Tena deni la kitapeli na kiwizi na kiunyanganyi wa kijanja, la mabilioni mengi sana kulinganisha na madai halali ya walimu. Dowans wana nguvu ya kuitetemesha serikali kuliko walimu???? Au tuseme kuwa serikali inaiogopa Dowans kuliko walimu??? Maana wao walikwenda mahakamani kwa madai ya kitapeli na serikali inawalipa fasta. Walimu walikwenda mahakamani na wakaambulia amri ya kurudi darasani kwa nguvu! Na wakati wa sensa tya taifa wakanyanyaswa kwa kukatwa majina yao kama adhabu. Kwa mtaji huo kwa nini watoto wetu wasifeli form four? Kwa uwazi huu kulikuwa na haja ya kuunda tume kuchunguza hii mass failure?? Sas eti madai yao ya msingi na kweli kabisa yanahusushwa na CHADEMA! Haiingii akilini. Waalimu, badilikeni. Kwa muda mrefu ninyi ndo kada iliyokuwa imeishikilia CCM. Haya, kalaga baho. Nyie ndo maskini kuliko wafanyakazi wengine wote. Mnafanya kazi vujijini katika mazingira ya ajabu, mnakaa katika vijumba vya ajabu, kazi yenu haithaminiwi kwa kuwa hata vitendea kazi hampewi, bado hampandishwi madaraja na wale waliopandishwa hawalipwi, mnatukanwa najuu ya yote bado mnawafundisha watoto kuimba wimbo wa CHAMA CHETU CHA MAPINDUZI CHAJENGA NCHI! Duuuuu!Dowans wameanza kulipwa deni lake
weweee! wacha kabisa. unafikiri zile sifuri 62% zimetoka wapi?
Dowans wameanza kulipwa deni lake
Ninakubaliana na na wewe kabisa kwamba CWT na yenye ni mzigo mwingine kwa walimu. Hii mijamaa inajali tu kukusanya hela, lakini hakuna namna yoyote huyo mwalimu anafaidika na hela anayokusanya kila mwezi.Mkuu kuongeza mishahara katika uchumi ambao haujadhibitiwa inasaidia nini? Kwa ujumla Kikwete ameshindwa. Kulinganisha elimu ya mwenye degree anayefundisha shule ya msingi, sekondari na Chuo kikuu ni kutokutenda haki ya mzigo alionao kila mmoja katika level yake. Mshahara hautolewi kwa elimu bali kazi unaoyofanya. Tumeona watu ni darasa la saba lakini wanalipwa vizuri kuliko mwenye degree lakini katika kada tofauti. Hao ulio wataja wote ni walimu na wote wako katika ELIMU katika level tofauti yenye mzigo tofauti wa kazi. Tusizunguke, Kikwete kazi imemshinda na CWT nao ni Bongo lala.
Usiseme hawana umoja wanarudi kazini je wanafanya kazi? walimu wengi kwa sasa wanajishughulisha na biashara zao ili kujiongezea kipato wale ambao hawana biashara wanaingia darasani mara moja kwa wiki,huwa wanagoma then wanarudi wenyewe bila mashauliano .hawana umoja wapowapo tu.