Walio Oa tu: Je, uliwahi kutuhumiwa umecheat na mkeo/mmeo?

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,065
5,393
Ndugu wanaJF,

Mimi nipo kwenye ndoa kwa miaka nane (8) sasa. Ndoa yangu inafuraha na amani sana ingawa hapo nyuma tumewahi kuwa na misukosuko sana hadi kushitakiana kwa wakwe zangu/zetu.

Sababu ya uzii huu ni kutaka kushare experience na kuona kama nyie wengine mmepitia niliyopitia. Nimewahi kukwaruzana na mke wangu mara zaidi ya 15 miaka nane iliyopita lakini mara zote ukweli katika moyo wangu sikuwahi kufanya aliyonituhumu nayo na alinipachika jina MALAYA MKUBWA. Ilifika mahali hata wakati wa usuluhishi alikua ananiita jina hilo. Roho yangu iliniuma sana kwa sababu makosa niliyofanya hajawahi kujua na sikuwahi kutukanwa nayo ila yale ambayo sijafanya natukanwa na kudhalilishwa nayo. Chanzo cha makosa yangu siku zote ni
  • wadada nafanya nao kazi akikuta nimempigia nje ya muda wa kazi kosa naitwa MALAYA,
  • akikuta message za wateja wangu wakiuliza kitu ni kosa naitwa MALAYA.
  • tukienda kanisani nikikutana na mdada tunafahamiana siku nyingi nimsalimia naambiwa MALAYA,
  • Tukitoka outing nikimwangalia mdada mrembo mara mbili mbili naitwa MALAYA

Lakini katika hawa wote sijawahi kufanya nao ngono na ndio kitu kinaniuma, Je wanaume wenzangu na hata Kina dada ndoa zenu zimewahi kupitia kwenye wakati mgumu kama sasa???

Naombeni Majibu

Tumekubaliana na Mke wangu tubadilike na sasa ni saa ya MABADILIKO hatuna ugomvi tena
 
Pole...... ndio mahaba bin wivu hayo...

Ila kama una mazoea yaliyopitiliza na hao wadada yapunguze.....

Vilevile mkeo anapaswa akusome na akujue wewe ni mwanaume wa aina gani kabla hajakurupuka na tuhuma......

Uwe na ndoa njema
 
Wenza wengine ni malimbukeni tu.

Marriage is not meant to be suffocating.
 
Sasa na wewe kwa nini Mpo outing na mkeo afu macho yote umeyaelekeza kwa mdada mnono mnono hadi unataka kudondosha glasi? Ilibidi akushtue na kelebu moja ili urudishe macho mezani teh
 
Sasa na wewe kwa nini Mpo outing na mkeo afu macho yote umeyaelekeza kwa mdada mnono mnono hadi unataka kudondosha glasi? Ilibidi akushtue na kelebu moja ili urudishe macho mezani teh

Umenikumbusha mbal sana namkumbuka x fiance alikuwa akiona mdada mthurii anajifanya yupo busy na cm! Ikafika wakati hadi namuonea hurumaa basi namwambia mkuu check toto vizuri bhnaa usizugee basi anachekacheka pale huku akizidi tupia mimacho yake!
 
Hahahahah nimekupenda bure. Unamuacha tu afurahishe macho
 
Sasa tutafanyaje mumy!! Jamaa alikuwa hana uhuruu na mm nilipenda awe huruu kwangu so nikampa uhuruu ila wakati mwingine huwa naumia kimoyomoyo ila nilikuwa simuonyeshi na yeye alikuwa ananishangaa umenikumbushaaa mbali sanaaa!
 
Daah kweli kuna muda lazima karoho kakuume. Ila naamini yalishapita hayo
 
Hata lowassa anatuhumiwa sana...kutuhumiwa ni jambo la kawaida saaana..any way mimi sijaoa ila my GF hajawahi nituhumu
 
Umenikumbusha mbal sana namkumbuka x fiance alikuwa akiona mdada mthurii anajifanya yupo busy na cm! Ikafika wakati hadi namuonea hurumaa basi namwambia mkuu check toto vizuri bhnaa usizugee basi anachekacheka pale huku akizidi tupia mimacho yake!
We dada wa ukweli sana..Vipi upo single now?
 
Hayo ni mambo ya kawaida haswa wakati mke wako ni mjamzito. Nimeshukiwa mara si moja hadi nikayowea. Lakini alipojifungua tu, yakaisha.
 
Back
Top Bottom