Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 490
Kama mtu ulishindwa kuelewa maana ya neno NGUVU YA HOJA na HOJA YA NGUVU, Sasa nafikiri huu ndio muda wa kulijua hilo. Ukiangalia jinsi mawakala wa ccm wanavyotumia nguvu sana kulazimisha hoja zao pasipo uchambuzi wa kina, bali kwa kukalilishwa tu! Ni tofauti kabisa na jinsi hoja za timu ya walio wachache zinavyodadavuliwa na kumfanya hata hamnazo nini kinachozungumziwa. Kwa maana nyingine waliowengi kama mngekuwa na cha zaidi ilitakiwa kujipanga na kufanya mchanganuo wa kina kama wenzenu wachache ili kuuaminisha umm kuwa mnachotazamia kuonekana katika mfumo ujao kitakuwa tofauti na sintofahamu iliyopo sasa! Lakini kama mtabaki na lugha nyepesi kuwa matatizo yaliyopo kwenye muungano ni madogo yanayoweza kutatuliwa wakati yameshindikana kwa miaka 50, hiyo ni danganya toto.