Walimu ni kada ilopoteza muelekeo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu ni kada ilopoteza muelekeo.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Malolella, Jun 19, 2012.

 1. M

  Malolella JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Walimu mliingia na vyeti vya kufoji? Mbona mnakandamizwa kama watu ambao hamjagusa hata darasa? Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa tz. Ajira mpya ngazi ya cheti: mwl 244,400/= afya 472,000/= kilimo/mifugo 959,400/= sheria 630,000/=. Ngazi ya Diploma: mwl 325,700/=, afya 682,000/=, kilimo/mifugo 1,133,600/=, sheria 871,500/=. Ngazi ya Degree. Mwl 469,200/=, afya 802,200/=, kilimo/mifugo 1,354,000/=, sheria 1,166,000/=. Kwanini walimu mnanyanyaswa hivi katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Kisa cha kuwadharau na kuwapa hela kiduchu ni nini? Eti sababu mpo wengi...hiyo siyo sababu. Walimu nawaombeni muungane msimame imara kudai ongezeko la mshahara kwa 50%. Msiwategemee hao viongozi wenu wa CWT au TUCTA, hao wanatumika kisiasa! Hamtakuja kufanikiwa kupitia cwt au tucta. Nawasilisha kwa uchungu mkubwa...maana mmekuwa watumwa ndani ya nchi yenu. Tena nyie ndo mnatumika na wanasiasa..kwnye uchaguzi, sensa etc. Kataeni kupuuzwa kwa vihela hivyo, mnakosa gani ktk nchi hii?
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kazi ya ualimu, hasa katika nchi yetu, kwa kiasi kikubwa imekuwa ya wale ambao ufaulu wao ulikuwa wa madaraja ya mwisho either kwenye form 4 au 6...sasa nadhani wengi wao wamejikuta wanaona kama vile wamepata upendeleo kwenye hiyo kazi! Hapo ni mbali na wale lukuki wanaotumia vyeti bandia au vya kununua! Wewe hapo unategemea watapiga makelele hata kama wanalipwa chenga?
   
 3. s

  sawabho JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Aina ya kozi wanazosoma zinawafanya wawe Kondoo. Hawa watumishi ndio chanzo cha maenedeleo na mafanikio ya kila mtu, lakini hawalitambui hilo, wanaburuzwa tu !!!! Laiti kama nyoka wangekuwa na umoja kama nyuki, hakuna binadamu angediriki kuua nyoka.
   
 4. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  siasa imewaua
   
 5. M

  Malolella JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama kuna kaukweli hapo! Hivi inawezekanaje kada nyingine zote mishahara iwe juu halaf nyie walimu ndo daraja a chini? Nyie mliofoji vyeti na kuingia kwa madili ndio mnasababisha maslahi duni kwa walimu.
   
 6. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Jamani mnanikatisha tamaa wakati mimi ndo nasubiri kama hata tcu watanifikiria ili nikasome ualimu. Kama mambo ndo hivyo,vipi tutafika? Waalimu muungane kwa ajili ya kulikomboa taifa lenu la kesho.
   
 7. G

  Gilly Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu, tatizo sio walimu. Tatizo ni kwamba hakuna dhamira ya dhati ya kisiasa ya kuboresha elimu yetu. Wanafalsafa ya Elimu wanaamini kwamba kila mtu anafundishika. Tatizo liko katika kudharau, kuonea, kunyanyasa na kupuuza walimu wetu huku bado tunawataka watufundishie watoto wetu kwa bidii na uzalendo wa hali ya juu. Wenyewe wanasiasa wetu wanatuaminisha kwamba ndivyo walimu wanapaswa wawe hivyo na Mungu aliwaumba hivyo. Uliona wapi nchi inawapuuza walimu wake kiasi kwamba wazazi wanadiriki kuwachapa viboko walimu mbele ya wanafunzi wao? Halafu mwalimu afanye nini? Baada ya kufanyiwa vitendo hivyo, mwalimu aende tu kuwafundishia watoto wa hao wazazi waliowapiga viboko hadi wafaulu? Ungekuwa wewe uzalendo wa namna hii ungeupata wapi? Nadhani atakayefanya hivyo lazima awe na moyo kama wa Nabii fulani.
  Kwa taarifa tu walimu wapo kwenye mgomo baridi tangu siku nyingi hata hawana haja ya kuhamasishwa na CWT kugoma. Walikwishagoma (baridi) siku nyingi tu Watanzania wasubiri "failures" kwenye ngazi zote hasa za chini. Au wategemee "ufaulu" wa kwenda "Form 1" wa wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika. Ningewasifu CWT kama wangefanya kazi ya kuhamasisha walimu waache mgomo baridi na badala yake wafanye kazi.
   
 8. M

  Malolella JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu upo sahihi. Walimu wamekuwa wakiidai serikali pesanyingi tena kwa muda mrefu bila mafanikio. Kwa staili hii sidhani kama walimu wanaweza kufanyakazi kwa moyo wao wote wakati mwajiri wao anawanyanyasa kimaslahi. Nafkr walimu wanaenda kazini2 ili kutimiza masharti yakwenda kazini kwani wasipoenda watafukuzwa, hawaendi kufanyakazi ila wanaenda kwa sababu wanatakiwa kwenda! Pole sana serikali dhaifu inayoongozwa na chama dhaifu na inataka kutengeneza taifa dhaifu.
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  hivi wewe unaish kwa data za miaka gani? je ni mwalimu wewe? au wewe ni afisa takwimu? basi ungeuliza kwanza kabla ya kuanza kuleta hoja zisizo na mashiko. hivi wewe unazodata za wanafunzi waliosoma degree ya ualimu kuanzia miaka ya 2000? je unajua data za waliosomea ualimu wa sayansi walikenda kwa point ngapi?

  mbona hakuna vilaza kama wanaokwenda kusoma ngazi ya cheti katika mifugo na sheria?ama unafikiri hatuyajui? basi nikutoe ujinga hizi data tunazo na ukweli wa waalimu pia tunaujua na kwanini hawawez kuishinikiza serikali kufanya lolote tunaujua.
  so far elimu siyo ishu ni kaajiriwa, awe na elimu ndogo awe na nini mbona huko kwenye sekta za mifugo na sheria kuna elim za vyeti hadi degree? kwanini wao walipwe tofauti? hapo ndio msingi wa swali swala eti wana elimu ndogo unazijua cv za wote?

  manake kama kuna elimu ya cheti cha sheria na ualim nao unayo iyo elim acheni matani na waalim ishu n kwamba inatumika loophole ya ualimu ni wito na heshima tunazolazimishwa as role models basi ninyi mnatufanya kama wajinga. ninao uhakika is just a matter of chance lkn waalimu wengi wanaelimu kubwa nna wako humu mashuleni kuliko hata nyie mnajiona mnaelimu kubwa ama akili sana.
   
Loading...