Walimu waahidi makubwa - Lazima kitaeleweka

GIB

JF-Expert Member
Mar 2, 2012
336
92
Lazima kitaeleweka!

Viva walimu

attachment.php



Source Habari leo
 

Attachments

  • walimu2.jpg
    walimu2.jpg
    16.8 KB · Views: 3,758
tutapambana mpaka tone la mwisho. je hawajui walimu ni sawa na ngombe wa maziwa. ukimchukiza kidogo tu hupati maziwa. pole yao wanafunzi yaani wataishi kupata division iv na 0.
 
Mungu wangu 1+3=13????? na mbaya zaidi mtoto akiambiwa kitu na mwalimu huwezi kumbadilisha, hata kama nawewe ni mwalimu wa chuo kikuu. wewe utabakia kuwa baba au mama tuu na hatakuruhusu umpotoshe kile alichofundishwa na mwalimu wake darasani na akawekewa alama ya vema
 
Nzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu, ndivyo watakavyo kufa CCM kwenye mioyo ya walimu maana walimu wamekata tamaa kwa kiasi kikubwa halafu serikali inawalazimisha kumaliza mgomo kwa njia ya mahakama bila hata kueleza angalau wanaweza kuongeza au kulipa nini kwenye list ya madai ya walimu.

Hatua yoyote watakao chukua iwe kuamua kufelisha wanafunzi, au kuendeleza mgomo kama jinsi wanavyo fanya, matokeo yake yatakuwa ni janga kwa taifa.

Tusubir tuone na kipimo chetu kiwe mitihani ya kidato cha pili inayo tarajiwa kufanyika miezi miwili ijayo.
 
Duh! Kali kweli kweli.Nzuri lakini,maana bila Mwalimu tusingekuwa na Rais,Wabunge,Wanasiasa,Madaktari,Wahasibu na Walimu wenyewe.Sasa sijui yupi muhimu,Daktari au Mwalimu?Nisaidieni
 
mtoto wa mlalahoi ndiye anayedhurika at last! wakwao wanasoma kwenye ma-academy na ma international schools! au nje ya nchi kabisa! stupid president ever! thats kikwete!

cacico unataka ban nini aise
Punguza hasira aise


shostito msiri wangu msikilize kaka mkubwa Mr Rocky. Ila miye kweli sijenda jon nnimegoma bado i will be the last person kwenda aisee. let matters take their natural way to me.
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha ha .....
hiyo ni hisabati....
sipati picha ticha wa geography atakavyokuwa anafundisha "nchi ya Tanzania iko barani Msumbiji, upande wa kaskazini imepakana na Marekani upande wa kusini imepakana na Ivory Cost..........na mengi tu yanayofanana na hayo"
Kazi ipo..........
 
Dawa ya waalimu ni mshahara tu,wakitishiwa kusitishiwa mishahara yao wananywea.Hapa kitakachofanyika ni kuimarisha Idara ya ukaguzi wa shule.
 
Kwa kweli hiyo picha inafundisha mengi, kama kweli waalimu watafundisha namna hiyo basi hatuna wasomi tena huko mbele. Lakini nimeipenda kwa sababu inawapa hawa watawala onyo kwamba ni kitu gani mwalimu anaweza kufanya, kama wataelewa natumaini watachukua hatua stahiki.
 
Back
Top Bottom