WALIMU: No 'big result now' without 'big salary now'!

mutahappy

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
529
Reaction score
188
"The way you treat your EMPLOYEE is the way they treat your CUSTOMERS, there is no big result now without big salary now"
huo ni ujumbe unaosomeka katika sms zinazo sambaa kwa walimu.

Mimi kama mwalimu naunga mkono hoja kwa 100% kwan hamna Taifa imara bila walimu madhubuti na wanao thaminiwa, kueshimiwa.

Teaching is the mother of all profesionals in the world.
Teachers can either build a strong or weak country.
 
Wanaoafiki waseme ndiyoooo,....Wasioafiki waseme Hapanaa....!!!! Nadhani wanaoafiki Wameshinda.....
 
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?
 
Hivi hapo Kinondoni Mtaa wa Ufipa hicho kiasi mnacholipwa kinatosheleza kukidhi mahitaji yenu muhimu?
 
naunga mkono hoja.....hii wizara ilinifanya nikimbie hii huduma,walinipeleka kwenye shule ya kata ambayo mie ndiye mwalimu wa kwanza pale na ndie nilieanzisha mchakato wa kuanza kupokea wanafunzi tena hukoo mbali kijijini kbs halafu hawakunipa haki yangu na nikakimbilia kwenye sector nyingine,i hate these people for sure......ngoja niwaunge tu mkono hawa walimu
 
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?

Unamuuliza nani sasa! Kama unajua si umwelekeze mleta uzi....!!
 
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?

Idiotic question on red. Unauliza majibu?

At least unajua kuwa si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake: hakuna mbadala wa MORALE ya ufundishaji mashuleni kwa kubadili badili majina na slogans huku unawanyonya watendaji na kujinufaisha kwa posho.

Ndugu yangu uliyegoma kutumia akili zako, ni hatua gani serikali imepiga kwa kuleta msamiati wa KILIMO KWANZA mashambani kwa pembejeo na urasimu ule ule?

Mtabadili majina hadi maneno yaishe, lkn kama hamkujifunza kuwajali wanaotumika, basi kina Kagame wataendelea kutupuuza huku tunalalama kama wauza matap-tap waliodhulumiwa na askari wa jiji.
 
Matokeo makubwa sasa bila mikakati ya muda mrefu ni upumbavu mkubwa,hiyo pesa ya semina wangenunulia madawati huko vijijini ambako magogo yanavunwa lakini bado wanakaa chini,

1)Shule ziwe na mazingira ya kusoma kweli
2)Mitaala ya masomo irekebishwe
3)Walimu wapewe wanachokidai
4)Wazazi watimize wajibu wao
5)Vijijini kupewe nguvu ya ziada kubadili hali ya elimu

Tofauti na hapo tusubiri hili janga lifike elimu ya juu muda siyo mrefu
 
Mkuu, si kila mtu anaweza kujibu swali hilo. maana wengi wanaoiba iwe serikalini, kwenye makampuni binafsi au mashirika ni wale wenye mishahara mikubwa.
 
Bora wewe umeonesha mwanga kuliko wengine wanaona suala la mishahara mikubwa tu ndo suluhisho la matatizo ya elimu nchini.
 
Walimu hamna lolote tuendelee na woga tu

Ogopa sana kitu inaitwa 'Passive Resistance', bila jasho wala kukunjana mashati watu wanadai haki zao. Serikali inayotenga 10bn kugharamia matibabu ya viongozi wastaafu ilhali hawaumwi at the same time inashindwa kulipa malimbikizo ya ya walimu 26bn for years unadhani ni serikali ya kibinadamu au ya kuzimu?
 
Mkuu, si kila mtu anaweza kujibu swali hilo. maana wengi wanaoiba iwe serikalini, kwenye makampuni binafsi au mashirika ni wale wenye mishahara mikubwa.

Wanaoiba serikalini ilhli wana mishahara mikubwa sio justification ya serikali kuwapunja walimu mishahara, hizo ni sababu nyepesi tena za kisiasa. Hainiingii akilini kuniambia ukiongeza mishahara haitaleta mabadiliko. Nikukumbushe kuwa, uwepo wa wizi serikalini na kwenye mashirika ya umma ni uzembe mwingine wa serikali na sio jambo linalohusiana na haki wanazodai walimu.

Unaweza kuongea maneno yako ya kuungaunga kadiri upendavyo, lkn nikuulize swali: mbali na mishahara, walimu pia wanadai malimbikizo ya stahili zao za uhamisho na likizo, je nahizo nazo hawapewi sababu wataiba?

Mimi sio mwanasiasa bwana, usinijie na hoja za kuungaunga, hapa tunazungumzia mtu kujikimu ili aweze kutumikia ajira yake kwa ufanisi
 
Katika mazingira magumu km haya wamekuja tena na kitu kinaitwa ophras sijui hopeless hawa watawala sijui wa karne gani kwani ni upuuzi kumbana mwalimu ambaye maslahi yake ni duni hata ukimbana hana kitu cha kupoteza
 
Wanaoiba serikalini ilhli wana mishahara mikubwa sio justification ya serikali kuwapunja walimu mishahara, hizo ni sababu nyepesi tena za kisiasa. Hainiingii akilini kuniambia ukiongeza mishahara haitaleta mabadiliko. Nikukumbushe kuwa, uwepo wa wizi serikalini na kwenye mashirika ya umma ni uzembe mwingine wa serikali na sio jambo linalohusiana na haki wanazodai walimu.

Unaweza kuongea maneno yako ya kuungaunga kadiri upendavyo, lkn nikuulize swali: mbali na mishahara, walimu pia wanadai malimbikizo ya stahili zao za uhamisho na likizo, je nahizo nazo hawapewi sababu wataiba?

Mimi sio mwanasiasa bwana, usinijie na hoja za kuungaunga, hapa tunazungumzia mtu kujikimu ili aweze kutumikia ajira yake kwa ufanisi

Kusema kuwa walimu wanadai malimbikizo ya stahili za likizo na uhamisho kwa ujumla bila ya kutolea mifano ni makosa. naamini kuwa wapo walimu wenye madai yao stahiki lakini naamini pia wapo walimu ambao hawana madai au wana madai ambayo hayana vielelezo. ni jukumu la mwajiri na mwajiriwa kukaa pamoja na kujadiliana juu ya madai hayo.
 
Waliofaulu vizuri nakuwa waalimu deserve big salary wale mapompopo walio feli na kukimbilia ualimu kama plan B deserve small salary. Unavuna ulichopanda. Period
 
Back
Top Bottom