Walimu nao wapewe Posho za mwezi kama maaskari

Askari polisi mwenye elimu ya kidato cha nne:-kipato chake kwa mwezi ni kama ifuatavyo hapa chini:-

Basic salary ni Tsh.430,000/=
Posho ya chakula Tsh.300,000/=
Posho ya vinywaji Tsh.100,000/=
Posho ya mavazi Tsh. ............/=
Posho ya nyumba Tsh............./=

Bado unaweza kukuta askari huyu ni traffic barabarani,yupo idara ya upelelezi au katika vitengo vingine ambavyo sent nje ya mshahara haikosekani.

Hapo hujamgusa graduate wa jeshi la polisi!!Dah walimu tuna hali ngumu sana ndg zangu.
Nimeishi na Dem Askar Askar nao njaa Kali tu asikudanganye mtu labda ubahatike uwe kitengo Cha barabaran au Doria za mara kwa mara hapo pesa ipo tofaut na hapo Ni hamna kitu maisha yao Ni sawa na Mwalimu tu ,coz jumla posho na mshahara kwa pamoja haivuk laki Saba wanachezea laki sita na vitoto na ukumbuke hiyo posho kwenye mafao haihesabik kabisa .
 
Ahsante kwa ufafanuzi
Askar hawez mfikia Mwalimu kwa mshahara Hilo Nina uhakika nalo kabisa .kinachomboost askar Ni ile posho ambayo kwenye mafao Haina madhara yoyote Yale .

So hapa kwa upande wa mafao mwalim lazima ampige gepu kubwa Sana askar ila nae askar anakuja mpiga gepu Mwalimu kwenye kaposho tu .

Take home ya askar anaeanza Kaz Ni around 350 wakat Mwalimu grade A 360,Diploma 450,bachelor 550 hizo Ni makadirio maana sijaweka visent .
 
Yaani unazungumzia hela utakayo kuja kuipata ukiwa na miaka 60?? Kweli walimu mna safari ndefu.
 
Ungeandika mwalimu ambaka mwanafunzi wake, au mwalimu akimbia na pesa za ujenzi wa madarasa, watu was ofisi ya rais wangefungua haraka sana kuusoma huu uzi kwa lengo wapi uko waende mshugulikia uyo mwalimu ili wapate sifa

Mwalimu asikilizwi matatizo yake bali anashugulikiwa makosa yake kwaiyo mitano tena mwalimu usife moyo
Nimesoma point zako nikajikuta nacheka kwa sauti kubwaa kwenye daladala......mpka watu wamegeuka kunitazama....
 
Habar zenu mabibi na mababu..

Mwalimu ni mtu anaesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu. Mwalimu ndie anaezalisha Madaktari, manesi, bwana afya, wanasiasa, wafanyabiashara n.k, na wote mnaweza kukubaliana nami kuwa bila mwalimu huenda usingeweza kusoma, kuhesabu na kuandika.

Pamoja na uzito huo alonao mwalimu lakini hakuna watumishi wa serikali wenye hali mbaya ya kiuchumi kama walimu yaani mishahara ni midogo, mikopo kwenye mabenki, hakuna nyongeza ya mshahara, hakuna kupanda madaraja, hana cha kulipwa over time, hakuna cha pesa za semina kama zamani, hakuna ata kudunduliza kupata hela ya tuisheni yani ni shida tupu zimewajaa.

Mbaya zaidi kwenye sekta ya ualimu kila mtu ni bosi wako yani hata mwenyekiti wa mtaa anaweza kuja ofisini kwako na akakugombesha na hata kukutia makofi, ni sekta ambayo imeshushiwa heshima kwa kiasi kikubwa sn.

Leo hii ukimkuta mwalimu barabarani anaongea peke yake unaweza kusema amemeza notes kumbe ni msongo wa mawazo unampeleka puta Vibaya mno akifikiria ni miaka mitano sasa lakini bado mshahara ni ule ule hakuna ata senti ya nyongeza, hajapanda daraja, anachopokea mwisho wa mwezi ni laki mbili akikatwa mkopo alochukua benki, huku ukizingatia gharama za maisha zimepanda na familia imeongezeka.

Kiukweli ukipasua vifua vya walimu utakutana na masononeko makubwa mnoo, walimu wamechooka sana ule uvumilivu walokuwa wanasifiwa nao sasa haupo tena nao ni binadamu, walimu wameshachoka na kutothaminiwa maslahi yao ni ule uoga tu wa kutosema hadharani wakihofia kupoteza ata hako kibarua. Leo hii bora ya bwana afya anaweza pata posho ya kukagua nyama na akarudi na kilo ya nyama nyumbani, heri ya maaskari wenye posho kila mwezi, heri ya watumishi wengine wenye hadi marupurupu ya overtime.. Leo hii kwa shida anazonuka mwalimu tukitaka kuwavalisha kiatu hiki cha mwalimu watumishi wengine wa serikali basi lazima kiwabane tu.

Asilimia 100% walimu waliamini kuwa kupata Rais ambae ni mwalimu kungepelekea kuboreshewa maslahi yao na mazingira ya kazi kwani anayajua yote yaliyomo kwenye sekta ya ualimu lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa mpaka walimu wanawaza ni nani sasa atakuja kuwa mtetezi wao kama sio mwalimu mwenzao.! Mara nyingi Mh Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akisema kuwa serikali yake haitawaacha walimu (maneno ambayo yamezoeleka masikioni mwa walimu mwaka wa 6 huu) tena anaenda mbali kwa kusema kuwa yeye ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, waziri mkuu ni mwalimu, mkewe ni mwalimu, huku baraza lake la mawaziri likiwa limesheheni walimu mbalimbali, lakini yote haya haijawahi kamwe kuwa chachu ya kuthaminiwa maslahi ya walimu. Kiasi kwamba walimu sasa wanamkumbuka na kumlilia mh Kikwete kwa namna alivyokuwa akiwapandishia watumishi mishahara yao.

Mheshimiwa Rais Magufuli walimu wako wamekata tamaa na wamechoka na maneno yako ya matumaini yasiyozaa matunda kila siku kuwa serikali yako iko pamoja na walimu lakin wapi! kiasi kwamba wanafanya kazi ilimradi siku ziende tu lakini hawana motisha yoyote wanayoipata ili kufanya kazi kwa moyo wote. Tena walimu wako wanatamani muda wako wa kuongoza (kutawala) uishe ata kesho ili wabadilishe upepo angalau Raisi ajae anaweza kuwaona na kujali maslahi yao.

Mheshimiwa Rais John Magufuli ikikupendeza walimu nao wapate posho za kila mwezi kama maaskari ili iwe sehemu ya kuwapa motisha wachape kazi kisawasawa, na ni imani yangu walimu wakiwekewa utaratibu wa kupata posho walau laki mbili basi tutaingia katika Mapinduzi makubwa ya elimu mana walimu watafanya kazi kufa kupona na kutakuwa na ushindani na hari ya kufundisha. Mhe Raisi wahurumie Walimu wenzako wanashindwa kukwambia ukweli kwasababu wanakuogopa.

~Gai da Seboga (Mwalimu wa Kujitolea)
Posho ya askari haijumlishwi kwenye mshahara, wakati wa kulipwa pensheni mwalimu analipwa hela nyingi zaidi ya askari kulingana na daraja na cheo, kwa hiyo kama mwalimu anapokea sh laki 7 ujue ni sawa na askari maana askari anaweza akapokea laki 4 ukijumlisha na posho inakuwa laki 7 ile ile, mwalimu akitaka apewe posho maana yake atapewa laki 4 ili kilicho baki iwe posho, tofauti hapo tu ni pesa nyingine haina makato serikalini
 
Nimeishi na Dem Askar Askar nao njaa Kali tu asikudanganye mtu labda ubahatike uwe kitengo Cha barabaran au Doria za mara kwa mara hapo pesa ipo tofaut na hapo Ni hamna kitu maisha yao Ni sawa na Mwalimu tu ,coz jumla posho na mshahara kwa pamoja haivuk laki Saba wanachezea laki sita na vitoto na ukumbuke hiyo posho kwenye mafao haihesabik kabisa .
Kwa hy kama askari analipwa Tsh 650,000/= kwa mwezi na mwalimu analipwa Tsh 350, 000/=kwa mwezi ni kwamba hawako sawa mkuu.
 
Kwa hy kama askari analipwa Tsh 650,000/= kwa mwezi na mwalimu analipwa Tsh 350, 000/=kwa mwezi ni kwamba hawako sawa mkuu.
Mwalimu wa chet ndie analipwa 360 take home ila degree anayeanza Kaz Ni 716000 take home Ni laki tano na vitoto huko ,askar Hana mshahara wa kumzid Mwalimu hata yule wa chet tu wanaringana ,askar ana boostiwa na posho anayopata ambayo Ni around 300k lakin kwenye mafao askar hamgus mwalimu hata kidogo
 
Yaani unazungumzia hela utakayo kuja kuipata ukiwa na miaka 60?? Kweli walimu mna safari ndefu.
Uelewa wako ndio tatizo ,tumeshuhudia askar wengi wakistaf wanavyotia huruma ,na ingekuwa Haina maana hiyo kitu nadhn tusingeshuhudia askar kibao wakistaf na kukatalia kwenye kota za polisi.

Huwez kujua faida ya mafao pengine had uwe na mzaz ambaye ashapata mafao.

Wazaz wang wote wawil walikuwa walimu na wamestaf mzee alilamba 106m huku bimkubwa akilamba 102m na ukiwaona Bado Ni shupavu na wanachapa Kaz za shamban ambazo kwa vijana wa Sasa hawawez ,kwa hapo kwann mafao yasizungumziwe na Kwann yasionekane Yana faida kwa maisha ya baadae.

Turud kwa askar ambao tunao kitaa yaan ukimwona askar aliyestaf alaf ukamringanisha na mwalim hapo ndio utaelewa nn namanisha .kwa kifup askar walio weng wanamaliza vibaya Kaz zao huku walimu wakimakiza vizur baada ya utumish wao .
 
Walimu hawajielewi kbs,
wametumika kupora haki ya watanzania kwenye uchaguzi mkuu,
yaan mwl ukimhakikishia kusimamia mtihan wa taifa kwa mwak mara moja apate hiyo sh laki 1- 3 basi umemmaliza,
wabinywe hivyo hivyo ili muda wote wawepo kazin ili ufaulu uzid kupaaa,
ukiwap nafas ya kushik hela ,wepesi kujisahau na kuleta dharau.
 
Uelewa wako ndio tatizo ,tumeshuhudia askar wengi wakistaf wanavyotia huruma ,na ingekuwa Haina maana hiyo kitu nadhn tusingeshuhudia askar kibao wakistaf na kukatalia kwenye kota za polisi.

Huwez kujua faida ya mafao pengine had uwe na mzaz ambaye ashapata mafao.

Wazaz wang wote wawil walikuwa walimu na wamestaf mzee alilamba 106m huku bimkubwa akilamba 102m na ukiwaona Bado Ni shupavu na wanachapa Kaz za shamban ambazo kwa vijana wa Sasa hawawez ,kwa hapo kwann mafao yasizungumziwe na Kwann yasionekane Yana faida kwa maisha ya baadae.

Turud kwa askar ambao tunao kitaa yaan ukimwona askar aliyestaf alaf ukamringanisha na mwalim hapo ndio utaelewa nn namanisha .kwa kifup askar walio weng wanamaliza vibaya Kaz zao huku walimu wakimakiza vizur baada ya utumish wao .

Uko sahihi kabisa, hili nimeliona sehemu nyingi sana na kuna askari wastaafu wanaenda kuomba kazi za ulinzi kwenye makampuni ili kujikimu kimaisha hali zao huwa mbaya sana.
Wale wa vyeo vya juu wakistaafu hawachelewi kufa sijajua ni stress au tatizo nini
 
Mlishaambiwa mnamishahara mikubwa sana kushinda taasisi nyingine hivo hakuna haja ya kuwaongezea kwakuwa ninyi ni wazalendo namba moja kwa nchi yenu chapeni kazi acheni kutaka maslahi makubwa
 
Askari polisi mwenye elimu ya kidato cha nne:-kipato chake kwa mwezi ni kama ifuatavyo hapa chini:-

Basic salary ni Tsh.430,000/=
Posho ya chakula Tsh.300,000/=
Posho ya vinywaji Tsh.100,000/=
Posho ya mavazi Tsh. ............/=
Posho ya nyumba Tsh............./=

Bado unaweza kukuta askari huyu ni traffic barabarani,yupo idara ya upelelezi au katika vitengo vingine ambavyo sent nje ya mshahara haikosekani.

