Walimu walitumiwa kuandaa mgomo feki.

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Mimi ni mmoja wa watu wengi wanaopinga mgomo 'feki' wa walimu uliofanyika wiki hii.naupinga kwa sababu naamini walimu na serikali yetu ni maswahiba wa siku nyingi na hakuna ushahidi kuwa uswahiba wao uliingia matatani.

Mgomo huu wa walimu uliibuka ghafla hasa baada ya kushuhudia mgomo wa kweli kutoka kwa madaktari.
Mgomo wa walimu umeletwa ili kutuaminisha kuwa utekelezaji wa madai ya madaktari unaweza kuzalisha madai mengi kutoka sekta nyingine.

Juzi niliweka thread kuwa mkoba ambaye ni kiongozi wa CWT alisaini kitabu cha mahudhurio ili asionekane amegoma,bado naamini tukio hili ni la kweli mpaka hapo mkoba atakapolishtaki gazeti lilioandika habari hii.

Leo hii tumeshuhudia CWT ikiwasihi walimu kuendelea na kazi bila kujua hatima ya madai yao.
Yaani ni usanii mtupu.

Ombi langu kwa walimu

CWT ni chama cha kisanii na kamwe hakiwezi kutetea maslahi yenu.pia mnapotaka kudai maslahi yenu msipende kuweka mbele umuhimu wenu katika jamii na kuwafanya watu wengine hawana thamani.mgomo sio kitu cha kuiga au show ya kwasakwasa.

Msipende kutumiwa kwenye kuiba kura au kukwamisha juhudi za makundi mengine ya kijamii kama mlivyofanya.
 
najua walimu wote miliomo humu jamvini mtaumizwa na msimamo wangu lakini hii ni changamoto kwenu ili msirudie usanii/ufisadi huu na kamwe msikubali kutumiwa kwa maslahi ya wanasiasa.
 
walimu wanasema mgomo umefanikiwa kwa asilimia 95

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Walimu wameonyesha mfano mzuri kuheshimu amri ya mahakama. Wameifundsha jamii umuhimu wa kuheshimu mhimili huo muhimu wa dola.
 
Kwenye msafara wa Mambo, huwa Kenge hakosekani. Walimu kulipwa 200,000/= wewe waona inastahili? Je, ni fair ukilinganisha na watumishi wengine? Unafiki wa nini jamani? Hivi jiografia ya nchi yetu mnaifahamu lakini? Je wajua kuwa kuna walimu wanasafiri siku 2 kuufuata huo mshahara? Mungu atawalipa wanafiki na wazandiki woote wanaoshangilia Walimu kulipwa KIDUCHU, halafu wao wanamegewa likeki KUUBWA la utajiri wa nchi yetu.
 
Wakati walimu wamegoma wewe ulichukua hatua gani? Ungetoka barabarani mgomo ungekuwa KWELI. Ukalala kwako acha unafiki!
 
Kwenye msafara wa Mambo, huwa Kenge hakosekani. Walimu kulipwa 200,000/= wewe waona inastahili? Je, ni fair ukilinganisha na watu
mishi wengine? Unafiki wa nini jamani? Hivi jiografia ya nchi yetu mnaifahamu lakini? Je wajua kuwa kuna walimu wanasafiri siku 2 kuufuata huo mshahara? Mungu atawalipa wanafiki na wazandiki woote wanaoshangilia Walimu kulipwa KIDUCHU, halafu wao wanamegewa likeki KUUBWA la utajiri wa nchi yetu.
mngesubiri ya madaktar yaishe tungewaelewa-maana ingekuwa njia rahis kwa madai yenu-tumestuka kuna picha picha!
 
Plse waalimu wote hapa jamvini,achaneni na hao jamaa wanafki wanaopinga kile tulichokitenda tokea 30-2 mwezi huu,naomba tusibishane nao saana kiasi tukatokwa na povu kwa mdomo,Plse let Us show them'kwani wao ndio watakao ingia darasani kufundisha?lazima waisome namba tyme hii
 
Mimi ni mmoja wa watu wengi wanaopinga mgomo 'feki' wa walimu uliofanyika wiki hii.naupinga kwa sababu naamini walimu na serikali yetu ni maswahiba wa siku nyingi na hakuna ushahidi kuwa uswahiba wao uliingia matatani.

Mgomo huu wa walimu uliibuka ghafla hasa baada ya kushuhudia mgomo wa kweli kutoka kwa madaktari.
Mgomo wa walimu umeletwa ili kutuaminisha kuwa utekelezaji wa madai ya madaktari unaweza kuzalisha madai mengi kutoka sekta nyingine.

Juzi niliweka thread kuwa mkoba ambaye ni kiongozi wa CWT alisaini kitabu cha mahudhurio ili asionekane amegoma,bado naamini tukio hili ni la kweli mpaka hapo mkoba atakapolishtaki gazeti lilioandika habari hii.

Leo hii tumeshuhudia CWT ikiwasihi walimu kuendelea na kazi bila kujua hatima ya madai yao.
Yaani ni usanii mtupu.

Ombi langu kwa walimu

CWT ni chama cha kisanii na kamwe hakiwezi kutetea maslahi yenu.pia mnapotaka kudai maslahi yenu msipende kuweka mbele umuhimu wenu katika jamii na kuwafanya watu wengine hawana thamani.mgomo sio kitu cha kuiga au show ya kwasakwasa.

Msipende kutumiwa kwenye kuiba kura au kukwamisha juhudi za makundi mengine ya kijamii kama mlivyofanya.

Ungekuwa feki kama wanachodai hakipo. Je hujui mwalimu mmoja nanalipwa fedha pungufu ya posho ya mbunge ya siku kama mshahara wa mwezi? Yaani tuwahurumie.
 
Back
Top Bottom