Walionunua hisa za DSE kurudishiwa fedha

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Habarini wanajamvini!
Kwa wale wenzangu wadau wa mambo ya soko la mitaji na mambo ya hisa , hi taarifa ni muhmu.
Kuna taarifa za ndani toka DSE dar es salam stock exchange, ambao juzi walijiorodhesha katika soko na kubadili mfumo toka private nature to public nature. Process hyo ilihusisha uuzwaji wa hisa za DSE, kwa hyo waliotaka kununua waliweza kufanya hvo.

DSE walitoa matangazo mengi sana magazetini, redioni, televisions kuhamasisha watu wakanunue hisa zao, na nadhani watu waliitikia wito na kwenda kununua.

Cha ajabu kitakachofanyika, wamesema watawarudishiwa baadhi ya watu fedha zao ili wabaki watu wachache tu wenye kumiliki hsa hzo za DSE wengi wao wakiwa ni Wageni.

Chakusikitisha, kuna watu wameuza nyumba, magari, mifugo, mikopo, ili tu wakawekeze huko DSE, sasa hi ya kurudisha fedha inakuwa ni tatizo sana. Sasa kwanini walitangaza kama walikuwa hawataki watu wanunue.

Kweli nimeamini ukitaka kuwa maskini tanzania ingia katika biashara ya hisa.
 
Hisa za kampuni gani? DSE inafloat hisa za makampuni mengi,sasa ukisema tu wanarudisha pesa taarifa inakuwa haijakamilika... kurudisha pesa hutokea na ni kawaida pale inapotokea over subscription ya hisa katika kampuni flani,kama ilivyowahi kutokea NMB walivyoweka sokoni hisa kadhaa miaka ya nyuma.
 
Wote tutakataa kurudishiwa fedha zetu vinginevyo tutasonga nao Mahakamani.
 
Mnyika pesa za mfuko wa jimbo kanunulia hisa huko DSE.. Bora wazirudishe zitumike kutuletea maendeleo jimboni
 
Hiyo ndo Tanzania. Unashangaa hilo tu na Hali kuna wafanyakazi walioajiriwa mwezi may na walilipoti kazini na kuitumikia serikali Kwa mwezi may na June na kuambiwa warudi home until further notice. Hii ndo Tanzania. Hapo mtu moshi mwingine alishaacha kazi Kwa mwajiri wake wa awali hapo Sasa ndo Hali inapokuwa ngumu
 
Mnyika pesa za mfuko wa jimbo kanunulia hisa huko DSE.. Bora wazirudishe zitumike kutuletea maendeleo jimboni

hujaelewa hi hisa zipi. hizo habari za mnyika kuwekeza zilikuwepo hata kabla DSE hawajafanya demutualization.
 
Hzi ni habari toka ndani kwao wenyewe. Hawawezi kutangaza watatumbuliwa, wanataka kufanya kimya kimya

sijawahi kusikia kitu kama hicho. na kama ni kweli basi ni janja ya kupaisha hisa zao zionekane zina thamani.
 
Hili ni jambo la kawaida, kibiashara inaitwa over subscription, yaani kama ulitaka milioni 100, kwa kuzigawa katika hiza 100 za shilingi za elfu moja moja, wakajitokeza watu 500, wewe utachukua hisa za watu 100 tuu, on the basis of first come first saved na wale 400, watarudishiwa fedha zao!.

Ununuzi wa hisa unafanywa kwa mnada, ila mnada huu sio wa highest bidder, bali ni wa fixed number of shares, minadana ya wazi ukishindwa unarudi na fedha zako kusubiria mnada mwingine!.

Pasco
 
Mnyika pesa za mfuko wa jimbo kanunulia hisa huko DSE.. Bora wazirudishe zitumike kutuletea maendeleo jimboni
Umeingiza siasa za kipuuzi tena!!
Hi I habari inatugusa wengi bila kujali cheo cha mtu.
Ni nini hii????....
 
Mkuu nahisi hao watu walikuwa hawajaingia payroll au ndo wanaoitwa wa ajira batili....maana ninalojua kama umeshaingia payroll na ajira yako imefata utaratibu unaotakiwa sio rahisi kufutwa...
Hebu tujue sababu na isiwe tu kulalamika maana sio rahisi tu bila saabu wakaambiwa warudi nyumbani na wao wakakaa kimya...
Mimi nina rafiki yangu yeye karipoti kazini na kuingizwa payroll mwezi June na hajaambiwa arudi nyumbani
 
Acha uongo wanasema mauzo ya hisa yamezidi kiwango kilichokadiriwa hivyo excess zitsrudishwa. Kuna sheria zinawabana
 
Mkuu wanarudisha za watu walio nunua hizo hisa za company kupitia DSA
Mm nimuanga wa hilo
 
Makampuni yaliyosajiliwa na DSE huuza hisa pale yanapohitaji kufanya hivyo,ama wamiliki wa hisa za kampuni flan labda TCC,TBL,TOL,Twiga Cement n.k...huuza kiasi flan cha hisa zao kwa sababu mbalimbali,DSE ni kama bridge agent wa wauzaji na wanunuzi.Wewe uneamua kuuza unazitupia DSE,wao wanauza kwa mwingine kwa bei iliyoko sokoni siku husika.Wewe utapata mpunga wako bila kujali nani kanunua,na mnunuzi hahitaji hata kujua zimetoka kwa nani.Mwisho wa siku ni mabadiliko ya umiliki tu wa hisa husika ktk kampuni husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…