Hisa za CRDB zimeanza kupanda bei kama mwaka jana (2020)

youngin

Member
Jan 31, 2020
13
45
Habari wana JF

@ Soko la hisa, UTT AMIS na Hatifungani
CRDB Bank PLC ni kampuni mojawapo iliyoorodheshwa hisa zake katika soko la hisa la DSE.

Hisa za CRDB zimekuwa zikifanya vizuri katika soko la hisa la DSE kwa urahisi wa kuuza au kununua, mabadiliko ya bei na kutoa gawio wa wanahisa wake, kama mtu utaweza kufanya uchambuzi mzuri utaweza kunufaika katika hisa za CRDB.

Mwezi January 2020, bei ya hisa moja ya CRDB ilifika hadi Tsh 95, lakini bei za hisa zikapanda hadi kufika Tsh 205, ikiwa ni ongezeko kubwa ndani muda mfupi. kuna watu walinunua kwa tsh 95 na wakaja kuuza kwa Tsh 205. ndani ya mwaka 2020 bei zilikua zinashuka na kupanda.

Tarehe 30/12/2020, bei ya hisa moja ilikua Tsh 195, kufika tarehe 8 january 2021, bei za hisa zikapanda na kufika 205, na inaonesha itaendelea kupanda zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom