Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

Walimu amkeni,mda ndio huu.hicho chama kipya kilichoanzishwa kifungue website ambacho kitawafanya walimu wengi kukifahamu kikiwa na taarifa muhimu kama katiba na jinsi ya kujiunga.Pia iwarahisishie walimu jinsi ya kujitoa cwt na kujiunga na hicho chama kipya,ili kazi ianze mara moja kutetea haki za walimu.Mshikamano daima!
Aisee umezungumza hoja nzuri sana lakin kina Barbarosa na Pasco watakupinga tu
 
Hili nakuunga Mkono cwt kwa kweli hakina msaada kwa Mwalimu katika kudai haki zake zikiwemo kusoma. Eti viongozi wanasema kusoma sana kwa Mwalimu hakuna maana mwisho ni bachela tu zaidi ya hapo ni mapambo. Huwa najiuliza hela hii ya walimu nani anaudhibiti na taarifa yake mbona huwa haitoki. Nadhani huko kuna ubadhirifu wa kutosha. Mwalimu House iliyopo pale Ilala boma mapato yake yanamfaidishe mwanachama? Au in sifa tu kuwa jengo kama hilo! Ndo maana chama hakina nguvu ya kutetea maslahi ya walimu hakina pesa ya kuwahudumia wanachama endapo watakuwa mathalani mgomoni ambopo ni kinyume kabisa na nchini Kenya.
Sisi wakenya huwa tunafanya mambo kwa uweredi mkubwa unlike tanzanians
 
wagome tu mpaka hiyo cwt isukwe upya...ni ujinga kitu kile kile kinakutesa kila mwaka lakini huchukui hatua
Haitawezekana kusukwa upya kwakuwa viongozi wake wengi ni mapapeti wa ccm
 
Hiyo 2% inayokatwa kwenda chama cha walimu, mwalimu akistaafu harudishiwi?

Naona huko CWT kuna ulaji wa hali ya juu, CAG atembelee huko akaone maajabu ya wanaojiita wako kutetea waalimu
 
Hiyo 2% inayokatwa kwenda chama cha walimu, mwalimu akistaafu harudishiwi?

Naona huko CWT kuna ulaji wa hali ya juu, CAG atembelee huko akaone maajabu ya wanaojiita wako kutetea waalimu
hiyo hela angetosha walau kuanzisha benk yao wenyewe wakakopeshana kwa riba ya ndogo ya 3% .ile ghorofa pale ilala ya mwlim hause hela huwa inaendaga wapi ?
 
Matatizo ya walimu TZ yanasababishwa na walimu wenyenye! Hata viongozi wa chama cha walimu ni walimu. Hata watendaji katika wizara ya elimu ni walimu.Hivyo hayawezi tatuliwa na walimu wenyewe, wanahitaji kusaidiwa.

Muasisi wa taifa hili alikuwa mwalimu akashidwa kutatua matatizo/changamoto za walimu wanzake badala ya kuwainua akawadidimiza zaidi kwa kusema walimu sio kazi ya malipo bali ni wito! akisahau kila kazi inahitaji wito (internal call) hata jeshi, udaktari, n.k ni kazi za wito. Madhalani ikitokea unapata nafasi nyingine ya kazi nzuri zaidi ukakataa, ukachagua jeshi kazi hii kwako ni wito na sio kukosa kupewa mshahara mdogo, hivyo hivyo hata ualimu ikitokea ulikuwa na nafasi ya kuchagua kazi nyingine ukazikataa, ualimu utakuwa wito kwako haina uhusiano na kupewa mshahala kiduchu!

Hata rais na waziri mkuu wa sasa ni walimu lakini hawataweza kutatua matatizo ya walimu wenzao. Kimsingi walimu hawawezi kutatua matatizo yao hata kama miongoni wmao watatoka mawaziri na marais mpaka atoke mtu kutoka katika field nyingine anaweza kusimamia walimu wakatatua matatizo yao. Ikitokea miujiza rais wa chama cha walimu madhalani akatoka katika fani ya udaktari au mwanajeshi anaweza kutatua changamoto zao lakini sio mwalimu.

Mwalimu hasa wale wanaopanda kutoka shule za msingi mpaka kupata kacheo wilayani au wizarani, hawa ni sumu kwa maendeleo ya walimu wenzao.Hawa ndiyo wanaodidimiza walimu wanzao.
A good teacher in Tz must have brain partly dormant!
 
