Walimu wairarua Serikali

Walimu wairarua Serikali

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kutokubali kupitishwa kwa bajeti ya serikali ya mwaka 2013/14 hadi hapo madai yao yatakapokuwa yamelipwa.Pia chama hicho kimeionya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha propaganda za kuwasingizia kuwa wanatumiwa na chama kimoja cha upinzani kudai malimbikizo yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiel Olouch alipokuwa akifungua semina ya uundwaji wa katiba mpya, umuhimu na wajibu wa walimu wenye ulemavu katika ushiriki ndani ya katiba hiyo.Akizungumza katika semina iliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la The Foundation For Civil Society, Olouch alisema kuwa serikali imekuwa na tabia ya kutengeneza propaganda za kukihujumu chama chao ili wasifanikiwe kudai madeni na haki zao za msingi.Alisema serikali imeshindwa kukaa nao meza moja kwa lengo la kulipa madeni ya walimu na badala yake imekaa na kutengeneza propaganda kwamba CWT kinatumiwa na chama kimoja cha upinzani.

"Nataka kuwauliza ndugu zangu walimu, ni kweli sisi tunadai madeni yetu kwa kutumiwa na chama cha siasa? Serikali walituandikia barua wakieleza kuwa sisi tunatumiwa na chama kimojawapo cha siasa, japo hawakukitaja lakini si inajulikana wazi kuwa kwa sasa chama ambacho kina nguvu ni CHADEMA?"

Sasa CHADEMA ndicho kimeelekeza sisi tusilipwe fedha zetu, naeleza kuwa kamwe CWT hatutakubali serikali ikae pale bungeni kupitisha bajeti yake ya mwaka wa fedha 2013/14 bila kutulipa fedha zetu, ikishindikana tutafanya mambo makubwa zaidi ya yale ya mwaka jana," alisema Olouch.Aliongeza kuwa serikali pamoja na CCM wana makusudi ya kuwagawanya walimu ili wasipate nguvu ya kudai haki zao za msingi na ndiyo maana haitaki kukaa meza moja na walimu ili kutatua matatizo yao.

"Mpaka sasa walimu wanadai sh bilioni 25. Wapo walimu zaidi ya 70 ambao wanatakiwa kupandishwa madaraja, lakini bado hawajapandishwa na kuna walimu 6,000 wamepanda madaraja, lakini hawajarekebishiwa mishahara yao."Hayo yote tukiohoji tunaonekana tunatumiwa na vyama vya siasa hususani wapinzani jambo ambalo ni propaganda za kutaka kuwadhoofisha walimu wasidai haki zao," alisema.Oluoch aliongeza kuwa hawawezi kuendelea kupokea mshahara wa sh 270,000 kwa mwezi na kusisitiza kuwa serikali isipokubali kulipa madeni yao na kuwapandisha madaraja walimu waonastahili pamoja na kurekebisha mishahara yao watafanya uamuzi mgumu.

Naye mwakilishi na mratibu wa semina hiyo, David Kisamo alisema itasaidia kuwawezesha walimu kutoa maoni yao ni jinsi gani waweze kupata haki zao katika katiba mpya.Alisema ili mwalimu aweze kufanya kazi zake vizuri, ni lazima katiba imtambue na kumpa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa kwani walimu wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu.

Alieleza kuwa ugumu wa maisha kwa mwalimu ambao unasababishwa na serikali unawafanya kutotambua haki zao na kujikuta wanagawanyika.Taarifa hii chanzo chake ni Gazeti Baba la Tanzania Daima taarifa ikiwa imeandaliwa na mwandishi Danson Kaijage kutoka Dodoma
 
Nikweli serikali walimu haitujali,wametutelekeza huku mapolini kwenye shule zao za kata,wache watajuta wasiporekebisha mishahara na kutupa nmarupurupu.
 
Wakurya na Wasukuma vipi, nao wanapaswa kuirarua serikali kwa sababu haiwajali pamoja na kuwa wamejaliwa kuwa na migodi mingi ya madini huko!
 
Hii kada ya elimu hivi sasa ni kero tupu. Kwa taarifa za uhakika kabisa ni kwamba hata wahadhiri wa vyuo vikuu hawajalipwa madai yao ya tangu mwaka 2011. Yaani kufanya kazi wizara ya elimu ni kama laana hivi. Binafsi najuta kuwa mwalimu. Na kwa hakika nafanya jitihada za hali na mali kuhakikisha naondoka kwenye hii kada. Maana kuendelea kufelisha wanafunzi siwezi, kwakuwa nawaonea huruma. Si kosa lao. Lakini pia mimi kama mwalimu hakuna anayenijali pamoja na shida zote zinazonikabili.
Yaani kuna wakati huwa nikiangalia mazingira ya kazi nawaza ya kwamba ni bora kuwa mfagizi TRA kuliko kuwa mwalimu hata kama una degree yako.
 
Mei mosi inakaribia. Wanabip tu halafu watanyamaza hadi mwakani tena!
 
Teh,teh,teh,teh,teh.-teh,tehh,teh!Acha bana,ukishindwa umeshindwa tu we uluke,uhepe,uiname,useme ongo ote,usingizie wengine yote hayasaidii ni kazi bure yaani kama kawa sikio la kufa _______ _____likitulia kidogo la kushoto la kulia linawaka moto.Mweee!!!Mie chipo chi nchachema chio ticha chichi chacha tuchemeje hapo?chitii neno ng'o wachije wakachema maticha wamepundiswa kugoma.
 
Colonel Gaddafi captured, tortured and killed on the Road


This is exactly what gonna HAPPEN in teaching field, wanasema sisi walimu vishoka tutaona, huu unyama wa magharibi unanyemelea Tanzania...kwa njia tofauti kabisa.

na sisi walimu tunasema...hakuna hakuna allahu akbaru


GADDAFI anaakili sana, alisaidia sana waafrika lkn wamemchinja. Tena sio WAMAREKANI...

Colonel Gaddafi captured, tortured and killed on the Road - YouTube

Gadhafi Son Mutassim Defiant Before Rebel Captors - IndepthAfrica - YouTube



INCHI HII inatesa watetezi, ni muhimu sana kuangalia na video hii..

http://www.youtube.com/watch?feature=fvwp&v=kAHBjcxA-SI&NR=1
 
Serikali iliyoko madarakani inaendeshwa kulingana na sera(ilani) ya chama cha mapinduzi na sera hizi huwa ni mikakati iliyoandaliwa kuongoza nchi kwa miaka 50 mbele.

Kiongozi yeyote aliye ndani ya utawala wa ccm hawezi kuongeza jambo lolote ambalo halimo ndani ya ilani ya ccm,

kwa maana hiyo matatizo ya walimu na wafanyakazi wengine wa serikali juu ya kuongezewa mishahara na kuboreshewa mazingira mazuri ya kazi ni vitu ambavyo havimo ktk ilani ya chama cha mapinduzi na kamwe havitaweza kuingizwa kwenye ilani hiyo ya ccm kwa sababu ilani ya sasa ya ccm ni mikakati ya miaka 50 mbele(wanahisi watatawala milele).

Kama mlipata kumnukuu Kikwete aliwahi kusema HAIWEZEKANI KUWAONGEZA MSHAHARA WAFANYAKAZI WA SERIKALI.

HIVYO BASI MADAI YA WALIMU KAMWE HAYAWEZI KUTEKELEZWA NA SERIKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWA MADAI YAO SI SEHEMU YA ILANI YA CHAMA.


CHADEMA PEKEE NDIO MUAROBAINI WA MATATIZO YA WATANZANIA WOTE.


KWA KUWA NDICHO CHAMA PEKEE CHENYE SERA MADHUBUTI ZENYE LENGO LA KUMNUFAISHA KILA MTANZANIA NA KUKUZA UCHUMI KWA MAENDELEO YA TAIFA KWA UJUMLA.
 

Kama mlipata kumnukuu Kikwete aliwahi kusema HAIWEZEKANI KUWAONGEZA MSHAHARA WAFANYAKAZI WA SERIKALI.

