"bongomuvi" bado inaendelea.
Tatizo si magezeti ya kibongo, ila tatizo ni mfumo wa kulindana na katiba ya sasa inayolinda watawala wasinyoshewe kidolge kwa lolote, Mtajwa mmojawapo kama ni mke wa Kigogo wa Juu pale Ikulu ujue analindwa na katiba ya sasa hivyo vigumu kwa mazingira ya kibongo kumwanika hadharani. Ingwa jina laeleweka maana vigogo wa Juu wanaoishi Ikulu si idadi ya kuhesabu bali ni familia moja, vinginevyo wengingine wanaingia kikazi na kutoka si makazi yao na wengine ni watumishi tu.
Thats the bottom line.Mi naona bora wenye acess ya kuiba waendelee kuiba,kwa maana watafichwa fichwa kuanzia kwenye vyombo vya usalama mpaka media
Hawakuwa na ulazima wa kuandika hiyo habari kama bado TAKUKURU wanafanya kazi yao...Nilitegemea waliposema majina haya hapa,wasingesita kuyataja. ...salima. ..salama nk. ...
Hili gazeti nalo ni umbea na májuñgu,majina wapi?Sasa mbona hakuna majina?
(Ila hata tukiwajua sidhani kama kutabadilisha mambo)
Ukimya wa Ikulu ambao Katibu Mkuu alivyokingia kifua sakata hilo kuna dalili za Ikulu kuhusika. Umeona waliokaribu na Ikulu walivyonywea/
Si utaje majina yote kama unayajua?
Mke wa kigogo hana jina?
Wapi majina ya mawaziri nk?
Hii sredi ishakuwepo hapa na zaidi ni hewa tu haina lolote...
Mie nadhani gazeti liko sawa kabisa. Gazeti la uchunguzi haliandiki habari zake straight kwani zingine zinaweza kukiuka maadili ya kiuandishi. Hapa tunafahamishwa kuwa wapo wazito wanahusika na wajibu wa kuwataja moja kwa moja ni wa vyombo vya kisheria vyenye uwezo wa kuwashtaki mahakamani.
Hata hivyo habari hiyo inatosha kujulisha wananchi kuwa Ikulu ni Pango la wanyang'anyi na wahusika wameshindwa kujisafisha.
Soma habari uielewe, kwamba ili kutoharibu upelelezi unaoendelea na TAKUKURU majina yamehifadhiwa. Lakini kuambiwa mke wa kigogo wa juu pale Ikulu aliondoka na gunia la pesa nini zaidi unataka? Kama ni Darisalama? Salmina? Salamania? Sadakiasa? Au Marejesho?
Hawakuwa na ulazima wa kuandika hiyo habari kama bado TAKUKURU wanafanya kazi yao...Nilitegemea waliposema majina haya hapa,wasingesita kuyataja. ...salima. ..salama nk. ...