Hapo hujamgusa graduate wa jeshi la polisi!!Dah walimu tuna hali ngumu sana ndg zangu.
Walimu tumeshachokaa sasa, mana namba zote tumezisoma had za kirumi... Mwalm mwenzetu john atutazame kwa jicho la tatu.
 
Askari analipwa posho kwa sababu yuko kazini 24hrs na hii iko kwenye sheria zao imeandikwa kabisa.
Maana yake ni kwamba askari muda wowote akihitajika kazini anatakiwa kwenda, iwe ni mchana iwe ni usiku, yuko zamu hayuko zamu atatakiwa kuvaa uniform na kutekeleza majukumu aliyoitiwa muda huo.

Kwa mfano ile miezi ya mwisho wa mwaka ambayo walimu mnaenda sikukuu kada zote za uaskari likizo zote husimamishwa kwa sababu suala la ulinzi linakuwa muhimu sana wakati huo kwahiyo askari wanakuwa standby kwa 75%+.
Mwalimu ukishapiga kazi masaa yako 8 kwa siku unarudi home kucheza na watoto wako huoni ni scenario tofauti sana? Askari anakuwa zamu alaf muda wa kutoka anapewa amri ya kuongeza masaa hata kumi au 20 kazini au pengine siku kadhaa tena bado unaona mnafanana?
Kama ndivyo ilivyo kwanini huwa hamlipi nauli kwenye mabasi wakati Waalimu wanalipa??? Ukweli ni kwamba Askari siyo kama mnaheshimiwa bali mnaogopwa. Waalimu siyo kwamba wanachukiwa bali wanadharauliwa.
Matokeo yakitoka na selection kufanyika utasikia vp hujafanikiwa Post yeyote jamani hata ya Ualimu??
 
Askar hawez mfikia Mwalimu kwa mshahara Hilo Nina uhakika nalo kabisa .kinachomboost askar Ni ile posho ambayo kwenye mafao Haina madhara yoyote Yale .

So hapa kwa upande wa mafao mwalim lazima ampige gepu kubwa Sana askar ila nae askar anakuja mpiga gepu Mwalimu kwenye kaposho tu .

Take home ya askar anaeanza Kaz Ni around 350 wakat Mwalimu grade A 360,Diploma 450,bachelor 550 hizo Ni makadirio maana sijaweka visent .
Yan unazungumzia mafao ya kuja pokea ukiwa na miaka60? Tuna uhakika tutafika huko, tunataka maboresho yanayoendana na maisha ya sasa, na sisi tuvunje mifupa angali meno iko
 
Askari analipwa posho kwa sababu yuko kazini 24hrs na hii iko kwenye sheria zao imeandikwa kabisa.
Maana yake ni kwamba askari muda wowote akihitajika kazini anatakiwa kwenda, iwe ni mchana iwe ni usiku, yuko zamu hayuko zamu atatakiwa kuvaa uniform na kutekeleza majukumu aliyoitiwa muda huo.

Kwa mfano ile miezi ya mwisho wa mwaka ambayo walimu mnaenda sikukuu kada zote za uaskari likizo zote husimamishwa kwa sababu suala la ulinzi linakuwa muhimu sana wakati huo kwahiyo askari wanakuwa standby kwa 75%+.
Mwalimu ukishapiga kazi masaa yako 8 kwa siku unarudi home kucheza na watoto wako huoni ni scenario tofauti sana? Askari anakuwa zamu alaf muda wa kutoka anapewa amri ya kuongeza masaa hata kumi au 20 kazini au pengine siku kadhaa tena bado unaona mnafanana?
Naunga mkono hoja 101%
 
Back
Top Bottom