HIVYO BASI MADAI YA WALIMU KAMWE HAYAWEZI KUTEKELEZWA NA SERIKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUWA MADAI YAO SI SEHEMU YA ILANI YA CHAMA.
Kwenye suala la kuongezwa kwa mishahara sitaki kuwa mnafiki. Kikwete ni rais pekee katika historia ya nchi hii ambaye ameweza kuongeza mishahara ya wafanyakazi hadi kiasi cha asilimia zaidi ya 200 katika kipindi cha miaka isiyofikia kumi aliyokuwepo madarakani.

Lakini changamoto aliyonayo Kikwete ni kushindwa kusimamia uchumi imara wenye mfumko mdogo wa gharama za maisha. Kutokana na kushindwa kusimamia hilo, wafanyakazi wamejikuta kila kinachoongezeka hakitoshi kumudu hali ya maisha ya wakati husika. Na wakati mwingine kupanda kwa gharama za maisha kumekuwa ni kukubwa zaidi ukilinganisha na mishahara inayoongezwa.

Changamoto nyingine ambayo ameshindwa Kikwete kuikabili ni uwiano wa mishahara kati ya kada moja na nyingine. Tutorial assistant wa chuo Kikuu ambaye ana degree moja. Analipwa mshahara milioni moja na kidogo, wakati mwalimu wa secondary ambaye na yeye ana degree moja analipwa mshahara laki nne na kidogo kama siyo tano. Hapa uwiano upo wapi, ilihali wote wana degree moja na ni wafanyakazi wa serikali? Basi na mwalimu wa sekondary alipwe angalau laki tisa au milioni moja amkaribie kidogo huyo tutorial assistant?

Mwalimu wa secondary mwenye masters analipwa around laki nane, wakati wafanyakazi wa kada zingine wanalipwa hadi milioni moja na laki nane. Tofauti ya milioni moja nzima, ilihali wote ni waajiriwa wa serikali. Hapa haki ipo wapi? ukizingatia wote wana qualifications zinazofanana?

Na la mwisho ni kwamba mazingira ya kazi ya mwalimu ni magumu na yasiyo na nafasi ya kumruhusu mwalimu kujikwamua kimaisha. Anachokipata mwalimu ni kile kinachoitwa hand to mouth. Hawezi kujenga wala kusomesha mtoto wake kwenye angalau shule ya private. Wakati wafanyakazi wengine wa serikali wakilipwa mishahara mikubwa sana, na marupurupu kibao. Safari za kila kuchapo. Je mwalimu ana marupurupu gani? Hata hayo malimbikizo tu kuyapata ni shida.

Halafu angalia treatment anazozipata kutoka kwa maafisa elimu na waratibu kata. Yaani ni shida tupu. Mwalimu anadharaulika kwa kweli siyo uongo. Ile heshima aliyokuwa nayo mwalimu wakati wa Nyerere imekwisha kabisa. Najiuliza kwanini wakati wa Nyerere kulikuwa na usawa kati ya wafanyakazi wa serikali, halafu leo kunakuwa na gap kubwa sana kati ya wafanyakazi wa serikali wenye elimu sawasawa?
 
Tutapata marupurupu siku ya kusimamia uchaguzi 2015. Tuvute subira.
 
Mnatumiwa kweli ndiomaana mnapayuka payuka kwa wananchi na si kufanya kazi kitaalamu tu na kuona selikali hailipi mpaka shinikizo.
Pelekeni hoja kwa wabunge wetu wapendwa deni la mfanyakazi selikalini lililoombewa madai na halijalipwa hadi miezi mitatu lilipiwe riba ya 10% kila mwezi hadi siku ya malipo.
 
Nakumbuka mzee wetu alisema. "Hata mgome kwa miaka 8 mshahara wa 315,000 hamtaupata" Kwa miaka hiyo sijui sasa imebaki mingapi kutimia tangu 2010?
 
huwa wanagoma then wanarudi wenyewe bila mashauliano .hawana umoja wapowapo tu.
 
