Waliobanwa katika ajali wafariki

Waliobanwa katika ajali wafariki

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Posts
16,511
Reaction score
11,911
Hii nchi ya ajabu sana,watu wamebanwa ndani ya ajali Iringa baada ya malori kugongana,zaidi ya masaa 8,hakuna huduma ya kuwanasua,jana walikua wanaongea na kuomba msaada,leo tunaambiwa wamefariki.Hata dripu wangewekewa hapo hapo kwenye ajali wakati wanasubiri kunyofolewa.TANROADS kazi kupima uzito tuu?kwa nini wasiwe na crane la kunyanyua magari kila baada ya umbali fulani?
 
wanajua kupokea rushwa na kuchukua hela tuu, mengine mtajijua wenyewe
 
Kwa wale mnaofuatilia taarifa ya habari, kuna vijana waliokuwa wakizungumza wakiwa wamebanwa na malori baada ya kupata ajali na kuomba msaada kupitia vyombo vya habari.

Majeruhi wawili waliobanwa katika lori la mizigo katika ajali iliyotokea eneo la Maseyu barabara ya Morogoro - Chalinze wamefariki Dunia baada ya kuchelewa kuokolewa kwa zaidi ya masaa 16 kutokana na kukosekana kwa vifaa vya uokoaji.

Jambo la kusikitisha, pamoja na kwamba wamekaa hai kwa muda mrefu lakini vyombo sahihi vya kuwakwamua kutokana na kubanwa na malori vimekosekana hadi wakafa wanaona.

Mungu isaidie Tanzania, watu wanakufa baada ya kuwa hai kwa zaidi masaa 10.

Swali la kujiuliza, vipi kama Lori hilo lingekuwa limembana waziri au mkuu wa mkoa akiwa ndani ya gari lake?.

Bila kuoneana aibu, hapo serikali mmefanya uzembe! R.I.P my fellow poor
Taarifa ya vifo vya watu wawili waliobanwa na roli kwa zaidi ya masaa 16 iliyotangazwa leo na ITV inasikitisha sanasana.

Jana ITV waliwaonyesha watanzania hao wakiwa wamebanwa na mizigo, huku wakiwa kwenye maumivu makali waliomba msaada kwa serikali yao sikivu ya CCM, cha kushangaza hakuna msaada wowote uliotolewa. Kamanda alijaribu bila mafanikio kuomba gari la kuinua mizigo winch.

Hivi serikali ilishindwa kutoa msaada wa haraka kwa kupeleka winch kwa zaidi ya masaa 16 au walifanya makusudi maana walionaswa kwenye tukio walikuwa walalahoi?

Hivi angekuwa kigogo amenaswa au fisadi papa kanaswa si wangepeleka winch kwa Helikopta? Watanzania umefika wakati wa kujiuliza,hivi serikali ya sasa ya CCM inajali usalama wa watanzania walalahoi?

Nini kifanyike ili watanzania wote tuwe na uhakika wa kupata msaada tunaouhitaji toka serikali sikivu ya CCM pale tunapokumbana na majanga?
 
Inasikitisha sana, na mpaka waandishi wa habari walifika kupiga picha wakiwa bado wako hai. Watanzania tumekosa serikali inayoweza kujali watu wake. Rest In Peace!
 
Ingekua yamemkuta mbunge,waziri asingeopolewa?sii ajabu hata RC,RPC hawakwenda jana ktk ajali ila wangesikia waziri mkuu yupo uharo ungewatoka
 
aiseee....pumbavu moja utalisikia tattizo chadema....pumzikeni kwa amani
 
Inauma sana kaka! Utaskia imesababishwa na Chadema,ngoja tusubiri.
 
Nchi imeoza,JK unda DISASTER RECOVERY AGENCY haraka sana,hatuwezi shuhudia kufa hovyo
 
Ohoo hii ni habari ya kuhuzunisha kabisa. Kina Kikwete vyombo vya usalama wametingwa na kutunga njama za kutokomeza wanaowakosoa!
 
Nchi za wenzetu Raia mmoja tu akifriki ni msiba wa Nchi nzima, na mataifa mengine yako radhi kutumia hata Bilioni 100 kuoko raia wao mmoja tu, huku hakuna anayejari kila mtu anaanali tumboaa famalia yake
 
Inauma na inasikitisha sana. Tanroad ni rushwa tu lakini kuokoa watu kwenye ajali huwa hawamo kabisa. Wana pesa sana na wanauwezo wa kununua crane za kutosha lakini ndo hivyo tena. Inauma sana.
 
Huwa nashangaa watu wanaofikiri au bado wanamatumaini na serikali ya magamba wewe madaktari wanasema watu wanakufa hatuna vifaa tiba serikali inakataa kama yenyewe inatibu wanaofikiri kunaserikali nawapa pole maana tukiwaambia tuandamane kuing'oa wanaogopa kufa sijui kufa kwa ajali za kutengenezwa na makusudi zamagamba au kufa hospitali kwa kukosa huduma ni tofauti na kufa katika maandamano ya ukombozi.
 
Taarifa ya vifo vya watu wawili waliobanwa na roli kwa zaidi ya masaa 16 iliyotangazwa leo na ITV inasikitisha sanasana.

Jana ITV waliwaonyesha watanzania hao wakiwa wamebanwa na mizigo, huku wakiwa kwenye maumivu makali waliomba msaada kwa serikali yao sikivu ya CCM, cha kushangaza hakuna msaada wowote uliotolewa. Kamanda alijaribu bila mafanikio kuomba gari la kuinua mizigo winch.

Hivi serikali ilishindwa kutoa msaada wa haraka kwa kupeleka winch kwa zaidi ya masaa 16 au walifanya makusudi maana walionaswa kwenye tukio walikuwa walalahoi?

Hivi angekuwa kigogo amenaswa au fisadi papa kanaswa si wangepeleka winch kwa Helikopta? Watanzania umefika wakati wa kujiuliza,hivi serikali ya sasa ya CCM inajali usalama wa watanzania walalahoi?

Nini kifanyike ili watanzania wote tuwe na uhakika wa kupata msaada tunaouhitaji toka serikali sikivu ya CCM pale tunapokumbana na majanga?
 
yaani katika mambo yalioniaribia siku ni taarifa ya habari ya ITV kuhusu majeruhi waliobanwa na lori.sijui hii ni serikali ya namna gani,watu wanakufa wanajiona kabisa kisa hakuna vyombo vya kuwaokoa!!! Mpaka saiv ile picha bado inanijia kichwani jinsi walivyokuwa kwenye mavyuma huku wakiomba msaada.pumzikeni kwa amani ndugu zangu!
 
unapolipia road licence siku hizi wanakata na fire and rescue fees sasa sijui huwa zinatumika kweli kwenye shughuli za uokoaji au zinatumika na wenye meno.
 
Hii nchi ya ajabu sana,watu wamebanwa ndani ya ajali iringa baada ya malori kugongana,zaidi ya masaa 8,hakuna huduma ya kuwanasua,jana walikua wanaongea na kuomba msaada,leo tunaambiwa wamefariki.Hata dripu wangewekewa hapo hapo kwenye ajali wakati wanasubiri kunyofolewa.tanroads kazi kupima uzito tuu?kwa nini wasiwe na crane la kunyanyua magari kila baada ya umbali fulani?
Imeniuma sana aisee maana jana niliwaona wakiongea kwenye tv leo hatunao,lkn ingekuwa mtu ,wenye title tungeona hata meli za kijeshi maseyu zikitoa msaada. RIP comrades
 
Serikali ya ccm ni kwa ajili ya vigogo,mafisadi tuu na sii walalahoi
 
Back
Top Bottom