Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
images

  • Mke wa kigogo Ikulu atajwa
  • Kampuni ya uwakili nayo imo
  • Takukuru yaingia kazini
MAJINA ya baadhi ya watu walionufaika na fedha za akaunti ya Escrow zilizowekwa katika akaunti ya Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam yameanza kutajwa, Raia Mwema linafahamu. Miongoni mwa majina ambayo vyanzo vya gazeti hili vimethibitisha kwamba yapo ni lile la mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye anaelezwa kuchukua kiasi cha dola za Marekani milioni tatu (Sh. bilioni tano).

"Tayari tunalo jina la mwanamke mmoja ambaye amefahamika kama mke wa mmoja wa watu wenye vyeo vikubwa Ikulu. Kwa sababu bado mapema kukupa jina kamili, vumilia kidogo hadi kila kitu kitakapokamilika," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kinachoshiriki kwenye uchunguzi wa suala la namna fedha za akaunti ya Escrow zilivyolipwa kwa watu. Raia Mwema linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi.

Wakati majina ya baadhi ya mawaziri, wanasiasa, majaji na viongozi wa dini yakionekana kulipwa fedha za mgao kutoka katika akaunti moja ya Benki ya Mkombozi, kumekuwa na kitendawili kuhusu ni akina nani hasa walilipwa fedha zilizokuwapo katika Benki ya Stanbic.

Wafaidikaji wengine wa akaunti hiyo ambao gazeti hili limefanikiwa kuwapata kwa sasa ni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajiv Bharat Bhesania, anayetajwa kuwa mojawapo wa wasaidizi muhimu wa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Seth Singh. Katika mojawapo ya miamala katika akaunti ya Stanbic iliyofunguliwa na PAP ambayo inaonekana katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Bhesania anaonekana kuchukua kiasi cha dola milioni moja (shilingi bilioni 1.6).

Mtu mwingine ambaye inaonyesha amefaidi fedha za akaunti ya PAP ni Mwanasheria wa PAP, Joseph Makandege, ambaye kampuni yake ya sheria ya Bulwark Associates imeonekana kupata malipo yakiwamo ya zaidi ya shilingi milioni 500 kwa nyakati tofauti.

Gazeti hili limefanya mawasiliano na mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa IPTL aliyedai kwamba Rajiv pengine ndiye mtu anayefahamu vizuri zaidi mienendo na biashara nyingi zaidi za Sethi na kama Serikali inataka taarifa za mfanyabiashara huyo mtata; basi inapo pa kuanzia. Ingawa PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu, Raia Mwema limeambiwa kuwa mmiliki huyo wa PAP hayupo nchini kwa sasa.

"Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu. "Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka," alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.

Malipo hayo yote yalifanyika katika kupitia katika akaunti namba 912 0000 12 52 94 ambayo ilifunguliwa tarehe 28 Novemba mwaka 2013 na kufungwa tarehe 14 Septemba 2014. Ni katika benki hii ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.

Ni katika siku hii ambapo ripoti za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha. "Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.

Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.

Habari za mke wa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Ikulu kuhusishwa na uchotaji wa fedha za Escrow inakuja katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akidai bungeni kwamba ofisi hiyo ya juu nchini ina mkono katika utolewaji wa fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati akizungumza bungeni, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alimtaja Prosper Mbena ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), kuwa ndiye aliyeandika barua ya kuruhusu fedha zilizokuwa zimehifadhiwa zitolewe katika akaunti hiyo.

Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda. Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba " watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi".

Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.

Chanzo: Raia Mwema
 
Sasa mbona hakuna majina?

(Ila hata tukiwajua sidhani kama kutabadilisha mambo)

  1. mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu
  2. Rajiv Bharat Bhesania,
  3. Joseph Makandege,

Unataka majina gani wakati hayo yametajwa, unataka ulishwe kila kitu kama mtoto mdogo?
 
Ngoja nipeleke mchango wangu wa buku 20 pale muhimbili atibiwe mamake na mshikaji wangu anaye umwa figo,
 
Si utaje majina yote kama unayajua?

Mke wa kigogo hana jina?

Wapi majina ya mawaziri nk?

Soma habari uielewe, kwamba ili kutoharibu upelelezi unaoendelea na TAKUKURU majina yamehifadhiwa. Lakini kuambiwa mke wa kigogo wa juu pale Ikulu aliondoka na gunia la pesa nini zaidi unataka? Kama ni Darisalama? Salmina? Salamania? Sadakiasa? Au Marejesho?
 
  1. mke wa mmoja wa vigogo wa ngazi za juu Ikulu
  2. Rajiv Bharat Bhesania,
  3. Joseph Makandege,

Unataka majina gani wakati hayo yametajwa, unataka ulishwe kila kitu kama mtoto mdogo?

