Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
Ok ni kwamba CWT kama kinavyojiita ni chama cha waalimu tukidhani ni cha kutetea haki za waalimu sio kweli maana ndio wanyonyaji wakuu wa waalimu.

Wamejining'iniza kwenye salary zetu kama mifuko mingine ya pension, bima ya afya,loan board ambapo hii mingine angalau tunajua ni jinsi gani tunafaidika nayo...kwa mfano tu pension PSPF wanakata 5% ya mshahara, na hii hela tunajua wazi ni mchango wa mafao ya uzeeni. Sasa hawa cwt wanakata 2% ya mshahara wa mwalimu. Kwa mfano mwl anayelipwa 720 000/= analipa cwt sh 14 320/=, mwalimu 940 000/= anakatwa cwt 16 400/= kwa hiyo unavyozidi kupanda nao wanapanda...

Japo ni sheria kwamba kila wafanyakazi wana chama cha kutetea haki zao, cwt walio watetezi wa waalimu hakina machungu na waalimu waliokuwa walalamikaji wa siku nyingi lakini matokeo yake ni wao walio kwenye chama wananufaika na kujitajirisha kwa kuwanyonya waalimu,tukumbuke kuwa kundi la waalimu ndilo lenye wafanyakazi wengi kuliko wote.

Kwa mfano tu mimi shuleni kwangu tupo waalimu 40 na tumeanza kazi miaka ya majuzi makato yetu ni kwenye elf 16 400*40= 656,000 hii ni makato ya mwezi mmoja.

Haiwezi kuingia akilini kwamba kila mwezi shuleni kwangu tunachangia hiyo hela kwa cwt ni vile tu wamepita juu kwa juu na hatuna amri juu ya hiyo hela..piga hesabu kwa mwaka, miaka n.k..

Au tufanye hesabu ya mtu mmoja japo ni ngumu maana mshahara unapanda kila mwaka na makato yao yanapanda pia. Lets take anayekatwa 25 kila mwezi..25 000×12=300 000 kwa mwaka mwalimu huyo mnyonge anaichangia laki 3.
300 000 × miaka 30 = 9 000 000.
Kwa hiyo mwalimu aliyefanya kazi miaka 30 anachangia 9m na zaidi kwa sabau mshahara unapanda maana kwa mfano mwl mwenye kulipwa 2.5m anakatwa elf50.
Sasa hawa ni watetezi wa wanyonge kweli?

Wakati wa uchaguzi wa uongozi wa cwt mtu anadiriki kukopa 20m ya kufanyia michongo ya kupata uongozi maana anajua akipata hiyo position atailipa hela na kuanza kula hela kiulaini ya waalimu wanyonge.

Makato ya cwt yamekuwa machungu sana kwa waalimu na ndio maana hatuitaki kwani hawana msaada wowote kwa waalimu zaidi ya kula jasho letu. NI BORA WANGEKATA FIXED RATE ya hela kwa mfano elfu5 tu kwa kila mwalimu kila mwezi kama raisi wetu atashindwa kutuondolea hili jipu kwenye salary slip yetu....

NIMESAHAU KITU...MWALIMU AKISTAAFU HAWA CWT WANAMZAWADIA MWALIMU MABATI 20 YALE YENYE THAMANI YA SH ELF17 NA KITAMBAA CHA SURUALI PINDI ANAPOSTAAFU BAADA YA KUMNYONYA MAMILIONI YA KUTOSHA
 
Cwt ni genge la wahuni wanaokula kiulaini kupitia shida za walimu,mara 100 wangekua wanatatua shida za walimu,cwt ndani ya mwaka mzma ndani ya wilaya 1 hutatua shida ya mwalimu 1 au wawl;wanatatua matatzo kwa sampling;hela wanayochota ni kubwa kulinganisha na huduma anayopata mwl toka kwao;walimu tupambane kuanzisha vyama vya kututetea viwe vingi,Inawezekana Tukishikama..
 
Nimeamua kuwatetea walimu manake imeonekana ni sector ilidharaulika kuliko hata udereva
 
kama ni jambo linalo wezekana walimu kadhaa watafute wataalamu wa sheria wapeleke malalamiko mahakamani. nadhani mahakama ndio sehemu pekee unapoweza pata haki yako, hivyo walimu waache kuwa wanyonge na kukubali kukandamizwa na kila mtu
 
Mshikamano ndio silaha;Mbona mbeya km cjakosea kuna chama kipya cha walimu;Tatzo pia serikali yetu na walaji wachache hukwamisha harakati za uundwaji wa vyama hv ili waendelee kupga hela;Kisheria mtu ana haki ya ku_join Union yyte,sio lazma Cwt;Problem walimu weng uchumi ni mbovu hvyo huongozwa na hofu juu ya kufungiwa mishahara yao au kufutwa kazi hvyo kupelekea kushndwa kutetea haki zao
 
kama ni jambo linalo wezekana walimu kadhaa watafute wataalamu wa sheria wapeleke malalamiko mahakamani. nadhani mahakama ndio sehemu pekee unapoweza pata haki yako, hivyo walimu waache kuwa wanyonge na kukubali kukandamizwa na kila mtu
Nakwambia hata madereva wanasikilizwa lakini sio walimu
 
kuanzishwe vyama vingi vya walimu walimu wachague chenye maslahi kwao,enzi zile kulikuwa na mifuko ya jamii miwili tu PPF na NSSF,sasa iko zaidi ya kumi,kuwe na chama cha walimu wa shule za msingi ,skondary,private,government etc na mwanachama aruhusiwe kuchagua mwenyewe chama kipi kinamfaa
 
Aisee hilo wazo lako limeenda shule mno,i hope walimu watalichukua kama lilivyo
kuanzishwe vyama vingi vya walimu walimu wachague chenye maslahi kwao,enzi zile kulikuwa na mifuko ya jamii miwili tu PPF na NSSF,sasa iko zaidi ya kumi,kuwe na chama cha walimu wa shule za msingi ,skondary,private,government etc na mwanachama aruhusiwe kuchagua mwenyewe chama kipi kinamfaa
 
Hapa yanahitajika maamuzi magumu kama alivyothubutu mh raisi Magufuli kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo raisi ajitose tu kuwaokoa waalimu kwenye hili jahazi la Cwt.... Cha ajabu viongozi wa cwt walikuwa waalimu.... sasa hivi wanakula maisha kwa anasa zote walizozikosa siku za huko nyuma
 
Kila mtumishi anacho chama chake cha wafanyakazi na kipo kisheria. Wanaweza kushusha kiwango cha malipo kama wana sababu hasa ukizingatia wao ni wengi. Kuhusu kufaidika, ukimpata alitefukuzwa kazi akatetewa akarudishwa kazini na kulipwa hawezi kukuelewa unakiponda chama chake. Nakubali viongozi kama kina Mgaya na Mkoba ni matatizo hawafai kuongoza wafanyakazi
 
nlitegemea mapambano makal baada ya walimu wenye digrii kuongezeka kuanzia miaka ya 2005 nikiamin kuwa watapambana kisom zaid lakin hamna lolote
 
kuendelea kuisupport cwt, ni kielelezo cha ujinga. Mzee wangu alianza kazi 1980,kastaafu kwa hiari amekaa miezi 7 pspf kabla hawajampa fedha zake na wala cwt hawakumsaidia lolote ambayo ameichangia maisha yake yote ya kazi. kwa pension bora Nssf.
 
Hapa yanahitajika maamuzi magumu kama alivyothubutu mh raisi Magufuli kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo raisi ajitose tu kuwaokoa waalimu kwenye hili jahazi la Cwt.... Cha ajabu viongozi wa cwt walikuwa waalimu.... sasa hivi wanakula maisha kwa anasa zote walizozikosa siku za huko nyuma
Hehehe wanafidia
 
kuendelea kuisupport cwt, ni kielelezo cha ujinga. Mzee wangu alianza kazi 1980,kastaafu kwa hiari amekaa miezi 7 pspf kabla hawajampa fedha zake na wala cwt hawakumsaidia lolote ambayo ameichangia maisha yake yote ya kazi. kwa pension bora Nssf.
Aisee pole sana kwa mzee hakika wewe mwanae uko responsible kusimama kwenye haki zake
 
Walimu amkeni,mda ndio huu.hicho chama kipya kilichoanzishwa kifungue website ambacho kitawafanya walimu wengi kukifahamu kikiwa na taarifa muhimu kama katiba na jinsi ya kujiunga.Pia iwarahisishie walimu jinsi ya kujitoa cwt na kujiunga na hicho chama kipya,ili kazi ianze mara moja kutetea haki za walimu.Mshikamano daima!
 
wagome tu mpaka hiyo cwt isukwe upya...ni ujinga kitu kile kile kinakutesa kila mwaka lakini huchukui hatua
 
Hili nakuunga Mkono cwt kwa kweli hakina msaada kwa Mwalimu katika kudai haki zake zikiwemo kusoma. Eti viongozi wanasema kusoma sana kwa Mwalimu hakuna maana mwisho ni bachela tu zaidi ya hapo ni mapambo. Huwa najiuliza hela hii ya walimu nani anaudhibiti na taarifa yake mbona huwa haitoki. Nadhani huko kuna ubadhirifu wa kutosha. Mwalimu House iliyopo pale Ilala boma mapato yake yanamfaidishe mwanachama? Au in sifa tu kuwa jengo kama hilo! Ndo maana chama hakina nguvu ya kutetea maslahi ya walimu hakina pesa ya kuwahudumia wanachama endapo watakuwa mathalani mgomoni ambopo ni kinyume kabisa na nchini Kenya.
 
Back
Top Bottom