Dira ya Maendeleo 2025-2050 inasema Elimu na ujuzi kwa Maendeleo ya Taifa na katika hilo Waziri Mkuu aliyepita alishauri na kusistiza sana watu waende VETA wakachukue ujuzi mbalimbali.
Katika hao walioitikia huo ushauri kuna wengine wamechukua driving kwa malengo, cha ajabu ni kwamba Vyeti vyao ambavyo vinawatambulisha kwamba wamehudhuria na kufuzu mafunzo ya awali ya udereva katika chuo kinachotambulika na Serikali hatimaye waweze kuvitumia kukata leseni wanacheleweshewa.
VETA Tanga kuna Intake kama 5 zote zinasubiria Vyeti, Waalimu wenyewe hawajui vinatoka lini, wao wanakwambia kazi yao ni kufundisha tu kama unataka maelezo zaidi onana na uongozi wa juu uulize.
Sasa naomba kuiuliza VETA Makao Makuu ni nini kinasababisha ucheleweshaji huu wa vyeti ukizingatia kwamba ili uruhusiwe kukata leseni ni lazima uwe na leseni hai ya awali ya kujifunzia ambayo nayo ina expire baada ya miezi 3.
Sababu Walimu muda mwingine wanakwambia changamoto haziko chuoni bali ziko VETA Makao Makuu kwamba anayehitajika kuvi-sign, hivyo vyeti ni mtu mmoja ambaye naye ana majukumu mengi. Kwa hivyo ili kurahisha utendaji kazi mimi naomba utaratibu urejeshwe upya vyeti viwe vinapatikana kwa urahisi eneo husika. Ila tu uwekwe mfumo mpya wa kuzuia kugushi.