Walimu waliogoma kutolipwa mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu waliogoma kutolipwa mishahara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dickson Ng'hily, Jul 31, 2012.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  WAKATI walimu wakianza mgomo wa kutoingia madarasani jana, serikali imesema
  kuwa walimu watakaobainika kujihusisha na mgomo huo hawatalipwa mishahara.


  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema hayo jana wakati akitoa tamko la serikali kuhusu mgomo huo kwa waandishi wa habari.
  Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, licha ya mwajiri kutowalipa mshahara walimu wote
  waliogoma watachukuliwa hatua kali huku wale wanaowatisha wenzao na
  kuwashirikisha wanafunzi kwenye mgomo, watawajibishwa


  SOURCE: Tanzania Daima

  My Take:
  Hivi waziri anadhani hilo la kutowalipa mshahara ndo litakuwa suluhisho! mshahara wenyewe hata sina hakika kama ndo huwa unamwezesha mwalimu kuishi..Me nadhani busara ingetumika badala ya kutumia ubabe ama kuonyeshana nguvu...Sasa nao (walimu) wakiamua kama ilivyotokea kwa madaktari itakuaje?
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  mimi mwalimu wa upe bora nifundishe maana hata vyeti sina.
   
 3. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  fedha wa ualimu ni sawa na kumdumaza mwl kuacha kufikiri na kujikuta maskini.wakifuta mshahara nichangamoto ya kufikiri upya.
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  wenyewe ndivyo wanavyoamini. Eti mshahara ndio unaowaweka walimu mjini.
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  fundisha tu, ila salio likiongezeka utawashukuru hawa wanaogombana na mwajiri wako. Njaa mbaya sana
   
 6. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mods wamekuokoa! nafyata mkia!
   
 7. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waziri anafikiria kwa kutumia masaburi.
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red ndipo walishajua kuwa tunaogopa kuchukuliwa hatu maana wengi huwa wanazilinganisha na scenario za Mabwepande lakini tukumbushane wakati wa mateso ya Dr. Ulimboka nasikia alitamka mwenyewe akasema "si mniue tu".
  Sijui itachukua muda gani watawala kutambua kuwa kuna watu hapa Tanzania tunapata mateso ya maisha ambayo ni makali kuzidi hizo hatua wanazotishia kuchukua.
   
 9. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ni kweli watu wanaogopa hatua kali kuchuliwa dhidi yao, hata hivyo kuna watu wachache ambao wako tayari kwa lolote na mimi nadhani hao ndo wanapashwa kusimama imara kwa ajili ya majority....Mtu mmoja huangaika kwa ajili ya wengine...Tukiogopa wote basi serikali itaendelea kutunyanyasa coz inajua kuwa ikitutishia basi tutafyata mkia na maisha yataendelea...
   
 10. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijatishika, sikanyagi shule hadi nimsikie kwa masikio yangu rais wa CWT akitangaza kuwa turudi shuleni tena baada ya kutangaza kuwa amefikia hatua gani na serikali, vinginevyo, LIWALO NA LIWE, najiandaa kwenda Bustanini, nitarejea jioni kwenye mtandao kujua ni kipi kilichojiri mjini....Mpanda kama kawa, tuko ngangari hadi kieleweke! Mkubwa hatishiwi nyau.
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Hii serikali ilikwenda likizo siku nyingi then ikasahau siku ya kurejea kazini! makinda kila siku anakomaa na mambo yaliyoko mahakamani yasijadiliwe, leo hili la mgomo Kawambwa kasema serikali imewasilisha submission yake mahakama ya kazi jana akaongeza kuwa uamuzi wa mahakama ya kazi utatolewa leo; sasa iweje tena aanze kutamka adhabu kwa walimu kabla ya hukumu ya mahakama?! au ndio mwendo mdundo wa serikali ya mabwepande Kawambwa anaujua hukumu itakuwaje!
  hili linatukumbusha kauli ya JK kuhusu mkasa wa dr. Ullimboka; kabla ya kamati ya kova/Pinda kuanza kazi na kutoa findings zake tukamsikia JK anasema "serikali hatuhusiki" hii nini hii!!
   
Loading...