Hao ndio wamechukua bilioni sabini??!!
Unaleta habari kama ya udaku hakafu unataka kuwaka!!!??

Ongeza maneno "baadhi ya" kwenye heading yako utaeleweka!!!!
 
Candid Scope, nyie wandishi msijifanye mnajua upelelezi mnadakadaka maneno ya vijiweni tu
 
Last edited by a moderator:
Soma habari uielewe, kwamba ili kutoharibu upelelezi unaoendelea na TAKUKURU majina yamehifadhiwa. Lakini kuambiwa mke wa kigogo wa juu pale Ikulu aliondoka na gunia la pesa nini zaidi unataka? Kama ni Darisalama? Salmina? Salamania? Sadakiasa? Au Marejesho?

Hawakuwa na ulazima wa kuandika hiyo habari kama bado TAKUKURU wanafanya kazi yao...Nilitegemea waliposema majina haya hapa,wasingesita kuyataja. ...salima. ..salama nk. ...
 
Magazeti ya bongo huwa yananishangaza sana!.

Heading kubwaaa lakini contents zero.

Heading inasema, Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Halafu kwa mbwembwe wanaandika,
Raia Mwema linahifadhi jina la mwanamama huyo pamoja na mumewe kwa sasa kwa vile kuwataja majina kunaweza kuingilia upelelezi

Halafu wanatutajia wafanyakazi wa IPTL ili kutuamisha kama wanamfahamu huyo kigogo wa Ikulu kitu ambacho kila mwenye kufahamu sakata hili anafahamu kuwa pesa zilitolewa ili walipwe IPTL.

Wanatufanya kama sisi ni wajinga wakati kama kuharibu upelelezi kama wanavyotaka kutuaminisha watakuwa wameishaharibu baada ya kuwataja wafanyakazi wa IPTL kama wamepokea hizo pesa kutokea Stanbic.

Magazeti kama haya huwezi kutofautisha na magazeti ya Udaku.

Wanauza magazeti kwa kutumia Heading.

Kwa mtaji huu...
 
Hao ndio wamechukua bilioni sabini??!!
Unaleta habari kama ya udaku hakafu unataka kuwaka!!!??

Ongeza maneno "baadhi ya" kwenye heading yako utaeleweka!!!!

Bora umemuambia. .....Uandishi wa style ya kina Shigongo. ...
 
nyie wandishi msijifanye mnajua upelelezi mnadakadaka maneno ya vijiweni tu

Ukimya wa Ikulu ambao Katibu Mkuu alivyokingia kifua sakata hilo kuna dalili za Ikulu kuhusika. Umeona waliokaribu na Ikulu walivyonywea/
 
Magazeti ya bongo huwa yananishangaza sana!.

Heading kubwaaa lakini contents zero.

Heading inasema, Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Halafu kwa mbwembwe wanaandika,

Halafu wanatutajia wafanyakazi wa IPTL ili kutuamisha kama wanamfahamu huyo kigogo wa Ikulu kitu ambacho kila mwenye kufahamu sakata hili anafahamu kuwa pesa zilitolewa ili walipwe IPTL.

Wanatufanya kama sisi ni wajinga wakati kama kuharibu upelelezi kama wanavyotaka kutuaminisha watakuwa wameishaharibu baada ya kuwataja wafanyakazi wa IPTL kama wamepokea hizo pesa kutokea Stanbic.

Magazeti kama haya huwezi kutofautisha na magazeti ya Udaku.

Kwa mtaji huu...

Tatizo si magezeti ya kibongo, ila tatizo ni mfumo wa kulindana na katiba ya sasa inayolinda watawala wasinyoshewe kidolge kwa lolote, Mtajwa mmojawapo kama ni mke wa Kigogo wa Juu pale Ikulu ujue analindwa na katiba ya sasa hivyo vigumu kwa mazingira ya kibongo kumwanika hadharani. Ingwa jina laeleweka maana vigogo wa Juu wanaoishi Ikulu si idadi ya kuhesabu bali ni familia moja, vinginevyo wengingine wanaingia kikazi na kutoka si makazi yao na wengine ni watumishi tu.
 
Mkuu,
Wewe unayeifahamu Katiba ya nchi. Hebu nitajie kifungu cha kwenye Katiba kinachomlinda huyo kigogo wa juu pale Ikulu.

Kwa hiyo Raia Mwema inamlinda huyo kigogo wa juu pale Ikulu?

Tuacheni kufanya utani kwenye masuala ambayo ni serious?
 
Back
Top Bottom