala kutendewa vibaya na polisi na ukiwa serious hakuna atakayekugusa. Huduma za afya kwangu hasa ndo jambo linalonikera hapa Bongo. Mtu unapata medical emergency hakuna cha ambulance, helicopter wala paramedics. Mijitu inajazana kupiga soga na kukuibia if possible. Yaani unaweza kufia pembeni mwaka barabara ka mnyama. Hata hospitali huko nako mambo yale yale tu...
 
We huoni wageni walivyojazana Tanzania ndo ujiulize wanapapendea nini? Kama ni matatizo yapo kila sehemu hata hivyo unatakiwa utatue tatizo na si kulikimbia.

Na wewe umefanikiwa kuona fursa zipi kama hao wageni?

Ushawahi hata kuwaza kumiliki mgodi? Lakini wachina wanakuja ndani ya miaka miwili tayari wanamiliki migodi.

Fursa za Tanzania ni kwa ajili ya wageni na sio wananchi.

Jaribu kujenga kiwanda uone..
 

Unachokiona ni kama mimi..

Mambo mengi tanzania yanakera sana.
 
From horse's mouth....
5.Fursa Tanzania:Hii ndio sababu kuu hata wewe kama uko huko ukiona fursa Tz usiiache maanake wazungu wanawaacha huko wao wanakuja huku na briefcase tu wanarudi na mamilion ya $$.

Hapan unadanganya.

Ushawaza kujilinganisha na mgeni kwenye kumata fursa Tz?

Jaribu kufanya kile mgeni anafanya uone nani atapewa kipaumbele zaidi..
 

Unachokiona ni kama mimi..

Mambo mengi tanzania yanakera sana.
 
tuko tunaendelea kupambana "positive vibrated" nje. maisha ni kuchagua.
 
@?Tangazo mahsusi :Leo umekula like yangu ya kwanza.
 
Mkuu Watanzania ndo tunapenda sana nyumbani ila Wanaijeria, waghana, wavenezuela, waarabu (Pakstan, Iran, Iraq), East Africa yote kasoro Tanzania hawarudi nchini.

Nadhani tuna uoga wa kuishi mbali na nyumbani na nyumbani kuna fursa nyingi sana na uhuru pia
 

Hiyo ndo concern yangu kubwa.

Umeishi sehemu yenye huduma bora, unapaacha then unarudi Tz wenye huduma za hovyo hivi?
 
Nadhani tuna uoga wa kuishi mbali na nyumbani na nyumbani kuna fursa nyingi sana na uhuru pia

Inawezekana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…