Lol...270000 dah jamani Serikal ione hata aibu japo m nakula 90 2 kwa mwezi...
 
hakuna chama cha kijinga kama CWT...viongozi kule ni mafisadi wanagawana tuu 2% ya mshahara wa mwalimu kila mwezi.
 
Kwenye suala la kuongezwa kwa mishahara sitaki kuwa mnafiki. Kikwete ni rais pekee katika historia ya nchi hii ambaye ameweza kuongeza mishahara ya wafanyakazi hadi kiasi cha asilimia zaidi ya 200 katika kipindi cha miaka isiyofikia kumi aliyokuwepo madarakani.

Lakini changamoto aliyonayo Kikwete ni kushindwa kusimamia uchumi imara wenye mfumko mdogo wa gharama za maisha. Kutokana na kushindwa kusimamia hilo, wafanyakazi wamejikuta kila kinachoongezeka hakitoshi kumudu hali ya maisha ya wakati husika. Na wakati mwingine kupanda kwa gharama za maisha kumekuwa ni kukubwa zaidi ukilinganisha na mishahara inayoongezwa.

Changamoto nyingine ambayo ameshindwa Kikwete kuikabili ni uwiano wa mishahara kati ya kada moja na nyingine. Tutorial assistant wa chuo Kikuu ambaye ana degree moja. Analipwa mshahara milioni moja na kidogo, wakati mwalimu wa secondary ambaye na yeye ana degree moja analipwa mshahara laki nne na kidogo kama siyo tano. Hapa uwiano upo wapi, ilihali wote wana degree moja na ni wafanyakazi wa serikali? Basi na mwalimu wa sekondary alipwe angalau laki tisa au milioni moja amkaribie kidogo huyo tutorial assistant?

Mwalimu wa secondary mwenye masters analipwa around laki nane, wakati wafanyakazi wa kada zingine wanalipwa hadi milioni moja na laki nane. Tofauti ya milioni moja nzima, ilihali wote ni waajiriwa wa serikali. Hapa haki ipo wapi? ukizingatia wote wana qualifications zinazofanana?

Na la mwisho ni kwamba mazingira ya kazi ya mwalimu ni magumu na yasiyo na nafasi ya kumruhusu mwalimu kujikwamua kimaisha. Anachokipata mwalimu ni kile kinachoitwa hand to mouth. Hawezi kujenga wala kusomesha mtoto wake kwenye angalau shule ya private. Wakati wafanyakazi wengine wa serikali wakilipwa mishahara mikubwa sana, na marupurupu kibao. Safari za kila kuchapo. Je mwalimu ana marupurupu gani? Hata hayo malimbikizo tu kuyapata ni shida.

Halafu angalia treatment anazozipata kutoka kwa maafisa elimu na waratibu kata. Yaani ni shida tupu. Mwalimu anadharaulika kwa kweli siyo uongo. Ile heshima aliyokuwa nayo mwalimu wakati wa Nyerere imekwisha kabisa. Najiuliza kwanini wakati wa Nyerere kulikuwa na usawa kati ya wafanyakazi wa serikali, halafu leo kunakuwa na gap kubwa sana kati ya wafanyakazi wa serikali wenye elimu sawasawa?

Mkuu kuongeza mishahara katika uchumi ambao haujadhibitiwa inasaidia nini? Kwa ujumla Kikwete ameshindwa. Kulinganisha elimu ya mwenye degree anayefundisha shule ya msingi, sekondari na Chuo kikuu ni kutokutenda haki ya mzigo alionao kila mmoja katika level yake. Mshahara hautolewi kwa elimu bali kazi unaoyofanya. Tumeona watu ni darasa la saba lakini wanalipwa vizuri kuliko mwenye degree lakini katika kada tofauti. Hao ulio wataja wote ni walimu na wote wako katika ELIMU katika level tofauti yenye mzigo tofauti wa kazi. Tusizunguke, Kikwete kazi imemshinda na CWT nao ni Bongo lala.
 
Back
Top Bottom