Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,663
842
Heshima sana wakuu,

Tumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kutupatia uhai mpaka sasa tunapoelekea kuukamilisha mwaka 2021.

Najua kwamba wapo wengi walitamani kuanza ujenzi wa nyumba zao na ni ukweli usiopingika kwamba baadhi yao wameweza kuanza ujenzi, wapo walioishia katikati, wengine wamemaliza na huku wengine wakiwa hawajaanza kabisa.

Vilevile mwaka huu ume-trend zidi kwenye sekta ya ujenzi hasa kutokana na ukweli kwamba bei ya vifaa vya ujenzi mfano cement na bati ilipanda maradufu.

Kutokana na hayo naomba tupeane uzoefu kwa wale wote walioanza ujenzi wa nyumba zao mwaka 2021 ulifanikiwa vipi kuanza ujenzi na ni kwa namna gani ulipambana mpaka kufikia hapo.

Itapendeza zaidi kama utaweka specification za nyumba yako mfano vyumba viwili na sebule na gharama yake mfano milioni 30.

Mchanganuo huo utachagiza ari na morali ya wanabodi lakini pia utatuongezea mwanga na kutupa funzo kubwa la kusonga mbele na kutokukata tamaa kama sio kuahirisha ahirisha ujenzi wa makazi yetu tarajiwa.

Kwa heshima yenu nawasilisha
 
1 master room, 2 bed rooms, Kitchen, dining, sebule, public toilet! Location mbezi dsm nmeanza oktoba 2021 hadi hapo 10m imekata.
IMG_0201.jpg
 
Heshima sana wakuu,

Tumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kutupatia uhai mpaka sasa tunapoelekea kuukamilisha mwaka 2021. Najua kwamba wapo wengi walitamani.

kuanza ujenzi wa nyumba zao na ni ukweli usiopingika kwamba baadhi yao wameweza kuanza ujenzi, wapo walioishia katikati, wengine wamemaliza na huku wengine wakiwa hawajaanza kabisa.

Vilevile mwaka huu ume-trend zidi kwenye sekta ya ujenzi hasa kutokana na ukweli kwamba bei ya vifaa vya ujenzi mfano cement na bati ilipanda maradufu.

Kutokana na hayo naomba tupeane uzoefu kwa wale wote walioanza ujnzi wa nyumba zao mwaka 2021 ulifanikiwa vipi kuanza ujenzi na ni kwa namna.

gani ulipambana mpaka kufikia hapo.

Itapendeza zaidi kama utaweka specification za nyumba yako mfano vyumba viwili na sebule na gharama yake mfano milioni 30.

kwani mchanganuo huo utachagiza ari na morali ya wanabodi lakini pia utatuongezea mwanga na kutupa funzo kubwa la kusonga mbele na kutokukata tamaa.

kama sio kuahirisha ahirisha ujenzi wa makazi yetu tarajiwa.

Kwa heshima yenu nawasilisha
Asante sana kwa uzi huu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom