BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Nipo hapa Mlimani City ndani ya Jiji la Chalamila (Dar es Salaam), taarifa ikufikie kuwa vijana wa security yaani wale walinzi wanaovaa yale mashati maupe wameandaa maandamanonmadogo ya mgomo wa ndani ya jengo hilo, wanadai hawajalipwa mshahara, imekuwa kero, hiyo maandamano yasiyo rasmi yametokea jioni hii ya leo tarehe 6 Septemba 2023.
Jamani mabosi wa Mmlimani City tunajua mna mahela mengi tuhuko benki, hawa vijana wanafanya kazi kubwa, wanalinda vitu vingi vya thamani.
Mnashindwa kuwalipa mishahara kwa sababu gani? Tatizo Tanzania tumezoa kila kitu mpaka watu wafanye fujo kama hivi.
Hawa vijana wasaidiwe wasisumbue watu, hiyo security company inaitwa AS GUARD