Walimu Wilaya ya Moshi washangazwa ya kurudishwa kwa katibu wa CWT Godfrey Irumba mkoani Kilimanjaro

Nov 17, 2016
8
5
MKUU WA TAKUKURU (M)
MKOA WA KILIMANJARO
S.L.P 1951
Moshi-Kilimanjaro​

Imetokea taharuki mkoani Kilimanjaro baada ya kuonekana mtaani kwa aliyekuwa katibu wa chama cha walimu CWT Mwl G. Irumba.

Walimu wa Halmashauri ya Moshi tumeshtushwa sana na kuonekana kwa katibu huyu kuwa amerudishwa mkoani kilimanjaro kwenye nafasi yake kwani baada ya kugundulika kwa ubadhilifu huo alisimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wake bila kupelekwa Mahakamani;

Kinachotuhuzunisha sasa sisi walimu wa Halmashauri ya Moshi ni kusikia eti katibu huyu aliyetuibia fedha zetu za 15% zinazorudishwa matawini zipatazo million ishirini na tano25, 000,000 kurudishwa kazini, kwanza kwenye mkoa ule ule aliotuibia.

Hii ni dharau na fedhea kwa walimu kwa ujumla. Pia historia inaonesha katibu huyu alipokuwa Dodoma kama katibu alibainika kuiba fedha za walimu zipatazo million 11,000,000 ambazo zilikuwa ni fedha za walimu za kurejeshwa matawini ambazo ni asilimia 15 ya marejesho.

Sisi walimu tunamwomba Mh Mama Samia Suluhu Hasani atumie vyombo vyake Vya ulinzi viweze kufuatilia ubadhirifu huu aliotufanyia walimu wa Moshi na kama alithibitika pasiposhaka vyombo vifuatilie alirudishwaje kazini? Tumeibiwa sana na hatutakubali tena kuibiwa na huyu mwalimu.

WALIU VIJANA
HALMASHAURI YA MOSHI
 
Moshi siasa za kina rabiu saa nane nimehamia cwt

USSR
 
Back
Top Bottom