Wacha waende mahakamani tu, ni haki yao ya kikatiba na kisheria.
Sasa unapo conclude kwamba serikali italipa mamilioni ya shilingi, wewe ndiye jaji utakayekabidhiwa kesi hiyo ili uitolee judgement kwa favour ya makampuni yanayokusudia kwenda mahakamani? au basi tu umeamua kuchukua mikoba ya sheikh yahya!!??
Nyenyere
Kwa ujumla kitendo cha PS kuingilia mchakato wa zabuni kwa kuipa zabuni kampuni ambayop haikushida/haikushiriki ni ukiukwaji wa dhana nzima ya zabuni na ushindani wa kibiashara. Kama kweli kulikuwepo na vitu ambavyo havikukaa vizuri kuhusiana na zabuni, njia sahihi ingalikuwa na kufuta mchakato wote na kuanza upya na kuweka vigezo ambavyo vingezuia makampuni ambayo yalifanya malpractice katika mchakato wa awali.
Kwa jinsi alivyofanya PS, amezuia tanesco kuweza kujua/kupata bei ya chini (maana tuna uhakika gani kama hiyo bei ya puma ndio ya chini, kama mchakato wake haukuhusisha washindani wengine)! Hii tug-of-war yote tunayoishuhudia, hakuna upande ambao umetanguliza maslahi ya taifa mbele. Wote wanatizama 'matumbo' yao kwanza!
Usiangalie kushinda tu angalia na makando kando mengine yatayomfanya mshindi apewe kazi, umeambiwa accounting officer hasa vetto on any issue regarding procurement provided is for public interest period.Kina zitto wana kesi ya kujibuMkuu asante kwa observation yako. Niliandika hivyo kutokana na ukweli kwamba haya makampuni matatu yalishinda zabuni na kuagiza mafuta hayo. Wakati yakiwa katika mchakato wa kupeleka mafuta hayo ndio ikaja taarifa ya zabuni kusitishwa. Vipi kuhusu hizo hoja nyingine?
Bado sijaona tatizo la Mh. Zito mpaka sasa unless rushwa ithibitike. Hapa nahisi kuna political motive.
Usiangalie kushinda tu angalia na makando kando mengine yatayomfanya mshindi apewe kazi, umeambiwa accounting officer hasa vetto on any issue regarding procurement provided is for public interest period.Kina zitto wana kesi ya kujibu
Hapana. Sipendi ufisadi na pia sipendi mafisadi. Lakini napenda sheria na principles. Ninachokisema hapa ni kuwa bila PUMA kushindanishwa na washindani wengine (kwa kutumia vigezo vya Maswi) tunajuaje kuwa bei yao ndio ya chini kuliko ile ambayo ingepatikana kama washindani wote wangeambiwa walete zabuni upya (kwa vigezo vipya)? Actually alichofanya Maswi apparently inaweza kuonekana kuokoa pesa lakini bado ni kiini macho kwa sababu ametufanya tulinganishe bei ya PUMA na zile za makampuni mengine lakini bei hizo hazikutolewa katia level playing field (PUMA alikuwa tayari anajua wengine wame quote bei gani!). Kwa mfano, kama sasa hivi wakisema waitishe zabuni hiyo upya, si kweli kuwa almost makampuni yote yataleta bei ya chini ya hiyo ya PUMA? - na hivyo taifa kuokoa gharama zaidi.Kwa hiyo mwenzetu uko happy na ufisadi.Mimi ninavyoelewa ni kwamba accounting officer ndiyo mwenye discretion ya kubadili upepo kama kwa kufanya hivyo ni kwa maslahi ya taifa.Hii imeonyesha alichofanya accounting officer/PS ni kwa maslahi ya taifa considering the matriality of the financial implication in terms of saving.Kwamba angeokoa shs.3billion kwa wiki mbili na hivyo 6bln kwa mwezi ni justifiable kuingilia na sheria imeruhusu.Akina zitto na wenzake imekula kwao.Maswi is safe for ever
Unaelezeaje kisheria kwamba tayari washindi wa zabuni walishapatikana na kuagiza mzigo kabla ya kuambiwa zabuni imefutwa. Are they not eligible kupewa compensation for damages resulted?
Kama habari iliyoandikwa na mwandishi Exavery Mzuzu wa Dira ya Mtanzania itakuwa kweli, basi sakata la zabuni ya mafuta TANESCO litachuma mapesa mengi kuliko linavyodhaniwa kuokoa. Mwandishi huyu anaripoti kuwa makampuni yaliyoshinda zabuni kabla ya kutenguliwa na katibu mkuu Maswi yamekimbilia mahakamani kudai fidia. Sasa sijui hili suala kisheria limekaaje, maana hawa PUMA walichofanya ni kuchungulia wenzao wametoa offer kiasi gani halafu wao wakashuka chini yao. Je hii siyo unfair competition?
Pia hivi hatuoni kuwa kuna madhara makubwa sana kama tutaruhusu individuals kuingilia michakato ya kisheria kwa kigezo cha kuokoa "maslahi ya taifa?" Kitendo hiki hiki tunachokiona ni cha kishujaa leo hii, baadaye kitatuumiza vibaya sana. Ni uzalendo huu huu ndio uliogeuka mwiba mchungu kwa Mh. Lowasa. Kwani ilikuwa ni lazima mshindi wa zabuni apatikane kama makampuni yaliyoomba yalitoa bei kubwa? Sheria za manunuzi ya umma zinasemaje kuhusu hili? Kwa nini zabuni isingetangazwa tena ili kuruhusu makampuni zaidi kushiriki (wakiwemo PUMA)?
Kauli aliyotolewa na waziri kuwa wanaodhani bodi haitaingiliwa wanajidanganya inaiweka wapi bodi. Je, kautamaduni haka kakijichimbia mizizi si ndio itakuwa loophole ya ufisadi? Tunashangilia leo bila kujua nini kinakuja kesho. Si lazima itokee kwa waziri aliyepo sasa, inaweza kutokea hata katika wizara nyingine pia, na tutapaswa kuwaelewa na kuheshimu uzalendo wao.
Suala jingine la msingi kabisa hapa: kama kweli PUMA nao walishiriki zabuni ya kwanza na bei yao ikawa juu hadi walipogundua wameshindwa ndipo wakashusha, walitaka kufanya ufisadi pia? Vipi kama makampuni mengine nayo yangepewa nafasi ku-bid kwa kigezo kuwa mshindani wao PUMA kashusha bei, je kuna uwezekano tungewezapata bei chini zaidi ya hiyo 1460/=?
Disclaimer: Mimi si msomi wa sheria za manunuzi au sheria kwa ujumla. Hii ni tafakuri yangu tu.
Mkuu asante kwa observation yako. Niliandika hivyo kutokana na ukweli kwamba haya makampuni matatu yalishinda zabuni na kuagiza mafuta hayo. Wakati yakiwa katika mchakato wa kupeleka mafuta hayo ndio ikaja taarifa ya zabuni kusitishwa. Vipi kuhusu hizo hoja nyingine?
Bado sijaona tatizo la Mh. Zito mpaka sasa unless rushwa ithibitike. Hapa nahisi kuna political motive.