Walimu tanga wasambazwa vijijini

miamia7

Senior Member
Jan 11, 2016
195
191
Katika mkoa wa tanga walimu wamejikuta wakipata wakati mgumu baada ya agizo la serikali kuwaondoa walimu walioko mijini na kupelekwa vijijini huku wakilipwa ghalama ndogo sana za uhamisho, labda ma gt humu mtoe mwanga kwa watumishi hawa ili wadai haki zao vizuri ni vigezo vipi hutumika kulipa uhamisho yawezekana utaratibu ukawa umebadilika mana awamu hii kila siku mambo yanabadilishwa,karibuni
 
Baadae tena watawarudisha mjini? Mjini ndio kuna wanafunzi wengi,kwa mfano shule za mjini si tanga tu hata mikoa mingine kuwa na form one 300 au zaidi ni kawaida au darasa la kwanza 400 ,sasa swali je baada ya muda watoto kama hao wakisonga mbele,walimu watawapata wapi wakati serikali haiajiri kwa sasa?
 
Serikali iairi walimu na sio kupunguza walimu waliopo mashuleni jamani, kama uchumi unakua kwa kasi hofu ya nini kuajiri walimu kwa nini kucheza na elimu ya watoto wa maskini amabo ndio wahanga wa hizi shule za serikali? Halafu hapo mbunge atasimama bungeni na kupongeza walimu kutolewa shuleni fulani kupelekwa jimboni mwake badala ya kuishauri serikali iajiri walimu waliomaliza mafuzno wanazaagaa mitaani na kuambiwa wamejifungia kwenye box, hii sio sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom