Walimu watangaza mgomo nchi nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu watangaza mgomo nchi nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John W. Mlacha, Dec 2, 2011.

 1. J

  John W. Mlacha Verified User

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Walimu watangaza mgomo nchi nzima
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 01 December 2011 20:42 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana , kuhusu mgomo wa walimu nchi nzima utakaoanza mwezi Januari kama Serikali haitatimiza makubaliano yaliyofikiwa ya kuwalipa madai yao. Picha na Venance Nestory

  Raymond Kaminyoge
  CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia Januari mwakani ikiwa ni hatua ya kuishinikiza Serikali iwalipe walimu deni la malimbikizo ya stahili zao mbalimbali, linalofikia Sh49.6 bilioni.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kuwalipa walimu fedha hizo tangu Novemba mwaka huu. Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wandishi wa habari kuwa Serikali iliahidi kuwalipa walimu Novemba hadi Desemba mwaka huu ili kumaliza deni hilo.

  “Natangaza kuwa shule zitakapofunguliwa mwezi Januari 2012, sisi walimu tutaendelea kuwa likizo mpaka kero zetu zitakapotatuliwa,” alisema Mukoba. Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo na ikafikia uamuzi wa kuwalipa walimu katika kipindi cha miezi miwili ambayo ni Novemba na Desemba mwaka huu.

  “Kumbe Serikali haikuwa na nia ya kweli kutaka kutulipa, waliona tunaweza kugoma katika kipindi cha mitihani ya taifa wakatudanganya,” alisema. Alisema kwa kuwa Serikali haina nia ya dhati katika kulipa madai hayo, wameamua kufikia uamuzi wa kutoendelea kufundisha.

  Mukoba alisema wakati mishahara na posho za wabunge zikizidi kuongezeka, walimu wanashindwa kulipwa madai yao ya msingi. “Tunawaomba wazazi watuunge mkono katika mgomo huu ili watoto wenu wapate elimu sahihi,” alisema Mukoba. Kwa mujibu wa Mukoba, madai hayo yanayowahusu zaidi ya walimu 3,000 ni ya kuanzia mwaka 2008.

  Alisema kero nyingine inayowafanya walimu wagome ni waraka kandamizi uliotolewa na Serikali mwaka 2007 unaowashusha vyeo walimu wanaojiendeleza kielimu. “Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema. Mukoba alisema waraka huo umelenga kuwakatisha tamaa walimu ili wasijiendeleze kielimu.

  Aidha, Mukoba alisema walimu wanakaa kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo ingawa wanastahili kulingana na sifa zao. “Walimu tumekosa nini, kwa nini kilio chetu hakisikiki na Serikali? Iweje tunadanganywa kila siku? Sasa ni lazima tuchukue hatua,” alisema Mukoba. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawamba hakupatikana jana kuzungumzia tishio hilo la mgomo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana kabisa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  hawa mbayu wayu wameammka?
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Tabaka kubla linalonyonywa huku fisi wachache pale mjengoni dodoma wakijilipa mabilioni
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  Wabunge wamejiongezeantoka 70,000 hadi 200,000
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wangekuwa ni madaktari na manesi ningeamini lakini hawa no....
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  Kwa nini?
   
 7. n

  nyangasese Senior Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi wa chama cha walimu ni wanafiki wakubwa.Hamna uwezo kufanya maamuzi magumu.serikali hii legelege inayomlipa mbunge kwa siku sawa na mshahara wa mwalimu graduate wa mwezi1.kumbukeni kuwa hata kama hayo mabilioni yatalipwa bado ni kazi bure.mfano hapa mwanza jiji walimu zaidi ya 1,000 waliopanda madaraja mwaka mmoja na nusu uliopita bado hawajarekebishiwa mishahara.Hii ina maana kuwa ktk zoezi hili hawatalipwa malimbikizo yao kwa kua mishahara yao haijarekebishwa.Hii ni kwamba leo selikali km watalipa bil 40,watakuta kesho wanadaiwa bil100. Ni ajabu kwa raisi wa nchi kulidanganya Taifa kuwa kuwa suala la malimbikizo kwa watumishi wa umma halitatokea tena.kwa upungufu wa mishahara walimu wanalazimika kukopa kny mabenki si kw lengo la kujenga bali kufidia mapungufu ya mshahara.kibaya zaidi ili upate mkopo ni lazima uhonge 50,000 tabia hii iko ktk tawi la Nmb kenyata usipotoa utazungushwa zaidi ya miezi 2 kwani kwa hp Mza unaruhusiwa kukopa nmb tu
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  anatafuta hela ya kula tu huyu
  sheria za kuanzisha mgomo anazijua je amezifuata au anatafuta kujitangaza
  CWT siwaamni ndiyo maana Kigoma walitaka kujitoa
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  naona anataka kupata umashuhuri kwani amesikia madai yao yanashughulikiwa ndio anapiga kelele za mgomo, huyu ni kibaraka wa serikali nadhani imefika wakati walimu waanze kimfukuza kwenye cheo hiki, anaendesha chama cha walimu kama CCM
   
 10. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Teachers diserves no pay as a price for their irresponsibity, as they don't teach sons a lesson that there is no hope in green and yellow...

  Shikaaaamoooooo! Mwalimu

  Natania tu Sir
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ndo take home ya mwalimu, askari polisi, magereza, na idara nyingine kibao kama malipo ya kazi yao ya mwezi mzima
   
 13. H

  Haika JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hv ugumu wa kuwalipa uko wapi? Manake hii ni fedheha nyingine
   
 14. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Hawana uwezo wa kugoma hawa....wanatishia kujamba wakati wana tumbo la kuhara. Hw comes umwambie mwl wa primary school mwenye div 4 ya point 28 agome ataenda wapi? Afadhali wenye diploma na degrees wanaweza coz wanaweza kwnda private bt wao ni wachache hawataweza kuongoza mgomo....so i ts better wakae kimya!
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  hawa nao, kila siku mgomo mgomo, muda ukifika utasikia ooooooooh, tumeahirisha. Mimi nadhan njai nzuri ya mgomo ni kutofundisha tu badala ya kutoingia darasani kwani matokeo ya njia hii ndo serikali itatia akili
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mi nadhani wafundishe topic za ahera, itasaidia serikali kuamka pindi idadi ya watakaofeli iongezeke kushinda ya mwaka juzi. Hili litasaidia kuitia akili serikali adabu.
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hawana jeuri
   
 18. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hawa viongozi wa CWT wanataka pesa za krismass wakipewa tu kimyaaaaaaaaaaa
   
 19. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Halafu watu wanapowatetea kitu chenye maslahi kwao(POLISI),wanawapiga mabomu na maji ya kuwasha.Mi Polisi ya Tanzania MIPUUZI sana.
   
 20. Nyaluhusa87

  Nyaluhusa87 JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,288
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  hao nimeshawazoea kupiga kelele kama hizo halafu muda ukifika hakuna anayegoma.
   
Loading...