Ndugu wanaJF,
Mimi nipo kwenye ndoa kwa miaka nane (8) sasa. Ndoa yangu inafuraha na amani sana ingawa hapo nyuma tumewahi kuwa na misukosuko sana hadi kushitakiana kwa wakwe zangu/zetu.
Sababu ya uzii huu ni kutaka kushare experience na kuona kama nyie wengine mmepitia niliyopitia. Nimewahi kukwaruzana na mke wangu mara zaidi ya 15 miaka nane iliyopita lakini mara zote ukweli katika moyo wangu sikuwahi kufanya aliyonituhumu nayo na alinipachika jina MALAYA MKUBWA. Ilifika mahali hata wakati wa usuluhishi alikua ananiita jina hilo. Roho yangu iliniuma sana kwa sababu makosa niliyofanya hajawahi kujua na sikuwahi kutukanwa nayo ila yale ambayo sijafanya natukanwa na kudhalilishwa nayo. Chanzo cha makosa yangu siku zote ni
Lakini katika hawa wote sijawahi kufanya nao ngono na ndio kitu kinaniuma, Je wanaume wenzangu na hata Kina dada ndoa zenu zimewahi kupitia kwenye wakati mgumu kama sasa???
Naombeni Majibu
Tumekubaliana na Mke wangu tubadilike na sasa ni saa ya MABADILIKO hatuna ugomvi tena

- wadada nafanya nao kazi akikuta nimempigia nje ya muda wa kazi kosa naitwa MALAYA,
- akikuta message za wateja wangu wakiuliza kitu ni kosa naitwa MALAYA.
- tukienda kanisani nikikutana na mdada tunafahamiana siku nyingi nimsalimia naambiwa MALAYA,
- Tukitoka outing nikimwangalia mdada mrembo mara mbili mbili naitwa MALAYA