Nahitaji mwalimu wa KUHAMA kahama aende popote anapoamini atapata nafasi
nasema aende popote sababu mimi nlimeruhusiwa kutoka bukoba mjini, ila kahama afisa elimu anasema hana nafasi nitafute anayetaka tutoka kahama ili nipewe mimi nafasi yake
mawasiliano: 0713134926 au 0763061425
 
Kwanza naomba niwapongeze walimu kwa majitoleo yao ya dhati kabisa kulitumikia taifa letu wakiwa na mazingira magumu sana. Walimu wangu wote popote mlipo nchi nzima shikamoooni!

Sasa nakuja kwenye huu mjadala wa wazi ili tusaidiane kuonesha ni njia ipi itasaidia walimu kujikwamua. Walimu wanaidai serikali mabilioni kibao, lakini walimu hao hao wanakatwa mabilioni kibao kila mwezi kutoka kwenye mishahara yao.

Sasa swali langu ni kwa viongozi wa CWT kwa nini mnashindwa kuwalipa walimu madeni yao kwa kutumia mfuko wao then chama kikabaki kinafuatilia madai ya walimu punde wakilipwa pesa zinapelekwa kwenye chama? Hii inawafanya viongozi wa walimu kulala bila kuumiza kichwa huku wakijilimbikizia mali na wanamali kwelikweli!
 
kuanzishwe vyama vingi vya walimu walimu wachague chenye maslahi kwao,enzi zile kulikuwa na mifuko ya jamii miwili tu PPF na NSSF,sasa iko zaidi ya kumi,kuwe na chama cha walimu wa shule za msingi ,skondary,private,government etc na mwanachama aruhusiwe kuchagua mwenyewe chama kipi kinamfaa

Mkuu asante kwa kuchangia vizuri, niliwahi sikia kwamba walimu wameanzisha chama kipya cha maafisa elimu kimefikia wapi? Yaani walimu wenye shahada ya kwanza ya chuo kikuu.
 
Watu wanaifananisha CWT na:
1. Chama cha kufa na kuzikana. Ndiyo maana utasikia walimu hasa wa sekondari wakiulza kwani hii CWT itanisaidia nini nikipata tatizo!!?
2. Mifuko ya Hifadhi ya jamii. Walimu wengi wanafananisha mlengo na madhumuni ya CWT kama vile mifuko ya hifadhi ya jamii kma vile PPF, LPF na PSPF.
Walimu ifike wakati mwache malalamiko yasiyo ya. msingi. CWT ipo kisheria na si watu from no where wakaanza kukata mishahara yenu. Hata sisi madaktati tuna chama na tunachangia kiasi/ asilimia hizo hizo ambazo nanyi mnachngia. Kila mfanya kazi wa Serikali anachangia 2% ya basic salary yake kwa chama chake kma gharama ya uendeshaji. Sasa kwenu walimu kukatwa hiyo pesa imekuwa uchuro!! Mnakera hebu msijaze server acha tujadili issue za maana humu ndani.
ANGALIZO:
Hata CWT ivunjwe na kikaja chama kingine makato yapo pale pale, hii ni sheria iliyotungwa na bunge na si maamuzi ya CWT. Hutaki hama nchi kafundishe Rwanda.
 
ki ukwel waalim wanapata shida nyingi ila hili la makato aseee ni shida, m nitoe mfano, kuna mwalim amekuwa akikatwa mshahara wake na anaishi kigoma vijijini, halafu kunajengo pale bugurun ilala linamnufaishaje hyo mwalim? na hicho chama kinatetea nn?

m naona hvyo vyama ni onyonyaji tu, kama hakuna uccm humo ndan basi serikal inahusika, wahurumien waalim, au basi kungekuwa na sheria kuwa hyo pesa iwarudie waalim, ni nyingi mno,

ifike sehem watu hili nalo liwe jipu, JF members plz waokoen waalm kwa kupinga hiki chama ni dude linalonyonya nguvu za waalim, naomba uanachama uwe kwa hiari..
 
ki ukwel waalim wanapata shida nyingi ila hili la makato aseee ni shida, m nitoe mfano, kuna mwalim amekuwa akikatwa mshahara wake na anaishi kigoma vijijini, halafu kunajengo pale bugurun ilala linamnufaishaje hyo mwalim? na hicho chama kinatetea nn?

m naona hvyo vyama ni onyonyaji tu, kama hakuna uccm humo ndan basi serikal inahusika, wahurumien waalim, au basi kungekuwa na sheria kuwa hyo pesa iwarudie waalim, ni nyingi mno,

ifike sehem watu hili nalo liwe jipu, JF members plz waokoen waalm kwa kupinga hiki chama ni dude linalonyonya nguvu za waalim, naomba uanachama uwe kwa hiari..
Ndio hivyo mkuu walimu wamegeuzwa kituko
 
Back
Top Bottom