Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

images
382_iptl.jpg

  • Mke wa kigogo Ikulu atajwa
  • Kampuni ya uwakili nayo imo
  • Takukuru yaingia kazini
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu. Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).

“Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu kitakapokamilika,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa watu. Raia Mwema linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi.

Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.

Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo ambao gazeti hili limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh. Katika mojawapo ya miamala katika akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).

Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.

Gazeti hili limefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia. Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa PAP hayupo nchini kwa sasa.

“Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu. “Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka,” alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.

Malipo hayo yote yalifanyika katika kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014. Ni katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.

Ni katika siku hii ambapo ripoti za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha. “Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa,” ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.

Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.

Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika akaunti hiyo.

Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda. Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba “ watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi”.

Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.

Chanzo: Raia Mwema
Sijanufaika sana na taarifa yako, weka mambo hadharani, kama huna hakika subiri, ukipakua chakula kibichi hakitalika, kama unadhani ukimtaja mtu wakati huna uhakika utapata matatizo, bora ukae kimya na kusubiri. Tunataka mwandishi anayejiamini na kusema Chenge alipewa bilioni moja la milioni mia sita na ukweli ukawa ndiyo huo. Una uhakika leta majina, huna uhakika kaa kimya, zama za uwazi na ukweli.
 
Pole naona ulilala usingizi wakati nilishaleta mada iliyomtaja mhusika mada kama ifuatavyo: Mke wa Prosper Mbena (wa Ikulu) Alichukua TZS 2 Billion za ESCROW

Tarifa kwamba mke wa kigogo mmoja wa Ikulu alichukua Tzs 2 billion za ESCROW, si vizuri kuzungukazunguka, mhusika ni mke wa Prosper Mbena ambaye alichukua pesa hizo bank ya Stanbic. Chombo mojawapo kilishamhoji huyu mama mke wa Prosper.

Prosper Mbena ajitokeze kutetea au abishe kama mkewe hakuchukua pesa hizo.

Hapa ni JF where we dare to talk openly.

Kwenu wadau.

An escrow is:

  • a contractual arrangement in which a third party receives and disburses money or documents for the primary transacting parties, with the disbursement dependent on conditions agreed to by the transacting parties, or
  • an account established by a broker for holding funds on behalf of the broker's principal or some other person until the consummation or termination of a transaction; or,
  • a trust account held in the borrower's name to pay obligations such as property taxes and insurance premiums.

The word derives from the Old French word escroue, meaning a scrap of paper or a scroll of parchment; this indicated the deed that a third party held until a transaction was completed.

KWANINI ISSUE YA ESCROW INA TISHA????
Wakati akichangia ripoti ya PAC
Tundu lissue alitoa pendekezo kuwa majina ya watu waliochota pesa PAP kupitia StanBic Benk ni pamoja na Shabani Rajabu Gurumo ambaye ni ndugu na JK harafu ni State Controller.
Hi indo sababu pekee ambayo inampa Kiburi Maswi,Werema, na Muhongo kwa Kuwa wanajua hata State Controller amekula
Spika Anna makinda amekiri Bungeni kuwa Suala la Escrow limeleta usumbufu ambao haijawahi kutokea tangia uhuru!
Hadi naandika hapa Bunge bado halijapata ufumbuzi na huu ni ushahidi kuwa dola nayo imepasuka.
Pamoja na Tundu Lissu kusemtaja Shabani Rajabu Gurumo kuwa amekula escrow Shs800,000,000. Spika hamkumtaka alete Ushahidi lakin Bi Mshana aliposema Mbowe amechukua fedha za escrow Kenya Zungu alimtaka alete Ushahidi.
Hapa ndo tunapata Ushahidi kuwa Maafisa wa Ikulu, wamekula escrow nan do Maana kuna mizengwe ktk suala hili.

Ikulu yamtetea Prosper Mbena

VYOMBO vya habari nchini vimeaswa kuripoti matukio yaliyofanyiwa uchunguzi wa kina na yenye kufuata maadili na taaluma ya habari, badala ya kufanya kazi kwa kuongozwa na ushabiki vinapotekeleza majukumu yake.

Hayo yameelezwa katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika kwa Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, Prosper Mbena katika kumpa mwongozo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ili auruhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo katika BoT.

Taarifa hiyo inasema baadhi ya vyombo vya habari (siyo HabariLeo) vimemhusisha Mbena kuingilia mchakato wa uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti hiyo iliyoibua hoja nzito nchini, kiasi cha Bunge kuingilia kati na kutaka baadhi ya mawaziri na watendaji serikalini wawajibike kwa kile kinachodaiwa kuchota fedha za umma, jambo ambalo bado halijathibitishwa rasmi. "Huu ni uongo na uzushi.

Ni jaribio jingine la kutia chumvi katika jambo ambalo limetawaliwa kwa kiasi kikubwa na mihemko ya aina yake.

Gavana Ndulu mwenyewe anathibitisha kuwa hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Katibu wa Rais kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa baada ya kutokea kwa mgogoro wa kimaslahi baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Tanesco.

Chanzo:Habarileo

Nimekusaidia kuonyesha swali lako lilishajibiwa kwa mada hiyo hapo juu, nini tatizo mdau?
 
magazeti ya bongo yakishaifulia yanakuwa km bongo fleva, na bongo movies,watakuja na vipande vya heading ili kuuza kwa jina la Investigative Journalism.
 
Hi ni nithamu ya uoga umetaja mengine ila kumtaja mke wa kigogo ni kupisha upelelezi kwani wengine hawapelelezwi
 
Mbowe na Lowassa tunataka majina ya waliochota pesa kupitia Standbic Bank issue ya Escorw-hapo tarehe 24/10/2015 jangwani!

Haiwezekani tumechoka kudanganywa!

Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi,
kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.

CC Tumaini Makene aione Lowassa
 
Last edited by a moderator:
Magufuli hebu tutajie japo mmoja ili tuone kama kweli una dhamira ya dhati.
 
Double Standard, Roho Mbaya, Kuabudiana, Uzuzu, Ukatili Na Misamaha Koko
 
Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC. 😭 😭 😭
 
images
382_iptl.jpg

  • Mke wa kigogo Ikulu atajwa
  • Kampuni ya uwakili nayo imo
  • Takukuru yaingia kazini
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu. Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).

"Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu kitakapokamilika," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa watu. Raia Mwema linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi.

Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.

Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo ambao gazeti hili limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh. Katika mojawapo ya miamala katika akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).

Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.

Gazeti hili limefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia. Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa PAP hayupo nchini kwa sasa.

"Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu. "Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka," alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.

Malipo hayo yote yalifanyika katika kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014. Ni katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.

Ni katika siku hii ambapo ripoti za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha. "Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.

Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.

Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika akaunti hiyo.

Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda. Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba " watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi".

Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.

Chanzo: Raia Mwema
Mh. Mbowe wewe ni Mzalendo halisi..una uchungu mno na mali za nchi hii....ala kumbe majizi bado yanadunda mtaani hadi wa leo!! Hayakamatiki.
 
Back
Top Bottom